Dalton elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 207
- 453
Na Mwl, John Pambalu
Waswahili wanao msemo usemao kuwa, "Asiyejua aendako, njia yoyote itamfikisha anakokwenda". Ndiyo maneno mafupi ninayoweza kuyatumia kumuelezea Rais Samia ambaye mwanzoni alionyesha sura ya uungwana, udemokrasia na uadilifu lakini taratibu ameamua kuachana na mkondo huo na kulirejesha taifa kwenye mikono ya wahuni walioumiza watu katika taifa.
Mwanzoni mwa utawala wake alijitambulisha kwa falsafa ya 4R (reconciliation, resilience, reforms & rebuilding) akimaanisha Uputanishi, Ustahimilivu, Mabadiliko na Kujenga upya.
Kila Rais aliyejiandaa kuwa Rais alikuwa na falsafa yake ambayo aliitetea na kuipigania. Mwalimu aliamini kwenye ujamaa na kujitegemea, aliishi humo kwenye hiyo falsafa.
Mwinyi akaamini kwenye uhuru akatoa Ruksa ya watu kumiliki uchumi tofauti na ilivyokuwa wakati wa Mwalimu. Mkapa akaamini katika ujenzi wa taasisi akaanzisha karibuni taasisi zote mnazoziona. Mara TAKUKURU, TRA nk.
Kikwete akaamini katika Demokrasia, licha matukio kadhaa ya mashambulizi ya wakosoaji wa serikali kama mauaji ya Ally Zona, Daud Mwangosy nk, lakini angalau chaguzi za wakati wa Jakaya zilikuwa nzuri ukilinganisha na za wengine. Magufuli aliamini katika ujenzi wa vitu, kaacha vitu chungu mbovu mara Bwawa la Nyerere, Treni ya Mwendokasi nk.
Sasa ukiondoa kuuza bandari, kuwanyanyasa Wamachinga kwa kuwavunjia mali zao na kuwaumiza Wamasai na kuwanyan'ganya ardhi ambayo ni urithi wa vizazi vyao unafikiri liko jambo lipi jema Rais Samia atakumbukwa kwalo?
Awali yeye mwenyewe alisema anataka akumbukwe kwa 4R, yaani Upatanisho, Ustahimilivu, Mabadiliko na Kujenga upya. Awali alisema anawaondoa wahuni waliosababishia watu mateso na anakutana na wapinzani walioumizwa zaidi ili wazungumze kuhusu kulipatanisha taifa. Gafla akauacha huo mkondo na akaanza kuwapa nafasi za juu wakina Ramadhan Kingai, Biswalo na jana wakina Makonda.
Kwenye eneo la Ustahimilivu unagundua yeye Rais mwenyewe hana hata huo uwezo wa kustahimili ukosoaji. alikosolewa na Mhe. Mbowe akamtupa Segerea zaidi ya miezi 8, akakosolewa na Mwabukusi. Dr. Slaa na Mdude, wakatengenezewa kesi ya uhaini.
Sasa tunashuhudia attempts za wahuni kuja kuvuruga mikutano ya CHADEMA kule Mwanza na Tunduma. Tunarudi kule kule ambako washenzi walitupa mabomu na kuua watu kwenye mkutano wa CHADEMA Arusha.
Kwenye eneo Mabadiliko, alivyozungumzia tu mabadiliko. watu wakajua anamaanisha kubadili sheria kandamizi na kuleta katiba mpya, mwisho akaishia kusema katiba ni kitabu tu. Hatuandiki Katiba mpya ila watu wajifunze ile ya 1977 kwa kipindi cha miaka 3 kama wanatafuta bachelor ya Katiba.
Kwa kifupi Rais Samia hana anachokifanya ambacho kama angejiandaa kuwa Rais angeanza nacho kutokana na shauku ya kutaka kuwa Rais.
Amekuwa Rais kwa nasibu, anaendesha serikali yake kwa nasibu na ataliacha taifa kwa nasibu ikiwa poa, isipokuwa poa tu ilimradi yeye na wanae wanakula na kuishi kama wako paradise huku mamilioni ya Watanzania wakitokomea katika lindi la umasikini.
Rai yangu kwa Watanzania, taifa hupiganiwa na mabadiliko hayaji tu bali kwa mapambano yenye kujitoa sadaka kwa ajili ya maslahi ya wengi. Mwalimu Nyerere aliwahi kutuasa vijana kuwa, "Tunataka kuona katika Taifa hili vijana jeuri na wenye kujiamini; si vijana waoga akina "Ndiyo bwana mkubwa", vijana wenye ujasiri wa kuhoji na kupiga vita mifumo kandamizi, ubwana na ufisadi katika Taifa".
Wasalaam,
John Pambalu,
Mwanza-Tanzania.
jpambalu@gmail.com
23.10.2023