Niwasaidiaje kaka zangu?

Niwasaidiaje kaka zangu?

Kwahiyo Dada Jesca kuniomba msaada wa kukuunga JF sikuile ndio nia yako hii kuja kutusema na bora ungebadili User name nisiikujue, haya yote situngeyaongea kifamilia kumbuka sisi kakazako huwezi kutuweka hadharani hivi mtaji kweli ulinipa ila mdogo sana.
 
.... Pole sana bila shaka unamoyo wa upendo kwandugu zako huko kwenu kskazini mnatabia za kukaa na wamama Nawababa nyumbani mnawaita watoto bado sisihuku kwetu kusini ukisha barehe unaonyeshwa kaeneona myanzi ilipo hapo umeazimwa ukimaliza shule hakuna was kukupa mtaji utajiongeza mwenyewe mambo yakianza kuku bana hakuna wakukupa sabuni wars shati wala wala jembe na baba akijua umekua huwa anaanza ulinzi kwenyeshamba lake LA kokoa hataki utani.hapo anakupiga tumajungu utaskia araa umekuwa mwanangu naona ndevu zimekuwa kama nywele"afu uko piii. Owa bwana.utakapo mwamvia baba sins Hera ndo anakupa makavu hapo hapo kwamba hapo unapo kaa nikwangu tafuta Hera ununue pakwako.kuanzia Leo noskuone unakuja kuvonge ugali humu huu ugali wakwangu Mimi na nama yako full stop."" Sasa hapo mtoto wakiume unaanza kujiuliza hivi yule lama niliye soma nae yukowapi?? Basis utapambana utajua yuko wapo mishegani kama madini mkokoteni nk unajichanganya huko mungu anabaliki unapata michongo maisha yanaenda. Kwahiyo kumsaidia saana MTU wakatimwingine unamhalibu punguza kiwango chamboga punguza shobo nao watajiongeza wenyewe unajua motto wakiume niwakiumetu ataondoka kwa kukuchukia akifanikiwa ataludi nakitenge na ahsante nhingi

Duh kiswahili ni lugha yako ya ngapi?
 
Habari zenu ndugu zangu!

Mimi ni mdada at my early 20’s. Na ni mtoto wa mwisho na wa kike katika familia yetu nikiwa na kaka zangu wawili mmoja early 30’s mwingine late 20’s. Katika familia yetu mimi ndiye niliyefanikiwa kufika hadi degree nawashukuru wazazi wangu waliweza kunipigania na juhudi zangu pia. Ila kaka zangu mmoja alifanikiwa kufika diploma tu.

Familia yetu ilipitia changamoto nyingi sana sana za kuumiza lakini nashukuru Mungu tupo hai mpaka sasa. Na Mungu kanijalia kazi nzuri, ninajitegemea na kusaidia ndugu zangu pale niwezapo. Nilianza kazi mwaka jana mwezi wa Tano, nikasave nikafanikiwa kununua kiwanja na kufikia hadi hatua ya kuweka msingi! Niliamua kufanya hivyo kwasababu familia yetu hatujawahi kuwa na nyumba yetu wenyewe ya kumiliki! Kwahiyo ni kitu kilichokuwa kinanipa wasiwasi sana vipi siku kikitokea cha kutokea tutaenda wapi? Hivyo nikalipa lengo langu hilo priority.

Lakini sasa kaka zangu bado wanabangaiza vibarua walivyo navyo vinawasaidia kula na nauli za kwenda vibaruani na mara nyingine hata inanibidi niwape mimi hata hela ya nauli na ya kula! Na ilifika kipindi cha kulipa kodi basi nitoe yote au niwachangie! Hili sio tatizo maana najua Mungu kanipa uwezo ili niwasaidie ndugu zangu.

Swali ni ‘niwasaidiaje kakazangu?’ ili waweze kusimama vizuri kiuchumi? Maana mmoja tulishawahi kumchangia mtaji lakini biashra ikawa ngumu ikafeli. Mwingine hana passion na biashra na haiwezi tu niseme ila kibarua chake ni cha kipato kidogo sana. Wanashindwa hata kuoa kwasababu hawako vizuri kiuchumi. Kiukweli naumiaga sana na ni kama inaniongezea depression nikiwafikiria! Kuna wakati nakwama lakini najua sina ndugu wa kumuomba msaada naumia sana!

Sasa naomba mnisaidie ushauri na maoni, niwasaidieje? Je, ina maana mimi kuendelea na ujenzi ilihali ndugu zangu hawako vizuri kiuchumi? Natamani nichukue mkopo niwape kwaajili ya biashara lakini vipi zikifeli maana tayari ilishafeli! Je, ni sawa kuwawazia sana?

Samahani kwa kuwachosha! Natanguliza shukrani.
Pole sana mdogo wangu. Mungu awatie nguvu
 
Mwalimu wetu wa physics form two sijui alikua anafundisha topic gani akatuambia ili rocket ipae inahitaji ukinzani wa hali ya juu sana kisha akaendelea akili ya binadamu ni kama rocket ili ifanye kazi inatakiwa ibanwe kisawasawa na kuanzia hapo alitupeleka mchakamchaka mpaka wengine walikimbia somo lake

Sasa nachotaka kusema hapa ni kwamba hao kaka zako acha kuwadekeza we wakatie mirija kabisa ikiwezekana hata wakikupigia simu usipokee badili namba kabisa kisha fanya mambo yako ya msingi haiwezekani dume zima at age of 30 unalilipia kodi na hela ya nauli unalipa litajiongeza saa ngapi sasa

We kata misaada fanya mambo yako wangekua wa kike kidogo inge make sense
 
Habari zenu ndugu zangu!

Mimi ni mdada at my early 20’s. Na ni mtoto wa mwisho na wa kike katika familia yetu nikiwa na kaka zangu wawili mmoja early 30’s mwingine late 20’s. Katika familia yetu mimi ndiye niliyefanikiwa kufika hadi degree nawashukuru wazazi wangu waliweza kunipigania na juhudi zangu pia. Ila kaka zangu mmoja alifanikiwa kufika diploma tu.

Familia yetu ilipitia changamoto nyingi sana sana za kuumiza lakini nashukuru Mungu tupo hai mpaka sasa. Na Mungu kanijalia kazi nzuri, ninajitegemea na kusaidia ndugu zangu pale niwezapo. Nilianza kazi mwaka jana mwezi wa Tano, nikasave nikafanikiwa kununua kiwanja na kufikia hadi hatua ya kuweka msingi! Niliamua kufanya hivyo kwasababu familia yetu hatujawahi kuwa na nyumba yetu wenyewe ya kumiliki! Kwahiyo ni kitu kilichokuwa kinanipa wasiwasi sana vipi siku kikitokea cha kutokea tutaenda wapi? Hivyo nikalipa lengo langu hilo priority.

Lakini sasa kaka zangu bado wanabangaiza vibarua walivyo navyo vinawasaidia kula na nauli za kwenda vibaruani na mara nyingine hata inanibidi niwape mimi hata hela ya nauli na ya kula! Na ilifika kipindi cha kulipa kodi basi nitoe yote au niwachangie! Hili sio tatizo maana najua Mungu kanipa uwezo ili niwasaidie ndugu zangu.

Swali ni ‘niwasaidiaje kakazangu?’ ili waweze kusimama vizuri kiuchumi? Maana mmoja tulishawahi kumchangia mtaji lakini biashra ikawa ngumu ikafeli. Mwingine hana passion na biashra na haiwezi tu niseme ila kibarua chake ni cha kipato kidogo sana. Wanashindwa hata kuoa kwasababu hawako vizuri kiuchumi. Kiukweli naumiaga sana na ni kama inaniongezea depression nikiwafikiria! Kuna wakati nakwama lakini najua sina ndugu wa kumuomba msaada naumia sana!

Sasa naomba mnisaidie ushauri na maoni, niwasaidieje? Je, ina maana mimi kuendelea na ujenzi ilihali ndugu zangu hawako vizuri kiuchumi? Natamani nichukue mkopo niwape kwaajili ya biashara lakini vipi zikifeli maana tayari ilishafeli! Je, ni sawa kuwawazia sana?

Samahani kwa kuwachosha! Natanguliza shukrani.
Sikia dada,hutaweza kuwaondoa kaka zako kwenye mduara wa umaskini hata kidogo,chakufanya wewe jenga msingi wa maisha yako,na wape msaada mkubwa wazazi wako kwa kadri ya uwezo wako,hao kala zako,hebu waache kwanza wapambane na hali yao,usiwalipie kodi,unawaharibu,hawatatafuta kwakuwa wanajua wewe upo
 
USHAURI WA BURE
Jenga kwanza alafu katk kujenga kwako kama unawez weka mabanda ya mifugo na fremu za biashara
Ukimalza Jenga ita Hao kaka zako wafuge na wafungue biashara wazisimamie kabla hujaolewa
Ukiwa na bwana usimpelekw apo kwako waheshimu kaka zako.
Kwa maelezo zaid njoo INBOX
 
Hapo tumia Elimination Method.​
Let X = Nyumba​
y = Kaka zako​
Halafu ondoa Kaka zako solve for X then malizia kusolve y.​
Application ya symliteneous equation kwenye real life ndo inatumika hapa.​
 
Habari zenu ndugu zangu!

Mimi ni mdada at my early 20’s. Na ni mtoto wa mwisho na wa kike katika familia yetu nikiwa na kaka zangu wawili mmoja early 30’s mwingine late 20’s. Katika familia yetu mimi ndiye niliyefanikiwa kufika hadi degree nawashukuru wazazi wangu waliweza kunipigania na juhudi zangu pia. Ila kaka zangu mmoja alifanikiwa kufika diploma tu.

Familia yetu ilipitia changamoto nyingi sana sana za kuumiza lakini nashukuru Mungu tupo hai mpaka sasa. Na Mungu kanijalia kazi nzuri, ninajitegemea na kusaidia ndugu zangu pale niwezapo. Nilianza kazi mwaka jana mwezi wa Tano, nikasave nikafanikiwa kununua kiwanja na kufikia hadi hatua ya kuweka msingi! Niliamua kufanya hivyo kwasababu familia yetu hatujawahi kuwa na nyumba yetu wenyewe ya kumiliki! Kwahiyo ni kitu kilichokuwa kinanipa wasiwasi sana vipi siku kikitokea cha kutokea tutaenda wapi? Hivyo nikalipa lengo langu hilo priority.

Lakini sasa kaka zangu bado wanabangaiza vibarua walivyo navyo vinawasaidia kula na nauli za kwenda vibaruani na mara nyingine hata inanibidi niwape mimi hata hela ya nauli na ya kula! Na ilifika kipindi cha kulipa kodi basi nitoe yote au niwachangie! Hili sio tatizo maana najua Mungu kanipa uwezo ili niwasaidie ndugu zangu.

Swali ni ‘niwasaidiaje kakazangu?’ ili waweze kusimama vizuri kiuchumi? Maana mmoja tulishawahi kumchangia mtaji lakini biashra ikawa ngumu ikafeli. Mwingine hana passion na biashra na haiwezi tu niseme ila kibarua chake ni cha kipato kidogo sana. Wanashindwa hata kuoa kwasababu hawako vizuri kiuchumi. Kiukweli naumiaga sana na ni kama inaniongezea depression nikiwafikiria! Kuna wakati nakwama lakini najua sina ndugu wa kumuomba msaada naumia sana!

Sasa naomba mnisaidie ushauri na maoni, niwasaidieje? Je, ina maana mimi kuendelea na ujenzi ilihali ndugu zangu hawako vizuri kiuchumi? Natamani nichukue mkopo niwape kwaajili ya biashara lakini vipi zikifeli maana tayari ilishafeli! Je, ni sawa kuwawazia sana?

Samahani kwa kuwachosha! Natanguliza shukrani.
Mkuu,hongera sana kwa kuwa na hekima.Kaka zako hawahitaji msaada wa kifedha,wala mtaji.Wanahitaji kuwa challenged-JENGA KABISA MJENGO uliokamilika wa maana.KOPA FUNGUA BIASHARA YAKO USIMAMIE IKUE,TAFUTE MUME MWENYE BUSARA ALETE POSA ANATAKA KUKUOA.

Fanya mambo makubwa mpaka wao waje kwako watake ushauri,msaada.USIWAPE NAULI WALE ELA YA KULA ISPOKUWA KAMA WANAUMWA.Kama ni njaa wacha wajifunze kuishi kwa bajeti yao.

Huo ni mtazamo wangu na ushauri wangu kwako.Kama unahitaji ushauri zaidi wa namna ya kwasaidia basi karibu PM
 
Mtoto wa kiume ashiki mimba...

Mtoto wa kiume mwache mwenyewe ajitume...

Mtoto wa kiume maisha yanavyomchapa ndo na akili hufunguka...

Concentrate na wazazi, hao ndugu zako uzuri ni wakiume ipo sku akili zitawakaa sawaa tuu na watazishika kuliko wewe na kuwasahau wazazi...
 
Kwakuwa Unapambana Upate Nyumba Iwe Msaada
Naona Ungetia Juhudi Kwenye Nyumba Ikamilike
Kwakuwa Uwezo Wako Ni Mdogo, Ukiwa Hutaweza Kumaliza Hiyo Nyumba

Halafu Maisha Yanakwenda Kasi Hakabadilika Wakati Wowote
Yanaweza Kuwa Mazuri/Mabaya. Jenga Nyumba
 
Kama sijakuelewa kaka! Kwamba nimejivuna au? Hali yoyote niliyoielezea hapo ni ili tu mpate picha halisi ilivyo ningeficha vingine cdhani kama ningeeleweka! Na wala sina majivuno kabisa! Km nimekukwaza pole
We achana naye huyo wamezoea kuiba ng'ombe, majangiri kwa kifupi uelewa wa ni mrefu kwenda chini.
 
Je wazazi wako hai? Huna obligation ya kuwabeba kaka zako. Unachoweza ni kusaidia kuwapatia uwezo wakujitegemea. Ask them what they need for them to stand on their own feet. Do not impose. If possible involve your parents. Karibu utakuwa na mji wako ie your own family na utashindwa ku sustain kusaidia kaka zako.
 
Malizia ujenzi..kwanza..
Unaweza fanya biashara za nyumbani kama kufuga kuku ..faida unagawana nao
Na wao wanapata uzoefu wa kufanya hizo biashara...

Unakuwa unawaonesha njia taratibu..
Lakini kujenga usiache...nyumba pia ni biashara
Ukiamua kuuza na kujenga ingine utapata pia faida ya kujenga hata mbili....

Nenda nao taratibu
Biashara zote zinahitaji uzoefu..

Kingine unaweza mtafutia kibarua kwenye biashara ambayo anaonesha interest..
Ataenda jifunza hadi aweze ifanye mwenyewe..

Tatu unaweza waambie watafute partnership
Na wanaojua biashara wajifunze mdogo mdogo
Jibu zuri sana
 
Yaani Jesca sikujua kama una tabia ya kuwasimanga ndugu zako hadi JF. Kwani Geoffrey alikosea kukuelekeza namna ya kujiunga JF hadi uje umsimange namna hiyo?
 
Back
Top Bottom