Alvin Slain
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 6,375
- 3,665
Ndugu hawabebeki, Hata ukuwabeba watasema umewabeba vibaya, Angalia future yako.

Jisaidie wewe mwenyewe ujenge nyumba kwanza, umalize, uwe na uwezo wa kusaidia wengine vizuri zaidi.
Sasa hivi itakuwa ngumu kuwakacha ghafla wewe chakufanya sitisha kwanza ujenzi kwa muda alafu tafuta kisingizio chochote kwamba kazini Mambo yameharibika na wewe iliye njaa utaone wenyewe wanajiweka pembeni na wewe maana asali imekata, wakati huo unachokipata unakitunza na wazazi unawasaidia kwa shida shida yaani wote muingie kwenye msoto, baadaye Sasa unaweza kujifanya Kuna sehemu umepata mkopo ukajenga haraka kwa ajili ya wazazi.
acha ufala we msagane kwan wakurya wao hawapendi sifa kwakua co bnadamu auHakuna 'Mkurya' Mjivuni ( Majipu ) na Mshamba ( Mbwiga ) hivyo Mkuu. Huyo nahisi atakuwa ni ama Mhaya au Mjita na pengine akawa ni Mjaluo.
Ila first born huwa wanawajibika sana kwenye kusaidia familia zao hata ukoo pamoja na changamoto za kiroho zinazowakabili. Cha kushangaza hata madogo wakiwa wametusua bado watamwangalia kwa kila kitu ikiwemo kushughulikia changamoto za wazazi na shida zote za familia, wao kazi yao ni kula bata na lawama kibao.Mtoto wa kwanza ana vita kubwa sana ya kiroho ila kwa leo sitozungumzia hilo....ila Shetani anapenda kuwaharibia future sana watoto wa kwanza kwa kuwa anajua kwamba mtoto wa kwanza akifanikiwa basi kwa wanaofuata huwa ni rahisi....Lichunguze hilo....Nimesema hivyo kumaanisha kuwa wewe ndie umebahatika na unaeweza kurejesha amani tena kwenye familia hivyo Focus kutengeneza maisha yako kwanza huku ukimuomba MUNGU akuongoze utimize hilo kwa haraka then ndio uangalie utaratibu wa kutengeneza ya hao wa nyuma yako....Hapo ukicheza vibaya mtajikuta level moja japo unasema una elimu maana hiyo vita ni ya Shetani
Achana na ndugu, nasema hivi achana na ndugu mdogo wanguHabari zenu ndugu zangu!
Mimi ni mdada at my early 20’s. Na ni mtoto wa mwisho na wa kike katika familia yetu nikiwa na kaka zangu wawili mmoja early 30’s mwingine late 20’s. Katika familia yetu mimi ndiye niliyefanikiwa kufika hadi degree nawashukuru wazazi wangu waliweza kunipigania na juhudi zangu pia. Ila kaka zangu mmoja alifanikiwa kufika diploma tu.
Familia yetu ilipitia changamoto nyingi sana sana za kuumiza lakini nashukuru Mungu tupo hai mpaka sasa. Na Mungu kanijalia kazi nzuri, ninajitegemea na kusaidia ndugu zangu pale niwezapo. Nilianza kazi mwaka jana mwezi wa Tano, nikasave nikafanikiwa kununua kiwanja na kufikia hadi hatua ya kuweka msingi! Niliamua kufanya hivyo kwasababu familia yetu hatujawahi kuwa na nyumba yetu wenyewe ya kumiliki! Kwahiyo ni kitu kilichokuwa kinanipa wasiwasi sana vipi siku kikitokea cha kutokea tutaenda wapi? Hivyo nikalipa lengo langu hilo priority.
Lakini sasa kaka zangu bado wanabangaiza vibarua walivyo navyo vinawasaidia kula na nauli za kwenda vibaruani na mara nyingine hata inanibidi niwape mimi hata hela ya nauli na ya kula! Na ilifika kipindi cha kulipa kodi basi nitoe yote au niwachangie! Hili sio tatizo maana najua Mungu kanipa uwezo ili niwasaidie ndugu zangu.
Swali ni ‘niwasaidiaje kakazangu?’ ili waweze kusimama vizuri kiuchumi? Maana mmoja tulishawahi kumchangia mtaji lakini biashra ikawa ngumu ikafeli. Mwingine hana passion na biashra na haiwezi tu niseme ila kibarua chake ni cha kipato kidogo sana. Wanashindwa hata kuoa kwasababu hawako vizuri kiuchumi. Kiukweli naumiaga sana na ni kama inaniongezea depression nikiwafikiria! Kuna wakati nakwama lakini najua sina ndugu wa kumuomba msaada naumia sana!
Sasa naomba mnisaidie ushauri na maoni, niwasaidieje? Je, ina maana mimi kuendelea na ujenzi ilihali ndugu zangu hawako vizuri kiuchumi? Natamani nichukue mkopo niwape kwaajili ya biashara lakini vipi zikifeli maana tayari ilishafeli! Je, ni sawa kuwawazia sana?
Samahani kwa kuwachosha! Natanguliza shukrani.
Kwahiyo Dada Jesca kuniomba msaada wa kukuunga JF sikuile ndio nia yako hii kuja kutusema na bora ungebadili User name nisiikujue, haya yote situngeyaongea kifamilia kumbuka sisi kakazako huwezi kutuweka hadharani hivi mtaji kweli ulinipa ila mdogo sana.



Ile roho ya kimaskini ndio inajidhirisha ndani ya comment yako hii. We mtu kusaidia kuwainua kaka zake unaona gere? Acha wivu wa kichawi mkuu!!!kusaidia ndugu ni kazi sana.
kwanza hawanaga shukrani
jengea wazee nyumba ,na wewe endelea na mambo yako
hao wakaka watakuja kukuingiza chaka hautakuja kuamini kama ni ndugu zako