Niwafanye nini hawa watu..?

Watoto wanasoma dear mmoja Bado mdogo hajaanza shule.nikiwachukua nitavuruga utaratibu wao na kwasasa nitakua Sina pa kuwaweka sijaandaa mazingira .. ..pia baba aone umuhimu wangu ...alishawahi kutamka "kulea kitu gani" kwahiyo zamu yake imefika
Hivyo unataka kumuacha mtoto wa under 5 kisa tu kumkomesha baba yake?🤔 Au mimi sijakuelewa
 
Wakati nasubiria huo utaratibu WA kimahakama nataka niwe nje ya mfumo .
Jambo jema kabisa , asije akakuua huyo mwehu maana ni kama Kuna mahali nimeona umesema alikupiga na kukufungia nje

Unawezaje kumpiga na kumfungia nje baby mama wako na usiwe mwehu
 
Hivi ukiondoka unachokitaka utakipata nje au unaona single mother wanafaidi nje

Kaza mwanamke ndoa sio lele mama hivyo zungumza nae zaidi shirikisha mtu wa bus busara baina yenu mkae sawa
Nimeshawahi kuwashirikisha ndugu zake mara kadhaa..nimeona najichoresha tu huku hakuna mabadiliko nimeamua kukaa kimya nipambane na Hali yangu.

Vipi nikibaki na Hali izidi kuwa mbaya?
 
Jambo jema kabisa , asije akakuua huyo mwehu maana ni kama Kuna mahali nimeona umesema alikupiga na kukufungia nje

Unawezaje kumpiga na kumfungia nje baby mama wako na usiwe mwehu
Si ndo hapo? Tatizo la baadhi ya WATU Huwa hawashughuliki na chanzo wanashughulika na matokeo..

Ndio alinipiga Tena alijisifu kabisa " ningempiga achakae awe kama kagongwa na boda" duh! Alafu huyohuyo unalala naye anakupa utamu na kukuzalia ukoo wako.. mmh
 
Asante kwa mafundisho Yako mkuu
 
Kama unahitaji kuondoka ondoka tu ila isiwe kwa ajili ya kuwaumiza, ukute wenyewe wanaona unawabana wewe nenda ufanye maisha yako unavyoona inafaa
 
Ni masikitiko kwakweli . Kuna siku alitamka... " Nitakuja kukufanyia kitu Cha kishenzi " mmmh Bado tu nisubirie kuja kutangazwa kwa kina Millard?
 
Reactions: ABJ
na mimi nikaanza kupunguza upendo taratibu kwake nikahamishia mapenzi kwa watoto wangu,kazi na kuanzisha biashara zangu
Unatuonaje wewe?

Enewei,

Pole sana kwa maumivu ya miaka mingi unayopitia. Umekuwa jasiri sana kusimama imara kwa ajili ya watoto na uchumi wako.

Uamuzi wako wa kuondoka na kumuacha mume na watoto ni wako na unastahili kuheshimiwa. Hata hivyo, kuhusu mpango wako wa kumtesa kisaikolojia na kuwalizisha pesa, naomba ufikirie kwa makini tahadhari hizi ili usijiumize mwenyewe.

Hatari ya Kisheria na Kiusalama

Ukichukua fedha zao kwa mitego, vitisho (blackmail), au utapeli kwa kutumia ushahidi ulio nao, wanaweza kukushtaki kisheria na kukuharibia kazi au biashara zako. Pia, mume mwenye historia ya kukupiga anaweza kuwa na hasira za kikatili na kukudhuru kimwili akigundua umemchezea mchezo wa fedha.

Kisasi Kinakuchelewesha Kupona

Kupanga kisasi kinawapa wao nguvu ya kuendelea kutawala akili yako. Kisaikolojia, hakuna uhakika kama watateseka kama unavyotaka wewe.

USHAURI WANGU NI,

Ondoka kwa utulivu mkubwa

Siku unayoondoka, usigombane wala usipige kelele.

Acha Ushahidi

Chapisha (print) zile screenshot za usaliti wao, ziweke juu ya meza, na uambatanishe na ujumbe mfupi: "Asante kwa miaka 10. Nilijua kila kitu, na sasa nakuachia nafasi uishi kwa uhuru. Simtaki tena mume wa mtu mwingine."

Kata Mawasiliano

Block namba zao zote. Ukimya huu wa ghafla bila kuwapa nafasi ya kujitetea humtesa msaliti kisaikolojia kuliko kitu chochote.

Dai Chako Kisheria

Kwa kuwa mna miaka 10 ya ndoa (sheria inatambua mchango wako), tumia mwanasheria kudai mgawanyo wa mali mlizochuma pamoja. Hili litamnyong'onyeza kiuchumi kisheria bila wewe kuvunja sheria.

Kisasi kikubwa zaidi kwa watu waliokudharau ni wewe kufanikiwa, kung'ara, na kuwa na furaha tele bila wao. Una kazi na biashara zako hadi hapo umeshawashinda!
 
Chart na chat ni maneno mawili tofauti yenye maana mbili tofauti.
 
Mkuu vipi ukijua mwanamke wako anakusaliti utalichukuliaje?
 
Hadi unafikia kutaka kuchukua huo uamuzi wa kuondoka na kumuachia watoto, ni kwamba huna wazazi/walezi wa pande zote wa kwenda kuwapelekea haya malalamiko yako ili muitwe na kufanya kikao cha maamuzi? Huna viongozi wako wa kiroho wa kuwashirikisha ili upatikane muafaka?

Kisa una kazi unaona ni sahihi kwako kuondoka na kwenda kuanza maisha mapya huku ukiwaacha watoto wako kwenye mkwamo wa kukosa malezi ya wazazi wote wawili!
Unafikiri ukiondoka kwa huyo mume wako mwenye mchepuko, siku ukapata bwana mwingine atakuwa ni mkamilifu?

Kwa taarifa yako wanaume wasiochepuka ni 1/100!! Au hatimizi majukumu yake kama baba wa familia?
 
Nimeshawahi kuwashirikisha ndugu zake mara kadhaa..nimeona najichoresha tu huku hakuna mabadiliko nimeamua kukaa kimya nipambane na Hali yangu.

Vipi nikibaki na Hali izidi kuwa mbaya?
Ninyi ni watu wazima mpaka sasa angalieni mstakabari wa damu zenu hizo
 
Dada Yang mimi nitakushauri;

KISASI SIYO DHAMBI

Kama huyo dada mchepuko ana mme bas anza kutoa uroda kwa mmewe ikibidi mpe na zawad nzuri ya mtoto.
Halafu mwambie mmewe kwamba mkewe anachakatwa na mme wako.

Halafu ondoka zako na Bendera ya ushindi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…