Niwafanyaje watu hawa wakuu mnisaidie.

Niwafanyaje watu hawa wakuu mnisaidie.

charger

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2010
Posts
2,320
Reaction score
1,374
Habari ya asubuhi/mchana/jioni wakuu.Bila kupoteza muda.

Ninaishi kwenye nyumba ya kupanga maeneo ya Tandale-popobawa.Sasa kama unavyojua nyumba zetu za uswahilini hazina dari jambo ambalo linakulazimu usikilize taarifa ya habari ya chumba jirani hata kama hutaki.

Kuna,jirani ninayepakana naye na mkewe wanakoroma sana usiku.Wanaanza taratibu kwa kupokezana kama kwaya flani na ikifika mida ya saa 6 usiku hali inakua mbaya sana.Mama anapiga kibwagizo kama generator inataka kuzima kisha baba anapokea kama bedford ya mkaa inapanda kitonga.Wakati mwingine inanilazimu niwastue kwa kudondosha kitu chumbani kwangu,basi hapo wanastuka kwa sekunde kadhaa ila sasa wakirudi wanaanza kwa mpigo na kwa nguvu zaidi.

Hapa niko maeneo ya airport kuna jamaa yangu najaribu kuona kama ntapata vile vifaa wanavyovaaga masikioni wakati wa kuongoza ndege.

Naombeni mnisaidie mawazo ndugu zangu.
 
Si utafute chumba maeneo mengne,au kama umezoeana na jamaa mwambie awe anapunguza volume wanapoanza kukoroma
 
Si utafute chumba maeneo mengne,au kama umezoeana na jamaa mwambie awe anapunguza volume wanapoanza kukoroma

Jamaa ni baunsa najishauri kumwambia.
 
Jamaa ni baunsa najishauri kumwambia.
Tafuta hela uongee na mwenye nyumba muelewane upige dari kwenye chumba chako kama umeyapenda maeneo,bila ya kumsumbua mtu!
 
Ha ha ha ha ha haaa, kazi unayo!!ndo shida ya vyumba visivyo na dari!!km vp hama hiyo nyumba.sasa bora hapo ni kukoroma kwa usingizi tu, mie niliwai kuishi kwenye nyumba ya aina hiyo mtihani ni pale jirani yngu mmoja wanapogegedana na mkewe ni balaa tupu, kelele mtindo mmoja!! inakulazimu kuzuga na radio kwa sauti ya juu mpaka wamalize.
 
Hiyo nyumba si umepanga......ingekuwa yako tungekuwa tunajadili mengine

waache wale raha zao kama unakereka we HAMA..........
 
Ha ha ha ha ha haaa, kazi unayo!!ndo shida ya vyumba visivyo na dari!!km vp hama hiyo nyumba.sasa bora hapo ni kukoroma kwa usingizi tu, mie niliwai kuishi kwenye nyumba ya aina hiyo mtihani ni pale jirani yngu mmoja wanapogegedana na mkewe ni balaa tupu, kelele mtindo mmoja!! inakulazimu kuzuga na radio kwa sauti ya juu mpaka wamalize.

Ngoja niwinde hiki kifaa cha masikioni kinaweza kunisaidia mkuu.
 
Tafuta hela uongee na mwenye nyumba muelewane upige dari kwenye chumba chako kama umeyapenda maeneo,bila ya kumsumbua mtu!

Hiyo nayl ni njia ya kuondokana na usumbufu. Anyway the best option ni kuhama kama vipi.
 
Ngoja niwinde hiki kifaa cha masikioni kinaweza kunisaidia mkuu.

Dawa nikuhama kaka au km unaweza gharamia kuweka board, laa sivyo utaendelea tu kupata tab bila sabab yamsingi ukizingatia ni nyumba yakupanga tu!au una maslahi binafsi kwenye hiyo nyumba nini?
 
Hiyo nayl ni njia ya kuondokana na usumbufu. Anyway the best option ni kuhama kama vipi.

Hapa nalipa kodi 3,000/- kwa mwezi ntapata wapi chumba cha bei hiyo?mjini kuzuri na mimi sitaki kuhama?
 
Mkuu umesema upo maeneo ya uwanja wa ndege kutafuta kifaa kile cha kuvaa ukiongoza ndege. Hilo ndio wazo muafaka. Kabla hujalala uvae. utasahau jirani yako. Chonde chonde mwanetu, usipokee vifaa vya wizi. Mwakyembe akikukamata, lile linyakyusa halina mchezo. Limetoka Mwakaleli na liliaga kwao. Wakalitupia ndumba ikagoma. Hali rushwa yule hivyo
Uombe chumba pale Segerea kabisa. Nafuu uhame huliko kununua vyombo vya wizi vya Mwakyembe ndg.
 
hama km vimezidi au ongea na mwenye nyumba muweke silingi bodi ili kero iishe...pole sana
 
Its you charger ? hahaha! Wacha nijionee!!
 
Last edited by a moderator:
Unaskia wakikoroma tu!! Tuhadithie na vyengine unavyovisikia
 
Mkuu umesema upo maeneo ya uwanja wa ndege kutafuta kifaa kile cha kuvaa ukiongoza ndege. Hilo ndio wazo muafaka. Kabla hujalala uvae. utasahau jirani yako. Chonde chonde mwanetu, usipokee vifaa vya wizi. Mwakyembe akikukamata, lile linyakyusa halina mchezo. Limetoka Mwakaleli na liliaga kwao. Wakalitupia ndumba ikagoma. Hali rushwa yule hivyo
Uombe chumba pale Segerea kabisa. Nafuu uhame huliko kununua vyombo vya wizi vya Mwakyembe ndg.

Mkuu mangatara mbona unanitisha sasa?na hapa ni karibu kabisa na segerea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom