Niwaepushaje hawa na hili?

Niwaepushaje hawa na hili?

Wewe tafuta hata namba mpya mtumue msg huyo dada


Kuwa huruma ya kibinadamu kwa huyo malaya haitampunguzia lolote atatafuta mwingine.
 
Habari za humu wanaJF?
Bila kuwachosha naomba niende moja kwa moja kwenye lengo la uzi huu.

Kuna jamaa (tunafanya nae kazi) pia ni rafiki yangu tunaishi nae ghetto moja.
Juzi katika kufanya usafi kwenye room nilikuwa naamisha mabegi naweka sebuleni ili nifanye intensive cleanness kuna kadi ya kliniki ya matibabu ya ARV niliiona, baada ya kuisoma nimegundua kuwa jamaa ni muathirika wa VVU na mbaya zaidi jamaa anatumia ARV kama mwaka wa 6 sasa. Hii sio shida maana kuumwa ni sehemu ya maisha ya yyte aliyezaliwa na mwanamke.

Kinachonisukuma kuwaomba ushauri ni juu ya tabia ya huyu jamaa. Yaani jamaa ni mchakataji mzuri wa papuchi hapa mtaani. Habagui barmaids wala waimba kwaya. Mbaya zaidi ni kiongozi kwenye kwaya yao na huwa naona anavusha baadhi ya waimba kwaya na watoto wa shule.

Hili ni tatizo ila mbaya zaidi kuna binti flani wanamiadi ya kukutana kesho kutwa; maskini binti wa watu namhurumia sana maana jamaa kwa anavyojitapa kuwa hatumii kinga yeye ni nyama kwa nyama. Natamani nimwambie huyu binti ila nakosa lugha nzuri ya kumwambia na ukizingatia binti huyu anatarajiwa kuolewa soon maana ndoa yake imeshatangazwa kwa mara ya kwanza kanisani.

Utata mwingine unakuja kwa sababu nahisi kumwambia huyu dada ukweli ni sawa na kumsaliti jamaa maana ugonjwa ni siri. Na kama hakuwahi nambia kwa miaka yote hiyo hii inamaanisha hataki yyte ajue.

Namshukuru Mungu; ameniepusha na wadada anaotembea nao...mimi sina tabia ya uhuni japokuwa huwa naona rafiki zangu wengine wanagonga mashemeji(mademu wa marafiki zako) .

Naombeni ushauri katika hili, na nitumie mbinu gani kumuepusha huyu binti.

NB: Ukimwi bado upo; Mungu atusaidie; tuepuke ngono haramu.

ASANTENI.
Sikia hili ni jambo rahisi sana,muokoe huyo dada kwa kumwambia ukweli oki aziugue na baadae mwambie jamaa yako huyo kuwa uliokota kadi yske ya kliniki na umeona kuwa anaumwa hiv
 
Hata kisheria anachofanya huyo rafiki yako ni kosa na kama utamuacha aendelee na hiyo tabia atakuja kuambukiza na mkeo Wa baadae na Dada zako pia kwa uzembe wako Wa kutosema ukweli. Chakufany mtafute huyo mdada mwambie kua unajua kwamba anataka kwenda kungonoka na jamaa wakati harusi iko njiani na km akifanya hivyo utasema kwa uongozi Wa kanisa.
Na kama jamaa akikuuliza kuhusu kumuharibia, basis we mwambie unajua kila kitu kuhusu hali yake kwahyo ukutaka kumtangazia hali yake kwa mdada na pia ulifanya kumuokoa mdada na mchumba wake ambae ana hatia kabisa.
 
Asante mkuu...ila kwa akili alyokupa Mungu nitumie lugha gani kumwambia.
Tafuta laini ya mtu ambe yupo mbali na hapo, mtumie huyo dada sms,. Mwambie, unachotaka kufanya hivi karibuni na huyo mwanaume acha. Na kapime hiv. Afu mwambie asikutafute ba umblock. Huwezi kosa simu ya kumtumia sms afu ukapiga block
 
Sio wajibu wako kuwaepusha....
Ni wajibu wa kila mtu kujua umuhimu wa afya yake na kujikinga na magonjwa.

Sababu hujui viral load ya huyo mshikaji....huna hakika kama anaambukiza makusudi....

Ningekuwa mimi ningemwambia nimekutana na hiki kielelezo kuwa unatumia hizi dawa....kama rafiki nakusaidiaje?
Wewe una roho mbaya
 
Habari za humu wanaJF?
Bila kuwachosha naomba niende moja kwa moja kwenye lengo la uzi huu.

Kuna jamaa (tunafanya nae kazi) pia ni rafiki yangu tunaishi nae ghetto moja.
Juzi katika kufanya usafi kwenye room nilikuwa naamisha mabegi naweka sebuleni ili nifanye intensive cleanness kuna kadi ya kliniki ya matibabu ya ARV niliiona, baada ya kuisoma nimegundua kuwa jamaa ni muathirika wa VVU na mbaya zaidi jamaa anatumia ARV kama mwaka wa 6 sasa. Hii sio shida maana kuumwa ni sehemu ya maisha ya yyte aliyezaliwa na mwanamke.

Kinachonisukuma kuwaomba ushauri ni juu ya tabia ya huyu jamaa. Yaani jamaa ni mchakataji mzuri wa papuchi hapa mtaani. Habagui barmaids wala waimba kwaya. Mbaya zaidi ni kiongozi kwenye kwaya yao na huwa naona anavusha baadhi ya waimba kwaya na watoto wa shule.

Hili ni tatizo ila mbaya zaidi kuna binti flani wanamiadi ya kukutana kesho kutwa; maskini binti wa watu namhurumia sana maana jamaa kwa anavyojitapa kuwa hatumii kinga yeye ni nyama kwa nyama. Natamani nimwambie huyu binti ila nakosa lugha nzuri ya kumwambia na ukizingatia binti huyu anatarajiwa kuolewa soon maana ndoa yake imeshatangazwa kwa mara ya kwanza kanisani.

Utata mwingine unakuja kwa sababu nahisi kumwambia huyu dada ukweli ni sawa na kumsaliti jamaa maana ugonjwa ni siri. Na kama hakuwahi nambia kwa miaka yote hiyo hii inamaanisha hataki yyte ajue.

Namshukuru Mungu; ameniepusha na wadada anaotembea nao...mimi sina tabia ya uhuni japokuwa huwa naona rafiki zangu wengine wanagonga mashemeji(mademu wa marafiki zako) .

Naombeni ushauri katika hili, na nitumie mbinu gani kumuepusha huyu binti.

NB: Ukimwi bado upo; Mungu atusaidie; tuepuke ngono haramu.

ASANTENI.
Tafuta mtu ambaye ni anonymous, akusaidie, kazi rahisi sana, njoo pm tumalize mchezo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom