Niwaepushaje hawa na hili?

Nebuchadinezzer

JF-Expert Member
Oct 1, 2018
1,403
2,545
Habari za humu wanaJF?
Bila kuwachosha naomba niende moja kwa moja kwenye lengo la uzi huu.

Kuna jamaa (tunafanya nae kazi) pia ni rafiki yangu tunaishi nae ghetto moja.
Juzi katika kufanya usafi kwenye room nilikuwa naamisha mabegi naweka sebuleni ili nifanye intensive cleanness kuna kadi ya kliniki ya matibabu ya ARV niliiona, baada ya kuisoma nimegundua kuwa jamaa ni muathirika wa VVU na mbaya zaidi jamaa anatumia ARV kama mwaka wa 6 sasa. Hii sio shida maana kuumwa ni sehemu ya maisha ya yyte aliyezaliwa na mwanamke.

Kinachonisukuma kuwaomba ushauri ni juu ya tabia ya huyu jamaa. Yaani jamaa ni mchakataji mzuri wa papuchi hapa mtaani. Habagui barmaids wala waimba kwaya. Mbaya zaidi ni kiongozi kwenye kwaya yao na huwa naona anavusha baadhi ya waimba kwaya na watoto wa shule.

Hili ni tatizo ila mbaya zaidi kuna binti flani wanamiadi ya kukutana kesho kutwa; maskini binti wa watu namhurumia sana maana jamaa kwa anavyojitapa kuwa hatumii kinga yeye ni nyama kwa nyama. Natamani nimwambie huyu binti ila nakosa lugha nzuri ya kumwambia na ukizingatia binti huyu anatarajiwa kuolewa soon maana ndoa yake imeshatangazwa kwa mara ya kwanza kanisani.

Utata mwingine unakuja kwa sababu nahisi kumwambia huyu dada ukweli ni sawa na kumsaliti jamaa maana ugonjwa ni siri. Na kama hakuwahi nambia kwa miaka yote hiyo hii inamaanisha hataki yyte ajue.

Namshukuru Mungu; ameniepusha na wadada anaotembea nao...mimi sina tabia ya uhuni japokuwa huwa naona rafiki zangu wengine wanagonga mashemeji(mademu wa marafiki zako) .

Naombeni ushauri katika hili, na nitumie mbinu gani kumuepusha huyu binti.

NB: Ukimwi bado upo; Mungu atusaidie; tuepuke ngono haramu.

ASANTENI.
 
Najua ukimwambia huyo msichana lazima atakuchoma kwa jamaa ako
Jaribu kuongea na jamaa ako kuwahufurahishwi na tabia yake
Umwambie aachane na yule msichana kwani soon ataenda kuwa mke wa mtu
Fanya hivyo huku uki quote vifungu vya biblia Kwa msaada wa Mungu najua jamaa atakuelewa.
 
Asante mkuu nitafanyia kazi mawazo yako.
 
Sio wajibu wako kuwaepusha....
Ni wajibu wa kila mtu kujua umuhimu wa afya yake na kujikinga na magonjwa.

Sababu hujui viral load ya huyo mshikaji....huna hakika kama anaambukiza makusudi....

Ningekuwa mimi ningemwambia nimekutana na hiki kielelezo kuwa unatumia hizi dawa....kama rafiki nakusaidiaje?
 
HIV ni ugonjwa unaojulikana na miaka nenda rudi tumeambiwa jilinde kuepuka maambukizi, na ikitokea umeshapata maambukizi walinde wenzio!

Mwambie huyo rafiki yako aache roho mbaya.... Mwambie unaujua ukweli na mashauri asiwe katili

Hiyo juhudi anayofanya kuambukiza watu asishangae mzunguko ukazunguka hadi nyumbani kwao akajikuta ndugu zake, wazazi wake na watoto wake kama anao wote wameingia kwenye mzunguko aliouanzisha yeye.

Kuna mijitu ina roho ngumuuuu sana
 
Sio wajibu wako kuwaepusha....
Ni wajibu wa kila mtu kujua umuhimu wa afya yake na kujikinga na magonjwa.

Sababu hujui viral load ya huyo mshikaji....huna hakika kama anaambukiza makusudi....

Ningekuwa mimi ningemwambia nimekutana na hiki kielelezo kuwa unatumia hizi dawa....kama rafiki nakusaidiaje?Nahisi ataniogopa sana.
Hebu fikiria pale jambo ulilolificha kwa muda mrefu ugundue kuna mtu analijua.
 
Asante kwa ushauri mzuri.
HIV ni ugonjwa unaojulikana na miaka nenda rudi tumeambiwa jilinde kuepuka maambukizi, na ikitokea umeshapata maambukizi walinde wenzio!

Mwambie huyo rafiki yako aache roho mbaya.... Mwambie unaujua ukweli na mashauri asiwe katili

Hiyo juhudi anayofanya kuambukiza watu asishangae mzunguko ukazunguka hadi nyumbani kwao akajikuta ndugu zake, wazazi wake na watoto wake kama anao wote wameingia kwenye mzunguko aliouanzisha yeye.

Kuna mijitu ina roho ngumuuuu sana
 
Habari za humu wanaJF?
Bila kuwachosha naomba niende moja kwa moja kwenye lengo la uzi huu.

Kuna jamaa (tunafanya nae kazi) pia ni rafiki yangu tunaishi nae ghetto moja.
Juzi katika kufanya usafi kwenye room nilikuwa naamisha mabegi naweka sebuleni ili nifanye intensive cleanness kuna kadi ya kliniki ya matibabu ya ARV niliiona, baada ya kuisoma nimegundua kuwa jamaa ni muathirika wa VVU na mbaya zaidi jamaa anatumia ARV kama mwaka wa 6 sasa. Hii sio shida maana kuumwa ni sehemu ya maisha ya yyte aliyezaliwa na mwanamke.

Kinachonisukuma kuwaomba ushauri ni juu ya tabia ya huyu jamaa. Yaani jamaa ni mchakataji mzuri wa papuchi hapa mtaani. Habagui barmaids wala waimba kwaya. Mbaya zaidi ni kiongozi kwenye kwaya yao na huwa naona anavusha baadhi ya waimba kwaya na watoto wa shule.

Hili ni tatizo ila mbaya zaidi kuna binti flani wanamiadi ya kukutana kesho kutwa; maskini binti wa watu namhurumia sana maana jamaa kwa anavyojitapa kuwa hatumii kinga yeye ni nyama kwa nyama. Natamani nimwambie huyu binti ila nakosa lugha nzuri ya kumwambia na ukizingatia binti huyu anatarajiwa kuolewa soon maana ndoa yake imeshatangazwa kwa mara ya kwanza kanisani.

Utata mwingine unakuja kwa sababu nahisi kumwambia huyu dada ukweli ni sawa na kumsaliti jamaa maana ugonjwa ni siri. Na kama hakuwahi nambia kwa miaka yote hiyo hii inamaanisha hataki yyte ajue.

Namshukuru Mungu; ameniepusha na wadada anaotembea nao...mimi sina tabia ya uhuni japokuwa huwa naona rafiki zangu wengine wanagonga mashemeji(mademu wa marafiki zako) .

Naombeni ushauri katika hili, na nitumie mbinu gani kumuepusha huyu binti.

NB: Ukimwi bado upo; Mungu atusaidie; tuepuke ngono haramu.

ASANTENI.
Utakuwa mjinga wa mwisho kunyamazia jambo hili, kwanza mchane rafiki yako na umwonye aachane na hiyo tabia vinginevyo utamwambia kila aliyemla na anayetarajia kumla.
Au nipe namba yake nifikishe ujumbe

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom