BABA TUPAC
JF-Expert Member
- Sep 30, 2015
- 1,526
- 3,802
Salama wakuu,
Naombeni ushauri wenu, kwakuwa humu ndani kuna wengi wametuzidi kimawazo na uzoefu wa maisha. Ntaelezea kwa uwazi zaidi ili mtengeneze picha kichwani na kuweza kunishauri vyema
Nina shamba la eka mbili kasoro, lipo Kibaha mkoa wa Pwani si mbali kutoka lilipo jeshi la Nyumbu. Hilo shamba, lina mabanda mawili ya kufugia, lina store kubwa, lina kijumba alichokuwa anakaa kijana wa kusimamia mifugo pamoja kisima cha kuvunia maji ya mvua na chumba cha kutumika kama ofisi.
Katika eneo hilo, pana maji ya bomba na umeme upo jirani kabisa (nguzo mbili). Kwasasa eneo hili sio mashamba tena, watu wameanza kuuza viwanja. Nilikuwa nafuga eneo hili lakini nina miezi sita tokea nimesimama kutokana na sababu ambazo zilishindwa kuzuilika. Kwa eneo lile nikiuza bei ya chini kabisa kwasasa ni sh milioni 80 net.
Sasa nilikuwa nimefikiria kuuza nipate hiyo pesa kisha niende kununua viwanja kama vinne maeneo ya Madale jijini Dar visivyozidi sh milioni 20 kila kimoja kisha niviuze angalau kwa sh milioni 22 kila kimoja. Hivyo nitakuwa nafanya biashara ya kununua na kuuza viwanja katika maeneo kama hayo Madale, Goba, Bunju nk
Nimekuja kwenu kupata ushauri wenu wa kufanya hicho kitu/ kuto kufanya hicho kitu/ kuboresha mawazo niliyo nayo au wazo lolote jipya katika jambo hili.
Asanteni sana ndugu zangu