Niuze shamba ili nikanunue viwanja niviuze kwa faida?

BABA TUPAC

JF-Expert Member
Sep 30, 2015
1,527
3,801
Salama wakuu,

Naombeni ushauri wenu, kwakuwa humu ndani kuna wengi wametuzidi kimawazo na uzoefu wa maisha. Ntaelezea kwa uwazi zaidi ili mtengeneze picha kichwani na kuweza kunishauri vyema

Nina shamba la eka mbili kasoro, lipo Kibaha mkoa wa Pwani si mbali kutoka lilipo jeshi la Nyumbu. Hilo shamba, lina mabanda mawili ya kufugia, lina store kubwa, lina kijumba alichokuwa anakaa kijana wa kusimamia mifugo pamoja kisima cha kuvunia maji ya mvua na chumba cha kutumika kama ofisi.

Katika eneo hilo, pana maji ya bomba na umeme upo jirani kabisa (nguzo mbili). Kwasasa eneo hili sio mashamba tena, watu wameanza kuuza viwanja. Nilikuwa nafuga eneo hili lakini nina miezi sita tokea nimesimama kutokana na sababu ambazo zilishindwa kuzuilika. Kwa eneo lile nikiuza bei ya chini kabisa kwasasa ni sh milioni 80 net.

Sasa nilikuwa nimefikiria kuuza nipate hiyo pesa kisha niende kununua viwanja kama vinne maeneo ya Madale jijini Dar visivyozidi sh milioni 20 kila kimoja kisha niviuze angalau kwa sh milioni 22 kila kimoja. Hivyo nitakuwa nafanya biashara ya kununua na kuuza viwanja katika maeneo kama hayo Madale, Goba, Bunju nk

Nimekuja kwenu kupata ushauri wenu wa kufanya hicho kitu/ kuto kufanya hicho kitu/ kuboresha mawazo niliyo nayo au wazo lolote jipya katika jambo hili.

Asanteni sana ndugu zangu
 
Wazo zuri, ila angalia watoto wa mjini wasije kukuingiza chaka
 
Safi ila madale na goma utahaha saana gharama zake... Km ni mvumilivu na una kipato cha kuendeshea maisha kwa sasa nakushauri nunua maeneo sehemu zingine km vikawe, vikindu, kigamboni.. afu kaa miaka mi3.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ningekuwa wewe ningefanya hivi.. kwanza siuzi eneo lolote ila naliweka bank wanipe mkopo nikafanye hiyo biashaara ya viwanja. Hilo eneo kuuza kwa sasa ni mapema sana acha majengo yaenee kote pakosekane kiwanja eneo la karibu na wewe ndo utakuja kuuza kwa bei ya kujipimia. Ukiuza kwa sasa utalia siku moja.
 
Mkuu iko hivi.

Biashara ya viwanja ni nzuri lakini pesa haipatikani kwa haraka.

Yaani ili uuze viwanja na kurudisha pesa yako na faida itakugharimu muda mrefu inakubidi usubirie angalau miaka 3 na kuendelea ili upate hiyo faida.

Usitegemee uandae viwanja uuze sasa hivi,kama hauna biashara zingine za kukusapoti kimaisha utasota sana.
 
Sure mkuu kama hana subira bhac hii biashara haitamfaa kabisa
 
Ningekuwa wewe ningefanya hivi.. kwanza siuzi eneo lolote ila naliweka bank wanipe mkopo nikafanye hiyo biashaara ya viwanja. Hilo eneo kuuza kwa sasa ni mapema sana acha majengo yaenee kote pakosekane kiwanja eneo la karibu na wewe ndo utakuja kuuza kwa bei ya kujipimia. Ukiuza kwa sasa utalia siku moja.
Good idea
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom