Niulize kuhusu biashara ya hardware, nitajibu kwa uwezo wangu

Forrest Gump

JF-Expert Member
Jul 2, 2021
583
1,266
Personally nimefaidika na madini mengi humu JF kwa ajili ya maswala mbali mbali, sio vibaya na mimi kushare info na wana jamii wafaidike pia.

Nimekulia katika familia yenye b'ness ya hardware, then na mimi nikajikita katika b"ness hio hio.

Nitashare kutokana na uzoefu, uwezo na kiwango cha ujuaji wangu.

Karibuni na wengine mtakao kuwa na majibu kwa wengine.
 
1. Katika mkusanyiko wa bidhaa za Hardware bidhaa gani ndio inaendesha biashara yote kwa mzunguko mkubwa?

2. Kumekuwa na dhana ya upatikanaji wa vitu vya wizi katika biashara ya Hardware ambavyo huwa na bei nafuu je kuna ukweli wowote katika hili?
 
Inaitaji mtaji wa shngap ili duka liweze kujiendesha lenyewe?
Boss cha kwanza hardware ni term pana sanaa..

Ukitaka uwe na hardware ambayo ni:

general hardware (handtools, appliances, power tools, materials za ujenzi, plumbing na sanitary)..yani mtu hakosi kitu..kama unaanza itakubidi uwe na kibubu cha 80million to 150million na zaidi

Plumbing na sanitary system: tenga 25million hadi 30million

Mchanganyiko wa vitu vidogo: Handtools, appliances ndogo(vitasa, komeo,), fixets kama screws, bolts etc, vifaa vya vidogo vya mafundi 25million to 35million,

Yenye Materials za ujenzi tu: kuanzia foundations hadi fiinishing 50 to 100million

Au unaweza kufanya cheat code kwa mtaji mdogo kwa kumix kidogo kidogo hivyo vyote hapo juu kidogo kidogo ila kuna bidhaa utamiss dukani ..35miillion

Kama ni mbao tu 15m to 25m
 
Kabla ya kuanzisha hardware ni vitu gani vya mhimu unapaswa kuangalia ili mambo baadae yaweze kwenda sawa
Cha kwanza angalia mtaji wako, çha pili usipate stress sana kutaka kuwa na kila kitu, hardware ni pana unaweza uka specialize katika kundi flani mfano: handtools na aplliances ndogo kama vitasa, plumbing, finishing materials, rangi na mshine ya kuchanganyia, ..etc

Usifanye mistake ya kufanya hardware yenye materials kubwa na una mtaji mdogo..otherwise una samples na unaleta kutoka kwa jilani au unapewa mzigo kwa credit ukiuza unarudisha..

Then angalia sehemu zinazo jengeka sana tupia hardware..

Kama ni sehemu zilizojengeka sana.. finishing materials italipa sana au vifaa vya ufundi kwa ajili ya ujenzi..

Enjoyy
 
Maduka kadhaa ya hardware upangaji wa stock hua ni holela sana(unaweza hata dondokewa na sururu)..Hivi utaratibu wa kuhesabu stock ukoje,unafanywa mara ngapi?..

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
Ahhaahah...kweli mimi mwenyewe nilikuwa naumia....

First of all... hardware nzuri ni ile yenye store kwa nyuma, yani mbele unaweka vichache ..nyuma una uwanja mpana wa kuviweka..

Mara nyingi unajikuta unasema kitu hakipo angali kipo,

Mimi huwa navipanga kutokana na nature ya bidhaa....mfano vitasaa, na komeo, na kufuri...

Vizito vinakaa chini , vyepesi juu..virefu kati kati
 
Kwanin wafanya biashara wanakuwa hardware wengi wao huwa wanatajirika sana?
Maisha ni ujenzi boss, pale unapokaa geto ukitaka kuweka pazia utahitaji screws na fisherplugs na star ya kufungia, hadi mtaani majengo na vitu vinaharibika kila siku, vifaa vya ufundi vya kichina vina haribika mapema,

Miji inakuwa kila siku...

Bidhaa za ujenzi haziozi, so price inabaki pale palle bila kuweweseka

Pia faida ni nzuri katika kila bidhaa
 
Ukiwa na mtaji wa milioni 15 huwezi fungua? Mfano NONDO, CEMENT NA SQUARE PIPE, MISUMARI, PIPE ZA CHUMA NA ZA MAJI.
 
1: Bidhaa inayotaka ni za foundations ni cement, nondo, paa, mbao,

Pia vifaa vya ufundi kama pliers, pasi, miiko inatoka sana kutokana wachina kutusaidia hahahah

2: Ni kweli kabisa mafundi huwa wanatuletea kila siku ila sina hulka ya kununua... mnaojennga mnapigwa sana kuweni makini
 
1.Katika mkusanyiko wa bidhaa za Hardware bidhaa gani ndio inaendesha biashara yote kwa mzunguko mkubwa?
2.Kumekuwa na dhana ya upatikanaji wa vitu vya wizi katika biasahra ya Hardware ambavyo huwa na bei nafuu je kuna ukweli wowote katika hili?
1: bidhaa inayotaka ni za foundations ni cement, nondo, paa, mbao,

Pia vifaa vya ufundi kama pliers, pasi, miiko inatoka sana kutokana wachina kutusaidia hahahah

2: ni kweli kabisa mafundi huwa wanatuletea kila siku ila sina hulka ya kununua... mnaojennga mnapigwa sana kuweni makini
 
Back
Top Bottom