Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

ninashida yakupata cylinder head au complete engine ya ford focus 2000 toleo la ujerumani
 
Hivi mkuu Kichuguu, huu mtindo unafanywa na chuo cha DIT wa kuongezea mfumo wa kutumia mitungi ya gas kwenye magari ya petroli kitaalam upo je?
Kuna madhara yoyote?
Mimi binafsi swala la mtungi kukaa ndani ya gari (hatchback) bado halijanibariki
 
Matumizi ya natural gas kwenye injini za petroli ni sawa tu; hakuna tatizo lolote kabisa. nadhani matatizo yanaweza kuwa ni namna ya ufungaji wa matanki hayo yasivujishe gasi.
 
Hivi kwanini hizi vanguard hazina spare tairi mkuu
 
Kuna gari natumia Toyota Brevis cc2490 imeanza tatizo la ku plink (kutoa ka mlio fulani k,a,k,a,k,a,k,a ) ila baada ya muda ina kuwa sawa hili tatizo linakua temperature ikiwa chini ikipanda linaisha.
 
Tazama engine oil kama imepungua.
 
Kuna gari natumia Toyota Brevis cc2490 imeanza tatizo la ku plink (kutoa ka mlio fulani k,a,k,a,k,a,k,a ) ila baada ya muda ina kuwa sawa hili tatizo linakua temperature ikiwa chini ikipanda linaisha.
Angalia aina ya oil unayoitumia ni nzito sana hivyo kufanya kazi hadi joto la engine liwe kubwa ndo iweze kusambaa vzr nakushauri kwa aina hiyo ya gari tumia oil 5w30/10w30 umekosa sana tumia 5w40 achana na sae40
 
Hata 5W-40 siyo nzuri kwa gari ndogo. AJitahidi apate 5W3-20. 5W-30 au 10W 30
 
Angalia aina ya oil unayoitumia ni nzito sana hivyo kufanya kazi hadi joto la engine liwe kubwa ndo iweze kusambaa vzr nakushauri kwa aina hiyo ya gari tumia oil 5w30/10w30 umekosa sana tumia 5w40 achana na sae40
Asante nitalifanyia kazi
 
mzee baba nissan cube yangu yapata mwaka sasa inatembelea kwenye L, na sio D ,kama nikiitumia hiyo D gari haibadili gear au mwendo kwa wakati ,shida itakuwa ni nini mtaalam?
 
Kuna gari natumia Toyota Brevis cc2490 imeanza tatizo la ku plink (kutoa ka mlio fulani k,a,k,a,k,a,k,a ) ila baada ya muda ina kuwa sawa hili tatizo linakua temperature ikiwa chini ikipanda linaisha.
Umshepewa majibu sahihi kuwa ni swala la oil. Injini yako ina hydraulic valve lifters, yaani tappets. Kinachoteka ni kuwa oil inakuwa haiwezi kupenya kiasi cha kutosha ili kusukuma tappets kufungua valve; kwa hiyo injini inakuwa na misfire ndogondogo mwanzoni. Oil ikishapata joto la kutosha na viscosity yake kupungua, ndipo inapoweza kupenya vizuri kusukuma tappets na hapo ndiop unaposikia gari limeanza kuunguruma vizuri. Hiyo ikiendelea kwa muda mrefu inaweza kukuharibia injini kwa vile baadaye inaweza kuziba matundu ya lifters na kusababisha misfire kubwa
 
Asante sana shule imeniingia sawasawa
 
mzee baba nissan cube yangu yapata mwaka sasa inatembelea kwenye L, na sio D ,kama nikiitumia hiyo D gari haibadili gear au mwendo kwa wakati ,shida itakuwa ni nini mtaalam?
Inawezekana gear box imeharibika ndani; au mafuta ya gearbox yamepungua sana au oil filter ya gearbox imeziba. Angalia level ya mafuta kwenye gearbox yako kwanza kabla ya kutafuta mafundi
 
oil ya gearbox ya gari ndogo nayo ni namba90?
 
Gearbox automatic ina oil yake maalum initwa ATF (Automatic Transmission fluid), na kuna aina nyingi sana za mafuta hayo. Kila gari ina aina yake. Ukiweka namba 90 utaua gearbox yote. Namba 90 ni kwa gearbox za stick shift na diff; usiiweke kwenye automatic transmission
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…