Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,571
- 19,453
- Thread starter
- #41
Naomba kujua hili swala la kuwasha gari asubuhi au likiwa limekaa muda mrefu bila ya kutembea,kuna wanaosema inabidi usubiri kama dkk 2 ndio uondoke na wengine wanasema unaweza tu kuondoa gari,tupe ufafanuzi hapa lipi hasa ni kweli na sababu ni nini...?
Jibu la Boeing 747 ni sawa kabisa; dakika mbili bado ni nyingi sana. Kwenye nchi za baridi sana engine huweza ku-contract na kusababisha vipimo cha parts mbalimbaliza injini visilingane kama ilivyokusudiwa, hivyo kusababisha injini isiweze kustart vizuri.
Watu wa huko huweka engine block heaters za umeme kuhakikisha injini inapata joto la kuweza kustart. Ikisha start, unahitaji kuipa sekunde 20 tu kusukuma oil kwenye sehemu mbalimbali za injini kabla ya kuanza safari; ni muda wa kutosha wewe kuvaa mkanda na kupuliza hewa ja joto kwenye windshield kukausha umande kabla hujaanza safari.
Ukikaa nchi za baridi unaweza kuona jirani anawasha gari analiacha linawaka wakati anakula breakfast; nia ya kufanya hivyo ni kuweka joto ndani ya gari kabla hajaingia, na kwa bahati mbaya huo sio utaratibu mzuri kwa sababu wakati injini iko kwenye idling conditions kwa muda mrefu, huweka masizi mengi sana kuliko wakati inatembea.