Nitumie nafasi hii kulipongeza Baraza la mitihani Necta

Reality of heaven

Senior Member
Nov 2, 2022
108
350
Habari wakuu! Nimeona majadiliano mengi kuhusiana na maamuzi ya necta kutofanya Ranking!! Mm kwa utafiti wangu nitumie nafasi hii kuwapongeza necta kwa maamuzi haya! Kimsingi hayawezi kuwafurahisha wengine kwa sababu ni biashara zao! Hizi ni sababu ambazo zinanifanya niwapongeze necta kwa mabadiliko haya!

1: kutangaza ranking, kunachochea wizi wa mithani: mm Nina mifano hai Nina mdogo wangu tulimpeleka kusoma shule moja kubwa tu hapa Tanzania na inafanya vzr sana! Kufika pale kila mthani uwe wa mock au ya mashindano yoyote lazima darasa nzima wapate A! Na hata mithani ya kitaifa wote wanapata A! Kwa sababu tunajua uwezo wake tulimbana atuambia kwa nini wanafaulu hivyo ndipo akatuambia mthani wanasolve wiki moja kabla na kila mmoja anakuwa na majihu yake!

Kwa shule za msingi wanasolve ule mthani siku ile ile ya kusimamia, na kinachofanyika wasimamizi wanapewa mkwanja mrefu alafu walinzi wanawekwa kwenye njia kuchunga magari ya ukaguzi, wanafunzi wanaambiwa wasijaze baada kama nusu saa hivi wanaletewa majibu yaliyosahihi kama 48! Alafu maswali mawili wanaachiwa kila mmoja apambane nayo! Haya yote yanafanyika ili kutangaza shule, hizo shule kubwa Wana network mpaka huko barazani wanahakikisha wanatumia hata 50M kupata mthani lengo wawe pale juu! Ndo maana ada zao ni kubwa sana! Unakuta kila mwanafunzi ana percent ya hela ya kununuliwa mthani! Hivyo uamuzi huu wa necta ni mabadiliko makubwa Sana yanaanza kuonekana kwa kipindi hiki cha mama samia! Kimsingi Mama Samia Rais wetu anaupiga mwingi!!

2: maamuzi haya yatapunguza ada kwa shule! Ada zimekuwa zikiongeza kila uchwao kwa kigezo kuwa shule inafanya vzr kumbe ni wizi mtupu! Ni kweli hizi shule zinafundisha lakini wizi umekitiri!

3: mazingira ya shule hayafanani! Wale vipanga wanapelekwa shule kubwa mfano tabora, iliboru nk na shule za private zinachukua pia vipanga lakini na kuandaa mazingira mazuri! Wanaobaki katika shule za kawaida ni zaidi ya asilimia 70, japo mthani unakuwa ni mmoja huwezi kutangaza kuwa huyu ameongoza kumshinda huyu! Wakati mazingira hayafanani!

Hicho kitendo ni unyanyasaji wa kielimu Kama ulivyo unyanyasaji wa kijinsia! Wenzetu Kenya wao, private matokeo yao yanakuwa pamoja na huku government wanatolewa matokeo yao kivyao! Lakini huku kwetu hata ukifanya hivyo bado kuna ubaguzi maana huwezi kulinganisha shule Kama tabora boys na shule ya itununo sekondari school kule manyoni vijijini! Utakuwa huwatendei haki bado!

Kwa maamuzi haya ya necta wanastahili pongezi kubwa!!
 
Hakuna lolote ni kutafuta uchochoro wa kukwepa kuwajibika, mazingira ya utoaji elimu yanakua ovyo shule inafelisha watoto - wanaogopa kuchafuka! Kwenye teaching and learning ranking and position inachochea morale!

Tutafute hela watoto wasome shule nzuri, pia mazingira ya utoaji elimu yaboreshwe ka shule za umma.
 
Back
Top Bottom