Nitumie kitu gani ngozi ya viganja vya mikono iwe laini

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
Habari wanajukwaa,

Mwenzenu sifurahii kabisa jinsi ngozi ya viganja vyangu vya mikono ilivyo kavu na ngumu, yaani hainivutii kabisa natamani ilainike.

Nilishauriwa zamani kutumia glycerine lakini sikuona matokeo niyatakayo.

Naomba kwa wajuzi wanifahamishe nitumie kitu gani ngozi yangu ilainike?

Nitashukuru kupata mawazo yenu ili niondokane na adha hii.
 
@Nyendo,Kwanza ni kwanini ngozi ya viganja vyako iwe ngumu?

ᵃʳᵉᵉᵐ
 
Oops!!! Yaani Kiganja Kiwe Soft
Mkuu Acha Mzaha, Nilifikiria Damu Haifiki Kwenye Kiganja
 
Mafua ya nazi.
Sukari.
Limao.

changanya hivi vitu alafu masaji mikono yako kisha osha. Alafu niambie jinsia yako na mafuta unayopaka.
 
Sanitizer.
Hii inakakamaza ngozi hatari aisee yani rona iishe tu jamani😎

Mtoa mada jaribu product yenye cocoa butter au shea butter lazima huo ukavu utaisha. Pia unaweza include oil kny routine yako. Vitamin e oil, au olive oil au sun flower oil au coconut oil. Oil unapaka juu ya ngozi baada ya kupaka body cream yako.
 
Back
Top Bottom