Nitaweza kujenga nyumba kwa Milioni tatu?

Nitaweza kujenga nyumba kwa Milioni tatu?

mbao unaijua mbao au sijakuelewa
Mbao ndio mkuu tena mninga! Huku DSM najua ni ghali sana ila mikoani ndani ndani rahisi mno haswa kwenye mashamba ya magereza.
.
Najua wewe unawapiga bei za ajabu wateja wako nawe unapigwa za ajabu ila wajanja hatuna hizo shida, nikipita pale buguruni nikiaikia zile bei najiuliza wanafidia gharama za usafiri ama mbona mbao upatikanaji wake ni rahisi?
 
Sasa mkuu naona kutufurahisha tu.

Yaani nyumba ya mawe tupu kibongo bongo ndio ya mtu tajiri.

Wewe jenga ya tope tu.
 
Mbao ndio mkuu tena mninga! Huku DSM najua ni ghali sana ila mikoani ndani ndani rahisi mno haswa kwenye mashamba ya magereza.
.
Najua wewe unawapiga bei za ajabu wateja wako nawe unapigwa za ajabu ila wajanja hatuna hizo shida, nikipita pale buguruni nikiaikia zile bei najiuliza wanafidia gharama za usafiri ama mbona mbao upatikanaji wake ni rahisi?
Tatizo fundi mkuu, kupata fundi wakujenga wooden house ya kisasa, ila still bado kujenga kwa mbao ni ghal at a kama upo mikoani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa mkoa wa morogoro inawekana kuna tofali za kuchoma kwa sasa hazijafika 150 kwa tofali moja, utajengea udongo badala ya sementi pao la flati mbao chini ya 50 bati kama ulivyosema, fundi wa kawaida laki 3 nyumba nzima. ila haitakua kama hio picha hapo juu na hautafanya finishing yoyote,
Hapo amepigia hesabu na uwanja mkuu
 
Mkuu ungekuwa na uwanja angalau ungejenga Ila kijijini kwenu,maana miti ungekata ya ukoo kupata mbao,materials zingine na nguvu kazi ungepata watoto wa Shangazi,baba mdogo etc
 
Anza na hicho kidogo ulicho nacho ndugu, hiyo m3 haitakamilisha Nyumba ila hiyo m3 unaweza kuanzia taratibu huku ukijikusanya ukitaka ushauri wa kujenga Nyumba humu JF hakika huwez kujenga maana hapa watakwambia bei za akina Ridhiwani Kikwete na akina Jesca Magufuli..., anza mdogo mdogo hata iwe miaka 5/6....utamaliza tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom