Tembea uone,
Leo nilipiga kwata pwani kijiji fulani kutafuta kuku aina ya kuchi. Baada ya kuona kuchi original hawapatikani mpaka kisiwani Juani mafia ikabidi nibadili mpango, nikaomba waniuzie Chotara wa Kuchi. Kila nikiwaambia nataka Bokea ( Bokea ni jina la chotara wa kuchi kwa baadhi ya maeneo ya Pwani), wenyeji wangu hawakunielewa, baadae nikafafanua kuwa ni kuku ambaye jogoo alikuwa kuchi na mtetea ni hawa wa kawaida.
Mara moja yule mzee kasema "kumbe unataka mwanaharamu wa Kuchi" hao wapo wengi utawapata mwanangu !!!. Ilibidi nicheke kidogo, kumbe hata kuku wanazaa haramu.
Nimepata hawa haramu wa kuchi mitaa ya Ikwiriri na Rufiji, nitawakusanya na kuwaleta Dar, atakayetaka basi tuwasiliane ili siku wakifika namjulisha ili awachukulie kwangu. Na nitaendelea kuwakusanya hawa Bokea pamoja na majogoo original ya kuchi taratibu, ila bei imesimama. Ambao hawajaanza kuwika bei ni Tsh 20,000/ pale Ikwiriri na Rufiji, ila Kuruti bei ni nzuri kiasi ni Tsh 15,000/ gharama ya Kuruti ni usafiri wa boti.
Je unataka Haramu wa kuchi nikupee!!!!!