Nitawakingaje wanangu wasitumie madawa?

Nitawakingaje wanangu wasitumie madawa?

Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. We kama mzazi ni jukumu lako kumlea katika maadili yanayompendeza Mungu
 
Ukiwa nao wazungumzie watumiaji kwa kuwadharau na kuwakejeli wafanye waone watu wa namna hyo wanaonekanaje kwenye jamii
 
Pamoja na kuchanganyika na kucheza pamoja lakini sio watoto wote mtaani wanatumia madawa ya kulevya. Wako watoto ambao hawavuti hata sigara ya kawaida ingawa wanaishi pamoja kwenye nchi, mkoa, wilaya, tarafa, kata, kijiji/mtaa au hata kitongoji au nyumba moja na watoto wengine ambao wanatumia madawa ya kulevya.

Hivi, ni sababu zipi zinazosababisha watoto watumie au wasitumie madawa ya kulevya?. Ni nini nafasi ya familia, shule, taifa katika kuzuia au kusababisha mtoto atumie au asitumie dawa za kulevya? Maana kinga ni bora kuliko tiba.

Wale wazazi wenye watoto ambao hawatumii dawa za kulevya naomba elimu/mbinu (kama ipo) ya jinsi ya kuwafanya watoto wangu wasipende kutumia madawa ya kulevya.
njia ni moja tu kua karbu na watt wako na uwe unawaaambia sio kwa ukali bali kirafiki madhara ya madawa na kama kuna uwezekano wa kuwapa mifano hai ni vzr
 
Mungu ndie mlezi ila kuna vitu mzazi unapaswa kuvifanya
Mfano kuwahimiza dini n ukiwaonyesha kwa mfano nenda nao kanisani, fanya maombi nyumbani, wakanye wakikosea,toa mkwara wa kutosha ukiona wana magroup yasiyo mema
Wapeleke shule zenye ufaulu mzuri, nidhamu na za kidini,wahimize kuwa watu wema ktk jamii, wavishe nguo za heshima nk..
 
Poa mkuu nikuelewa
 
Back
Top Bottom