kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,718
- 14,150
Pamoja na kuchanganyika na kucheza pamoja lakini sio watoto wote mtaani wanatumia madawa ya kulevya. Wako watoto ambao hawavuti hata sigara ya kawaida ingawa wanaishi pamoja kwenye nchi, mkoa, wilaya, tarafa, kata, kijiji/mtaa au hata kitongoji au nyumba moja na watoto wengine ambao wanatumia madawa ya kulevya.
Hivi, ni sababu zipi zinazosababisha watoto watumie au wasitumie madawa ya kulevya?. Ni nini nafasi ya familia, shule, taifa katika kuzuia au kusababisha mtoto atumie au asitumie dawa za kulevya? Maana kinga ni bora kuliko tiba.
Wale wazazi wenye watoto ambao hawatumii dawa za kulevya naomba elimu/mbinu (kama ipo) ya jinsi ya kuwafanya watoto wangu wasipende kutumia madawa ya kulevya.