Nitasimama na Rais Samia Suluhu, kuna watu wameanza kumchukulia poa hawatoi risiti

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
18,200
27,255
Mimi binafsi nathubutu kusema ni raia mwema, sijawahi kuwa na kesi Wala kushtakiwa kwa chochote tokea nizaliwe pamoja na kukulia mazingira hatarishi Kinondoni Manyanya.

Mimi nipo pamoja na mama, na pale ntapoona hakupo sawa nitaandika humu, Sina namna nyingine ya kumfikishia lengo kubwa ni aelewe mambo yanayotokea huku mtaani ili achukue hatua haraka mambo yakae sawa.

Hapo nyuma Serikali ilifanya jitihada kubwa Sana kuhakikisha kila kituo Cha mafuta kinatoa risiti za electronic na walifungiwa mfumo huo wa risiti kila kwenye pump machine( risiti zinatoka automatically).

Lakini nimestaajabishwa na nilichokiona Jana, risiti hazitoki tena automatically kwenye petrol station niliyoenda , eti mfumo umeharibika, sasa mbona mauzo yanaendelea? Serikali itapata wapi kodi stahiki kweli?

Kwa nini wasisimamishe huduma mpaka watapotengenza machine ya risiti?

Mama tuma vijana wako field wafanye ukaguzi na wasaidie machine zitengenezwe ili Kodi stahiki ya serikali ipatikane.

Wafanyabiashara chondechonde tusianze kumhujumu mama, ameonyesha busara kubwa kwenye kudai Kodi basi na sisi tutimize wajibu wetu wa kulipa bila kubugudhiwa.

Tukiendelea na haya tutamkwamisha mama, maana Kodi itapatikana kidogo na atashindwa kuendeshea vizuri serikali.

#mama Samia kanyaga twende# kazi iendelee#
Screenshot_20210415-171736_1.jpg
 
Hii ni taarifa nzuri sana, tena inabidi iwe kama Kampeni ya kusimama na Madam President kwenye kodi, ila nashauri twende mbele zaidi kutaja na kituo cha mafuta kilichofanya hiyo hujuma, jukumu liwe la TRA kwenda kufanya ukaguzi.
Siwezi kutaka kituo kwa kuwa inaweza kuwa vipo vingi Sana tena pengine nchi nzima, Bali mama atume vijana wake waende kazini kubaini hivyo vituo
 
Mhn! Nahisi hili bandiko lako ni la kinafiki. Usichowachonganishe wananchi na Rais. Wewe yana hiyo Petrol station na usilete “blanket statements” hapa.

Nitashangaa sana kama hilo ni kweli. Kwasababu Hiyo EFD machine hata ikiacha kutoa risiti, huwa mauzo yanasimamishwa hadi itengenezwe. Na hiyo huwa inaripoti TRA directly. Ikiacha kutoa risiti TRA watafahamu.
 
Nchi yetu inahitaji TAASISI imara sio uiamara tu wa no 1,watanzania nani aliyetologa?uimara wa no 1 ni wa kupita ila strong and independent institutions ni wa kudumu,mtoa hoja hapo ulibidi upate FACTS na unawapigia simu TRA(toll free number)nao wanachukua hatua SIO kazi ya no 1 hii.
 
TRA baada ya virungu vya mama wako busy kuona watoke vipi.

Baada ya mama kuwavuruga hadithi za kubumba kama hizi mbona zitakuwapo nyingi tu kupalilia uhalali (relevance)?

Sasa hivi nyanja nyingi wakiwamo mataga nguli ziko busy kutafiti watoke vipi kum impress mama.

Hiiiiii!

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Mimi binafsi nathubutu kusema ni raia mwema, sijawahi kuwa na kesi Wala kushtakiwa kwa chochote tokea nizaliwe pamoja na kukulia mazingira hatarishi Kinondoni Manyanya...
Naona mwisho wa siku umeheshimu na kutii mawazo yetu kuwa huwezi kuwa mpinzani ndani ya chama ukabaki salama.
 
Back
Top Bottom