Nitasimama na Rais Samia Suluhu, kuna watu wameanza kumchukulia poa hawatoi risiti

kuna uwezekano mapato yakapungua sana, hakuna mtu hapa duniani ambaye huwa anapenda kulipa kodi kwa hiari, amini usiamini, hata mimi sitalipa kodi kama ni kwa kubembelezana.

Kodi unatakiwa kulipa kwa mabavu, ukijua kuwa usipolipa kinanuka. tunahitaji hela za kuendeshea nchi na kufanya maisha yawe bora kwa wananchi wetu.
 
Ni kweli huyu Mama wanamchukulia poa sana. Jana Lusinde alikuwa anamuita SAMIA, ila katika hotuba hiyo hiyo, Magufuli ambaye ni Marehemu alikuwa anamuita Muheshimiwa Magufuli!!
 
TRA baada ya virungu vya mama wako busy kuona watoke vipi.

Baada ya mama kuwavuruga hadithi za kubumba kama hizi mbona zitakuwapo nyingi tu kupalilia uhalali (relevance)?....
Ndiyo, unasema uongo.
 
Nijuavyo mimi mashine hizo haziwezi kutoa MAFUTA kama MFUMO WA RISITI NI MBOVU.
Acha uongo
 
Ni kweli huyu Mama wanamchukulia poa sana. Jana Lusinde alikuwa anamuita SAMIA, ila katika hotuba hiyo hiyo, Magufuli ambaye ni Marehemu alikuwa anamuita Muheshimiwa Magufuli!!
Kibajaj atajikuta yuko kwenye hali mbaya sana.
Lakini jeuri hiyo anapewa na subwoofer
 
Mimi binafsi nathubutu kusema ni raia mwema, sijawahi kuwa na kesi Wala kushtakiwa kwa chochote tokea nizaliwe pamoja na kukulia mazingira hatarishi Kinondoni Manyanya.

Mimi nipo pamoja na mama, na pale ntapoona hakupo sawa nitaandika humu, Sina namna nyingine ya kumfikishia lengo kubwa ni aelewe mambo yanayotokea huku mtaani ili achukue hatua haraka mambo yakae sawa.

Hapo nyuma Serikali ilifanya jitihada kubwa Sana kuhakikisha kila kituo Cha mafuta kinatoa risiti za electronic na walifungiwa mfumo huo wa risiti kila kwenye pump machine( risiti zinatoka automatically).

Lakini nimestaajabishwa na nilichokiona Jana, risiti hazitoki tena automatically kwenye petrol station niliyoenda , eti mfumo umeharibika, sasa mbona mauzo yanaendelea? Serikali itapata wapi kodi stahiki kweli?

Kwa nini wasisimamishe huduma mpaka watapotengenza machine ya risiti?

Mama tuma vijana wako field wafanye ukaguzi na wasaidie machine zitengenezwe ili Kodi stahiki ya serikali ipatikane.

Wafanyabiashara chondechonde tusianze kumhujumu mama, ameonyesha busara kubwa kwenye kudai Kodi basi na sisi tutimize wajibu wetu wa kulipa bila kubugudhiwa.

Tukiendelea na haya tutamkwamisha mama, maana Kodi itapatikana kidogo na atashindwa kuendeshea vizuri serikali.

#mama Samia kanyaga twende# kazi iendelee#
View attachment 1752901
Mimi mwenyewe hayo hayo yamenikuta. Nikaambiwa nifuate risiti baadae….like really?
 
Back
Top Bottom