Nitashinda kwenye rufaa asema dr. Dalali kafumu...

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
27.jpg

Aliyekuwa Mbunge wa Igunga Dr. Dalaly Peter Kafumu kwa tiketi ya "Magamba"(CCM) ambae alivuliwa Ubunge na Mahamaa Kuu Kanda ya Tabora mwezi Agosti, 2012, pichani juu kulia, "amefumuka" kwenye Kipindi cha Medani za Siasa kinachorushwa na STAR TV na kusema kuwa anatarajia kushinda kwenye Rufaa kuhusu kutenguliwa kwake ubunge kutokana na sababu zilizotolewa na JaJi wa Mahakama Kuu kuwa dhaifu na hazimuhusu yeye.

Kafumu amesema sababu hizo ni pamoja na: (i) yeye kuhusishwa na vurugu zilizopelekea aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Igunga Fatuma Kimario kuvuliwa Hijab na wafuasi wa Chadema jamba ambalo haoni kuwa na mantiki kwani vurugu zilihusisha vyama vyote CDM, CCM na CUF na kwake hajaona ni kwa nini ahusike moja kwa moja ; (ii) kitendo cha Magufuli kutoa ahadi ya Daraja wakati hizo zilikuwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM na yeye hakuhusika kutoa ahadi hiyo na (iii) ni Wananchi kugawiwa Mahindi ya njaa wakati wa Kampeni za Uchaguzi, jambo ambalo kwake anasema linaihusu Serikali zaidi na sio yeye binafsi na kuwa mgao huo ulianza kabla ya kampeni kuanza na kuwa ulilenga kuwanusulu wananchi na janga la njaaa ambalo Mahakama ingepaswa kuona kuwa ulifanyika kwa nia njema.
 
Huyu Dr ni kigeugeu ameshavutwa masikio na wakina Nape, wiki zilizopita alisema hataki tena Ubunge anataka kufanya kazi aliyosomea. Pili huyu Dr wa mambo ya Udongo anashindwa kuelewa zoezi zima la Uchaguzi ndio lilosababisha kutenguliwa kwa ubunge wake mfano ahadi za wakina magufuli ambazo zilifananishwa na rushwa kutokana na madaraka aliyo nayo sasa huyu DR anafikiri lazima zimuhusu yeye moja kwa moja
 
Lakini pia amesema endapo atashindwa kwenye hiyo rufaa na hivyo uchaguzi ukarudiwa yeye binafsi HATAGOMBEA ubunge tena na badala yake atashirikiana na Magamba wenziye kumnadi mgombea wao atakayekuwa ameteuliwa. Huyu jamaa anaonekana ameshachoka na siasa na hivyo hataki tena udhalilishaji wa kwenye majukwaa ya siasa. From Commisioner of Minerals to MP to nobody! Chezea siasa weye?
 
Nijuavyo mimi mnapokuwa kwenye kampeni mtuyoyote akisemachochote huhesabika kuwa amesema kwa niaba ya mgombea hivyo yote yaliyokuwa yanatamkwa/yanatendwa na viongozi wa serikali ya CCM ni kwaniaba ya mgombea wao kama vile kugawa vyakula, kuahidi mdaraja...
 
Lakini pia amesema endapo atashindwa kwenye hiyo rufaa na hivyo uchaguzi ukarudiwa yeye binafsi HATAGOMBEA ubunge tena na badala yake atashirikiana na Magamba wenziye kumnadi mgombea wao atakayekuwa ameteuliwa. Huyu jamaa anaonekana ameshachoka na siasa na hivyo hataki tena udhalilishaji wa kwenye majukwaa ya siasa. From Commisioner of Minerals to MP to nobody! Chezea siasa weye?
anaujua ukweli kuwa uchaguzi ukirudiwa Igunga CCM haiwezi kushinda hata wakitumia bil 20...
 
jamaaa wanashindwa kuelewa kuwa ccm watu hawaipendi hata wafanyaje ngoma ni nzitooo
 
Mtoa mada anajifurahisha tu hii ni habari ya muda sana kabla ata hajavuliwa ubunge wakati rufaa ikiwa mahakamani.......

star tv wanarudia kipindi hiki kila mara na taarifa hizi, sijui kwanini?

Mod: pls toeni habari hii haina mantiki na maana

V
SENGEREMA
 
mwenzie Mukama sasa anajuta kisirisiri kufanya kosa la kuingia kwenye siasa. Mwacheni aendelee kuvutwa masikio tu
 
Ahaa!mwendawazimu ni mwendawazimu tu....kilichonichekesha ni huyo fupi nyundo bwm,
 
Hana jipya ,kwani hata akishinda hiyo rufaa yake 2015 sio mbali ,nadhani Wana Igunga hawatafanya kosa tena ,kwani nasikia vijana wanasubiri kwa hamu kubwa huo uchaguzi kwani watakuwa tayari wameisha jiandikisha kwenye daftari la wapiga kura
 
27.jpg

Aliyekuwa Mbunge wa Igunga Dr. Dalaly Peter Kafumu kwa tiketi ya "Magamba"(CCM) ambae alivuliwa Ubunge na Mahamaa Kuu Kanda ya Tabora mwezi Agosti, 2012, pichani juu kulia, "amefumuka" kwenye Kipindi cha Medani za Siasa kinachorushwa na STAR TV na kusema kuwa anatarajia kushinda kwenye Rufaa kuhusu kutenguliwa kwake ubunge kutokana na sababu zilizotolewa na JaJi wa Mahakama Kuu kuwa dhaifu na hazimuhusu yeye.

Kafumu amesema sababu hizo ni pamoja na: (i) yeye kuhusishwa na vurugu zilizopelekea aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Igunga Fatuma Kimario kuvuliwa Hijab na wafuasi wa Chadema jamba ambalo haoni kuwa na mantiki kwani vurugu zilihusisha vyama vyote CDM, CCM na CUF na kwake hajaona ni kwa nini ahusike moja kwa moja ; (ii) kitendo cha Magufuli kutoa ahadi ya Daraja wakati hizo zilikuwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM na yeye hakuhusika kutoa ahadi hiyo na (iii) ni Wananchi kugawiwa Mahindi ya njaa wakati wa Kampeni za Uchaguzi, jambo ambalo kwake anasema linaihusu Serikali zaidi na sio yeye binafsi na kuwa mgao huo ulianza kabla ya kampeni kuanza na kuwa ulilenga kuwanusulu wananchi na janga la njaaa ambalo Mahakama ingepaswa kuona kuwa ulifanyika kwa nia njema.

Kweli kuwa CCM kimeo,sasa yeye anasema hakuhisika kama yeye wakati mahakama imejiridhisha kuwa alifaidika na haya mambo,wether kw akujitakia au lah.

Kinachokazia zidi hayo mambo ni kwave inathibitisha kile yalifanywa na chama chake na yalifanyw amakusudi ili kumpa ushindi.Hakuna shemu alijitahidi waondoa hao watu katika timu yake ya kampeni.Hii yote inathibitisha kuwa alishiriki bila mashaka.Alikuwa akilala na kumka na hii timu.Sijui huyu dr. naye kageuka kuwa walewale ma Dr na Maprof wa CCM.
 
Back
Top Bottom