Mchimwachimego
JF-Expert Member
- Jun 15, 2020
- 358
- 271
Kila nikikumbuka maamuzi magumu ya Rais Magufuli kuhusu Corona, sina shaka na utimamu wake na ujasiri.
Kwa kipindi kama kile ambacho nchi nyingi ziliamua kufunga biashara na shughuli nyingi za kiuchumi, mtu huyu aliamua kwamba wafanyabiashara waendelee na biashara zao na shughuli nyingine ziendelee.
Hakuna biashara iliyofungwa, lakini watanzania hawana shukrani wanasahau yote kisa mtu ambaye kwa ninavyomtazama mlengo wake si wa kimisimamo binafsi bali ya kuongozwa na anaowaamini.
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Magufuli anastaili kukamilisha kipindi cha miaka 10, uongozi si wa kubadilisha kama nguo. Tukipata kiongozi mzuri basi tumuache amalize awamu zote mbili.