Nitashaingilia Msumbiji kwa Nguvu zote.

Nitashaingilia Msumbiji kwa Nguvu zote.

Kwani walitokaje na msumbiji?
Ila hii timu bana,maisha tuyawaze na timu tuiwaze?
Acha niwe mtumwa wa kijerumani na uholanzi,manchester united, sometimes simba sc
hapo bas
 
Mi hata siwazagi kuishabikia taifa starz mana hamna kitu pale hasa akina ngasa mi nashabikia team inayocheza na taifa starz
 
uzuri ni kwamba taifa stars ni serikali 2 na mimi nashabikia Tanganyika, taifa stars ni zao la kifisadi.,.
 
Nakuunga mkono mkuu.Husitake kuumiza moyo wako mara kwa mara kwa timu ya taifa.Hakuna kitu hapo.Tena itasaidia starz kubadilika labda hapo baadae.Lakini mkuu hata mimi ningekuwa hapo ningeshangilia sana Msumbiji
 
Mnaeweza kuthubutu kumshangilia adui,basi hata ukimfumania mkeo live utashangilia.Use less.

m

Kwenye mpira hakuna uadui.
walipocheza timu yenu na I.coast ulishabikia ipi? na I.Coast na japan kwnye w.c ipi?
 
Hata Petro alimkana YESU mara tatu kabla jogoo hajawika lakini MUNGU alimtumia
kuanzisha kanisa na anakumbukwa kama mmoja wa watakatifu leo..
.................... Deo Corleone utabakia kuwa Mtanzania tu.............
 
Kama nilivyokataa kuzishabikia timu za Afrika kwenye WC,ndivyo nilivyoacha kushabikia starz kuanzia leo.

Mechi inayofuata kati ya Stazi na mozambique nitashabikia Mozambique.

maumivu ya kushabikia starz nayajua mimi na nimechoka

Niiteni tu msaliti
Nakufananisha na mtu anayetaka kujiua kisha anaawatangazia watu. Hujawahi kuwa shabiki kindakindaki wa Stars, ulipoanza kuishabikia hukujinadi hapa. Ya nini kututangazia wakati unatoka?

Nenda mwanakwetu, washabikie hao ambao wala hawataki hiyo sapoti yako...
 
Unaiaga Taifa starz leo? Wengine tulishachana nayo hata kabla maximo hajawa kocha wa hii timu.

Inshort nimeachana na mpira wa Africa hasa Tanzania kipindi Micho anafundisha Yanga.

Kazi ushirikina na ujinga usiokuwa na maana. Timu inaendeshwa na wazee wa club wanaowaza uchawi kila sekunde.

Unamsajili jama mba wakati vijana wa rolling stone au copa coca wanarudi mtaani na vipaji vyao.

Africa tumelaaniwa.
Nakuunga mkono, Ulaya wanakozini watu wa jinsia moja, ndugu wanapakuana bila kusahau zinaa na wanyama ndiko amebarikiwa.
 
Uzalendo? Mini maanavya uzalendo? Kushabikia mambo ya hovyo ndiyo uzalendo!! Hapana uasi dhidi ya mambo ya hovyo ndiyo uzalendo.
Big up kwa Deo Corleone ingawa umechelewa Sana kufanya maamuzi.
Kuhusu Africa , ni Africa ipi mnayoiongelea?
Kama no Africa hii itoshe tu nikawaambieni kuwa katika maisha halisi Africa doesn't exist. Africa ipo kwenye museums, inaishi humo, you can plan a visit.
 
Last edited by a moderator:
Nakuunga mkono, Ulaya wanakozini watu wa jinsia moja, ndugu wanapakuana bila kusahau zinaa na wanyama ndiko amebarikiwa.

Wewe utaona hvyo ila hako kagari ulichonunua, nguo unayovaa, viatu, network unayotumia, au hyo simu unayotumia ni idea ya shoga fulani pale silicon valley, kwahyo hatuchekani.

Au rudi uwe kama mababu zetu
 
Wewe utaona hvyo ila hako kagari ulichonunua, nguo unayovaa, viatu, network unayotumia, au hyo simu unayotumia ni idea ya shoga fulani pale silicon valley, kwahyo hatuchekani.

Au rudi uwe kama mababu zetu
Ndio maana nimeilipia bob, kumbuka teknolojia za nguo, mahesabu na usafiri wa hali ya juu zilianzia Afrika. Sawa maamuma?
 
Kama nilivyokataa kuzishabikia timu za Afrika kwenye WC,ndivyo nilivyoacha kushabikia starz kuanzia leo.

Mechi inayofuata kati ya Stazi na mozambique nitashabikia Mozambique.

maumivu ya kushabikia starz nayajua mimi na nimechoka

Niiteni tu msaliti


Pamoja na kwamba una uhuru wa kushabikia chochote unachopenda ili mradi usivunje sheria, nataka kuwa wa kwanza kupingana waziwazi na msimamo wako na kuwaomba wengine pia wasikupongeze wala kukuunga mkono.

Waswahili tunatabia mbaya ya kupenda vya watu, na kupenda kufanyiwa vitu bila sisi kuumia. Pia tuna tabia ya kujipendekeza kwa vitu vya watu vilivyofanyiwa kazi kwa muda mrefu na watu waliosacrifice kufikia mafanikio hayo.Ulaya na popote mpira ulipoendelea, ni juhudi ya machozi, jasho na damu ktk uwekezaji, miundombinu, mifumo na utawala kwa ujumla wake, kitu ambacho Tanzania na sehemu nyingi ya Afrika, bado tunasuasua japo tunazidiana matatizo.

Hivi, wewe unavyowaponda Stars kiasi hicho unaweza kutueleza ni mchango gani umewahi kutoa kwa timu au soka la Tz kwa ujumla? Unawafundisha nini wachezaji waliojitoa kwa hali na mali ktk mechi zilizopita na hata hii kupata matokeo na mambo kuwa magumu kuliko uwezo wao? Wakati ninyi mnalalamikia sare kiasi hata cha kukufuru, kumbukeni mnawavunja nguvu na kutokuwatendea haki wachezaji na makocha waliopigana kiasi cha kuumia kupata angalau sare hiyo.

Matokeo yoyote tunayopata Tz, yako proportional na juhudi na uwekezaji tuliouweka. Na ni hivyohivyo katika sekta karibu zote. Tumepanda vichache, tukubali kuvuna vichache. Tuangalie tukipojikwaa sio tulipoangukia. Tunataka watu wanaokosoa na kuonyesha kutokuridhika na hali ya mambo huku pia wakitoa suluhisho la matatizo tuliyonayo, sio wakana timu na taifa.
 
Nilikuwa naipenda sana taifa stars ila kilichonitoa ni pale tuliposhinda Burkina faso ilivyokuwa inasifiwa kwa nyimbo kila kona ya nchi kama ndo tumeenda WORLD CUP nikaacha palepale.
Soka la bongo haliniumizi kichwa tofauti na matokeo mabaya ya CHELSEA.
 
Back
Top Bottom