Nitapata wapi na ntazitambuaje USB charger Original?

Nitapata wapi na ntazitambuaje USB charger Original?

LICHADI

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2015
Posts
4,727
Reaction score
13,466
Hivi sasa usb cable fake zimezagaa tanzania nzima, yani ukinunua zinakaa mda mfupi tu zinaungua au zinakufa kabisa, na hazijulikani zipi ni original na zipi ni fake yani nyingi ni majanga

sasa hebu wataalam tupeane uzoefu tutazitambua vp usb cable og, na zinapatikana wapi?
 
Njoo nikupe usb isipomaliza Mwaka...nirudishie nikupe Hela yako ila Tu inapoirudisha iwe vile vile nilivyokupa haijakatika wala haijachubuka..ichakae hata ipoteze rangi ila iwe tu vile vile..Nakuruhusu rudisha.

Usipokuja kwangu nenda kanunue Oraimo/Amazon/Nokia hizi brand 3 zina usb nzuri sana japo zina Fake zake pia nyingi zimetoka na ndio wanazouziwa watu.

Mimi situmiii hata aina moja ya hizo Brand hapo Juu nina USB haina Jina hata dukani haina Jina ina mwaka wa pili...niliichukua dukani mwaka juzi x.mass Ninayo hadi leo.
 
Usb haitaki mbwe mbwe hata ukinunua hizo brand Original itunze..usiikunje kunje... Brand hizo tatu za Oraimo/Nokia/Amazon zina aina mbili mbili za usb yani zipo usb Refu na Fupi...Wamefanya hivyo makusudi kwasababu wanajua USB haitakiwi kukunjwa kunjwa au kusokotwa kama NGATA.

usb refu zao zina kama 1Meter(ambazo ndio kila mtumiaji humu anatumia)
usb fupi zao zina urefu wa kiganja Chako..hizi ni kwa ajili ya kuzurula nazo maana ni kadogo na hautokakunja unakatupia kwenye BEGI kakiwa kazima hivyo hivyo..

Ila hizo refu ukiiweka kwenye begi lazima itajikunja..na ukiwa mtu wakuitumia kila mahali kuna siku utaamka utachomeka haitopeleka yani itakua ishakufa.

Ukihitaji uhakika siku hizi kuna mabegi ya mgongoni yenye USB kwa ndani na p.bank...waharibifu wa usb na wasahaulifu hayo yanawafaaa.
 
Sasa unakuta unanunua usb ya elfu tano sijui nane yaan hapo lazma utalia kila sku chukua oraimo og 12000 unaeza pata
 
Kanunue oraimo, ukiweza nunua na powerbank yake... ufurahie maisha, maana siku hizi charger og ni mchongo kuliko kiwanja...! 😂😂😂 ila hakikisha imeandikwa oraimo
 
Back
Top Bottom