Nitapata wapi kitabu cha Allan Gwartaman?

Nitapata wapi kitabu cha Allan Gwartaman?

slowpancha

Senior Member
Joined
Jul 27, 2014
Posts
184
Reaction score
102
hiki kitabu cha hekaya za allan gwantaman nilikisoma miaka ya nyuma,nakitafuta nikisome tena.mwenye kuweza kijua nitakipata wapi anisaidie wadau
 
unamaanisha allan quartermain, katafute movies zake zimejieleza kama allan quartermain and the lost city of gold, King solomon mines, kama ni huyo,
 
Allan alikuwa ni character aliekuwa anatumiwa na mtunzi sir richard haggerd akiwa na wenzie kama henry Curtis,(inkubu )yaani tembo, pia umslopogaas, john good au bwana bougwan pia umbopa hao walikuwa washiriki wa allan katika vitabu tofauti sasa ungesema jina la kitabu kama mchangiaji hapo juu alivyojitahidi kukuelimisha pia napenda kusema tena ukipata kitabu unakuwa upo uzuri kuliko alieona picha coz matukio mengi yamefutwa au kupunguzwa katika picha.
Nahisi utakuwa ulisoma hadithi ya 'Allan quartamain na wenzake ".humo ndo utamkuta umslopogaaz na swaga zake za kizulu acha nikuonjeshe.
Maneno yako yote unayoyasema si ya kweli makumazahn sikuangamia kwa kupenda ukubwa na nguvu zaidi ila ni aibu juu yangu kusema ni uso mzuri wa mwanamke ndio ulioniangusha na sasa tutaona mambo kama tulioyaona zamani makumazahn? tulipowinda na kupigana katika nchi ya uzulu? ndio nitakuja! ikiwa kwa maisha !ama kwa mauti ni mamoja kwangu! mapigano yaanguke upesi na damu imwagike,nimepigana vita kwa miaka arobaini, nimekuwa mtu wa vita kuliko watu wa vita.
 
hiki kitabu cha hekaya za allan gwantaman nilikisoma miaka ya nyuma,nakitafuta nikisome tena.mwenye kuweza kijua nitakipata wapi anisaidie wadau

Daah..kaka kitabu cha Allan nakumbuka nilikisoma enzi hizo nipo Dakawa na mwanangu wa ukweli Abdul ( Potter) he was a real friend..umenikumbusha mbali sana aisee..!!
 
hiki kitabu cha hekaya za allan gwantaman nilikisoma miaka ya nyuma,nakitafuta nikisome tena.mwenye kuweza kijua nitakipata wapi anisaidie wadau

Mkuu Allan Quarterman vitabu vyake maarufu vya Kiswahili ni Machimbo ya mfalme Suleiman na Safari ya nchi ya watu weupe (Wazuvendi)
hiko cha kwanza- mashimo, kinapatikana katika maduka ya vitabu posta ila hiki cha pili adimu.

Mimi ninavyo vyote viwili lakini kuazimisha nilishaacha baada ya kupoteza vitabu vyangu kadhaa adimu
 
kaka napenda hilo jina la akajase mbamba nlisoma vitabu vyake zamani.sijui kama unaweza kuvipata au unavyo.
 
yaah mzee mwenye shoka mkuu wa kikosi cha nkomabakosi mwana wa makedema mimi nawaita kama kulungu aitwavyo.
 
Wakuu
Wabongo tunafurahisha sana. Kati ya wachangiaji wote wa uzi huu hakuna aliye jibu swali la mwanzilishi wa uzi huu.
Hakutaka kumbukumbu za inkoskazi na msolopagazi ameuliza wapi atapata kitabu hiki.
Je majibu hayo yanatuweka level ipi kwenye issue ya kureason.
 
Mkuu refer post #5 by Hikma ameshajibu swali.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom