nitampataje

nitampataje

KICHUMVI

Senior Member
Joined
Aug 12, 2012
Posts
113
Reaction score
14
habar wana jf
wiki moja imepita sasa nilikuwa nimekwenda chuo kikokwe kufuatilia chet changu katika kurusha macho uku na uko nikatokea kumwona mdada mmoja mzuri, kiukwel amenivutia ile sana nilitamani awe mke wangu, ilikuwa sehemu ya chakula alikuwa amekaa wakati mimi nahudumiwa! bila kusita na japokuwa zilikuwa sehemu nyingi ziko wazi za kukaa ikanibidi niende alipokuwa amekaa yeye na kumwomba tukae wote,nae bila kinyongo alinikaribisha,tulifahamiana na alikuwa hajisikii kula lakin nilimshawishi kula chakula ambacho niligharamia mimi,tulimaliza kula akaomba nimsindikize anaelekea darasan ,nami nikamsindikiza kila ninapotaka kuishia aniambia tuendelee ,gafla akapigiwa simu sikujua ilikuwa inatoka wapi maana ilimstua na hakuwa na muda tena wa kuongea.nikajikuta nimetoa businesscard yangu na kumpa nikimsihii baadae anitafute kwa haraka akaichukua na kukimbia alipopigiwa simu,
jamani jaman leo siku ya 7 cjapata ata missed call ya namba mpya najuta kwanini sikuchukua namba yake muda wote,namfikiria yeye jinsi alivyonikosha moyon nimetokea kumpenda sana jinsi alivyo na ata sijui nitampataje nachokumbuka jina lake moja la kwanza na bado sina hakika nalo,course anayosoma,mwaka anaosoma na hall analoishi sina zaidi ya details hizo,naombeni mnishauri nitampataje ili nimwambie yangu ya moyoni na nilishakosea kutochukua namba yake tangu mwazon, anitoki kichwa kila cku namkumbuka yeye tu.
 
potezea tuu...baaada ya wiki mbili utamuona mrembo mwengine
 
Mmmh pole...huyo ninamashaka nae pili wewe hata kwenye kutongoza unatoa business card?

Hahaha aisee tafuta kozi bwana...it shuld be exchange of numbers not one way around
 
Yaani ulimkuta kakaa na misosi ambayo hana appettite nayo, na kisha ukalipia na kumshawishi kula?
Naomba tukutane udasa lunch time tafadhali.
 
Rudi eneo la tukio mda na wakati uleule utamkuta tu mana ile ndio ofis yake ya kula vichwa vya waliobarikiwa macaring kama wewe
 
Rudi chuo kamsake tena usikubali kumkosa.....!!!!!
Afu wanachuo huwa hawahitaji maneno mengi, ile b'card uliiambatanisha na pesa au kadi tu chukuchuku?
 
Hiyo sim aliyopokea ni ya yule aliyekuwa anamsubiria hiyo sehemu ya chakula, ndio maana alivyoona muda unakaribia msela wake kufika akakuzuga umsindikize darasani.
 
Charger amenena vema sana. Ungemuachia ATM card na business card yako usingepata tabu sana.
 
we boya kweli, kila kizuri kinamwenyewe, asa unampa business card yako ambayo si unafanyia kazi wapi sijui, wenzako wanatoa business card anafanyia kazi sehemu ya maana, ebu edit hiyo business card yako andika unafanya kazi BOT manager mikopo, au TRA
 
Milima haikutan ila watu wnakutana subiri utakuja kukutana neye one tyme au vuta hatua nenda hapo chuon pengne waweza kutana naye kaka

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
mda wote mmeagizia chakula mmekula,mlikua mnaongea vinini hivo
hadi umeshindwa kuulizia detalis za muhimu
 
Mmmh pole...huyo ninamashaka nae pili wewe hata kwenye kutongoza unatoa business card?

Hahaha aisee tafuta kozi bwana...it shuld be exchange of numbers not one way around
hapana ndugu sikumtongoza na wala sikuwa na haraka ya ivyo kwani nilihisi kumpenda kweli na ndyo maana nikampa bussinesscard ila anitafute maana alikuwa na haraka baada ya kupigiwa simu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom