Michosho
JF-Expert Member
- Mar 17, 2012
- 662
- 651
Hiyo imekuwa ni kauli ya mke wangu,niliyezaa naemtoto mmoja,ambaye ana umri wa miezi 9.Kauli hiyo amekuwa akiitoa mara kwa mara hasa kunapotokea ungomvi(mara nyingi unatokana na wivu mwingi alo nao) wa aina yeyote ile unaopelekea kupigana.
Hayo maneno ya kuwa ipo siku ataniua ,nimekuwa nikijiuliza sana,endapo anamaanisha au ni hasira tu!!Kila nikitafakali na kuangalia mwenendo wake na tabia yake, nashindwa kuelewa km ni kweli hilo suala lipo kichwani mwake kwa maana ipo siku atalitekeleza ua la!!.ni miaka 3 imepita tangu tuanze maisha na huyu mke wangu.
Suala hili nalileta kwenu JF MEMBERS,mnipe walau mwanga wa nini nifanye juu ya hii kauli ya mke wangu.
Natanguliza shukrani kwa mchango wenu wadau.
Suala hili nalileta kwenu JF MEMBERS,mnipe walau mwanga wa nini nifanye juu ya hii kauli ya mke wangu.
Natanguliza shukrani kwa mchango wenu wadau.