Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 11,824
- 18,066
- Rais aliyeingia madarakani kwa ahadi lukuki na kuwapa matumaini makubwa Watanzania kuwa na maisha bora!
- Rais aliyeingia Ikulu kwa bwembwe kubwa na wafuasi wengi!
- Rais aliyeunda baraza kubwa la mawaziri kuliko wote waliomtangulia!
- Rais aliyeteuwa viongozi vijana wengi na hasa wanawake kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi!
- Rais aliyeanzisha mikoa na wilaya nyingi nchini bila kuzingatia uwezo wa kiuchumi na kiutawala wa serikali yake!
- Rais aliyeteuwa majaji wengi bila kuandaa mazingira mazuri ya utendaji wao na uwezo wa kifedha wa serikali yake kuwahudumia!
- Rais aliyeteuwa viongozi wengi wake kwa waume, wazee kwa vijana kwa kuzingatia ushwahiba badala ya uwezo na uzoefu wa kazi au taaluma husika!
- Rais aliyefanya safari nyingi za nje kuliko wote waliomtangulia na hata kuvunja rekodi kwa viongozi wa bara la Afrika!
- Rais aliyedidimiza uchumi kwa kiasi kikubwa kwa kukosa mipango sahihi!
- Rais aliyeshindwa kukemea maovu na waovu katika serikali yake kwa kuogopa lawama!
ATHARI KWA TAIFA:
- Ukubwa wa serikali umekuwa mzigo mkubwa kulingana na uwezo wa kiuchumi wa Taifa.
- Serikali imeshindwa kupata fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo na hivyo kusababisha miradi mingi kusuasua.
- Mfumuko wa bei umekuwa mkubwa na hivyo kuathiri wananchi wengi wenye kipato cha kati na chini.
- Wananchi wengi wamekata tamaa ya kuwa na maisha bora kama walivyoahidiwa.
- Taifa limekosa dira ya maendeleo kwa kutokuwa na hakika ya fedha.