Keshokutwa nategemea kwenda Mbeya kikazi na nitakuwepo pale kwa siku 5. Sijawahi kufika kabisa nyada za juu kusini, naombeni mnitajie basi zuri na linalokimbia sana ili niwahi kufika jijini Mbeya mapema. Karibuni mtiririke wadau...
Nilizafiri na ndenjela mwaka jana ni zuri ila mbeya tarajia kwenye saa mbili usiku,
Ila Ilas ndio habari ya mjini mbeya ni saa kumi na mbili jioni.Hili ndio basi lenye kasi zaidi kwa njio hio lenyewe linapita mbeya kwenda Tunduma.
Rungwe express is the best! Huduma nzuri, lugha nzuri, mwendo mzuri na uhakika wa kufika na mkubwa. Usisahau gloves, sweta/koti zito, mafuta ya mgando na kofia.
Ndenjela imechoka siku hizi wewe. Nimepanda tarehe 23 Mei Dar to Mbeya hata huduma za soda hakuna,wale wadada wahudumu hawapo. Siti ngumuu zinaumiza matako. Pia hakuna USB za kuchajia simu. Kibaya zaidi tulifika Mbeya saa 5 usiku.
Ni bora kupanda Dar lux, Happy nation(mpya) au Rungwe.