Nitafungaje FB, insta, na whatsapp zisitumike katika simu

Nitafungaje FB, insta, na whatsapp zisitumike katika simu

Wadau watoto wangu nikiacha simu tu sheeda utakuta wanatembelea mitandao yoote ya kijamii nahitaji anayejua kulock hiyo mitandao ktk simu sio kuweka password

Ninadhani hakuna kitu hicho. Maana hata ukipiga password, wataingia kwa akaunti zao.

Aidha, kama kuna kitu kinachonishangaza kwa baadhi ya wazazi ni kushindwa kudhibiti watoto kushika simu zenu! Hivi mnashindwaje? Mbona mimi nina watoto na hawagusi simu yangu?Yani mpaka niamue mimi kuwaonyesha jambo ndiyo muda wa wao kuona na kushika simu yangu. Na amini usiamini bado watoto wangu ni rafiki zangu sana tu kuliko hata kwa mama yao. Ninajua namna ya kuwafurahisha kupitia vitu ambavyo ni haki zao toka kwa baba yao. Nawasihi mbadilike na inawezekana.

Ninawasilisha
 
app hider ndio suluhisho kwa hicho unachotaka kufanya Google apphider apk sijui kama play store itakuwepo then install hiyo itaficha app unazozitaka na unaweza kutumia pale unapohitaji


Kama watoto wenyewe ni wale dadyyyy...mumyyyyyy....! akigusa kitu, utasikia heh! jamani Prince anaweza kufungua simu, wow! Hao hata afiche wapi lazima ipo siku watajua tu. Maana watoto si wajinga kihivyo, si ajabu wao ndiyo watakufundisha namna ya ku-hide.
 
Back
Top Bottom