Nitaficha wapi uso wangu? Rais Kikwete ameniumbua


Anaeweza kukuumbuwa ni yule aliyekuumba tu.

Wacha ushirikina kudhani kuwa binaadam mwenzio anaweza kukuumbuwa.
 
Tena licha ya Ikulu, Mjerumani kafanya kweli, reli ya kati mpaka leo.

Barabara karibu zote unazotumia leo ni zile zile za Mjerumani, sanasana tumezipanuwa na kuweka lami.

Nenda Tanga, moja katika miji ambayo imepangika vizuri na hiyo ni toka Mjerumani, si leo.

Ukweli ubaki kuwa ukweli. Natamani tungebaki kutawaliwa na Wajerumani hadi leo hii. Hatuwezi lolote.
 
Kuna wakati Rais Kikwete aliwahi kusema hii nchi ina viwanda vya kutengeneza uongo...

Vyovyote vile mimi naamini utawala wa Mjerumani ulikuwa na manufaa maradufu ya Mwingereza.
kwani mleta mada kasemaje?
 

Kwa nini CCM wanashindwa kuendesha nchi Kama walivyoiendesha Wajerumani?
 
bado naona ww mawlm ndo una matatizo...... katika kufundishabkwako koooote hujaaahi kuona swali la "colonial rule was brea and butter to Africans discuss "........we unadhan hapo utabishana na swali.....


nenda kasome tena
 
Kama JK amesema hivyo basi mwacheni Mugabe aitwe Mugabe. Hiyo ni aibu kwetu sote na ndo maana tunahitaji Raisi mwenye macho ya tofauti kuwafundisha watanzania kuwa wanaweza na wajiamini waondokane na mtazamo wa kutembeza bakuli dunia nzima
 
Ninawasiwasi na baadh ya wachangia thread kama kwel ni great thinkers kwa wanavyofagilia ukolon.
Da! Mleta mada mi nahis kuna wajeruman humu jf.
 

Sometimes huwa nawashangaa sana watu wanaosema shule za kata na chuo kikuu DODOMA kimejengwa na JK.

Ninavokumbuka hizi shule zilianza kujengwa 2004 wakati Benja M akiwa bado madarakani. UDOM pia kilianza kujengwa kipindi cha MKAPA.

Ifike mahali watu tuwe wakweli na sio kuleta propaganda mfu ambazo hazijengi???
 
Siamini kuwa alisema hivyo, hataaa haiingii akilini kwa Rais tena Prof. APONGEZE WATU WALIOTULETEA ADHABU YA KIFO
 
sisi tunawashukuru Wajerumani kutuletea Lutheran church,machame yote ni walutheri,ingekuwa siyo wakoloni inawezekana kilimanjaro yote ile ingekuwa kama Tanga vibaghashia kila kona,Thank you Jesus

So your the best human because of your belief? Mental slavery
 
Haa haa, kikwete haishi vituko! Si angewaomba waje tena kututawala angalau kwa miezi 8 kuanzia sasa?
 
Waarabu walileta Utumwa na kujitoa muhanga tuu
 

Hatujashindwa kujenga ikulu yetu, ninadhani ni suala la maamuzi tu, majengo mangapi ya thamani ya hali ya juu yamejengwa including nyumba ya J.K Nyerere, makumbusho ya Nyerere kule Musoma, na Nyumba za marais wastaafu kama ya Mwinyi, Mkapa, na hata ile ya Kikwete pale Msoga zote zinajengwa kwa pesa ya watanzania. Nadhani pesa ya kujenga ikulu pale Dodoma ipo tatizo hawataki kuhamia kule sababu ya per diem huo ndio ukweli.
 
Siamini leo watu wanashukuru wajerumani jamani someni Historia najua maisha magumu yamewachanganya ndugu zangu watanganyika hamna cha kuwashukuru mali zetu ndio zimeijenga berlin!!! Wao ndio watushukuruu dah
 
Wewe kachukue buku saba ukapumzike,kwamba babu zako walibebeshwa mataruma ya reli begani na wengi kufa kwa mateso bado unasema walikuachia miundo mbinu?????hivi ikulu inatengewa bajeti ya shilingi ngapi kila mwaka toka 2005???? hizo pekee hazitoshi kujenga IKULU nyingine DODOMA,acheni akili mgando kama za CHINESE PROFESSOR
katika mataifa yote wajerumani pekee ndiyo ambao angalau walituachia majengo na miundo mbinu kadhaa.
 
Haya ndiyo matokeo ya kuendekeza njaa,kayasema haya Ili asinyimwe kibaba,hizi zote ni mbinu za kuombea kibaba maana serekali ya chama cha kina fulani inapenda sana kuomba na bila kuomba kibaba serekali haipo,imekuwa serekali ya kuendeshwa kwa kutegemea vibaba vya kuomba,siku mwenye vibaba akikataa kutoa vibaba watanzania ndiyo watakufa kwa njaa.

Ni kweli wakoloni walifanya mambo mengi mazuri tena kwa uadilifu mkubwa pengine hata kushinda watawala wetu wa sasa,kitu kinachoitwa ufisadi kwao hakikuwepo kwao,pamoja na mazuri waliyoyafanya,Je ni vitu vingapi walichukua kwetu?,Je hayo mazuri waliyo yafanya tena kwa kutumia kodi ya wananchi wa ujerumani waliyafanya kwa hasara pasipo kupata faida yoyote?

Hapa ndipo ninapo mkumbuka mzee wa uzanaki angewasema kwanza tena kwa maneno makali yaliyojaa maudhi lakini mwisho angemalizia kwa kuwaomba msaada na kuwaambia kuwa hivi vitu mnavyotusaidia ni mali zetu mlizotupora kwa hiyo mnaturudishia mali zetu.
 
Faiza nadhani mababu zetu waliotangilia mbele ya haki wangeisikia kauli hii wangekuchuna ngozi,sema wewe na serikali yako ndo hamuwezi lolote hivyo basi wapisheni wanaoweza kazi hapo magogoni msaidiwe maana imeshawashinda!!!!Kwamba unasifia ukoloni kwamba wametujengea barabara na kutupangia mji wa Tanga hii mishahara mnaowalipa TOWN PLANNERS ni za nini???? haya mabilioni mnayoyatafuna hapo BOT yangetosha kujenga barabara ngapi zetu kama watanzania???Unyama uliofanya na kila TOM VON PRINCE na wengineo unausifia,historia tunaijua nashauri mkawadanganye huko vijijini wasiojua historia ya unyama wa wajerumani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…