Nitaendelea kuwaheshimu waliosoma chuo kikuu kuanzia huko Nyuma mpaka walau 2010, siku hizi kitu ni full ku claim kuwa na Universal knowledge

Nyinyii ambao mlisoma vizuri na kupata elimu bora kama mnavyojinasibu wenyewe ndo wanafiki wakubwa na ndio mlioifikisha hii nchi hapa tulipo na hiyo elimu mnayoiponda.


Wengi wenu kila siku mnahubili vijana mjiajiri wakati huo nyie mnang'ang'ania madaraka. Mkitumbuliwa mnalia lia ovyo .what a shame ..!!
Jiangalie wewe babu au ushachukua buku saba yako Lumumba unakuja kutoa pumba zako hapa .
enheee britanicca njoo hapa
 
Jumapili hii najua mpo salama mkiwa mnaendelea kumsaka tycoon viunga vya Dsm,

So Mara ya kwanza kupigia kelele juu ya kushuka kwa elimu yetu, na ukiongea sana utaonekana unasumbua taifa,

Maana ya universal ni kwamba kila kitu, inamaana wa University uwe na simple general knowledge , Kuna vitu vidogo vidogo ambavyo mtu uliwahi kuvisoma uko Nyuma kabla ya kufika chuo kikuu lazima uvijue, Leo hii mwanafunzi wa chuo kikuu hajui mambo madogo madogo, alafu unamtetea eti siyo specialization yake??

AAUNIVERSITY UNIVERSITY STUDENT MUST HAVE WHAT WE CALL UNIVERSAL KNOWLEDGE

Miaka ya hivi karibuni mwanafunzi wa chuo kikuu anaweza ulizwa swali la darasa la tano akashindwa na kisingizio ikawa kwamba siyo specialization yangu!!!!

Mambo ambayo kabla hajafika chuo kikuu aliyapitia katika madarasa ya chini Leo hii anasema siyo specialization yake,

Uwezo wa wanafunzi wa vyuo vikuu wa sasa hivi wa kufikiri na kutunza kumbukumbu uko chini ya uwezo wa mwanafunzi wa kidato cha nne wa mwaka 1995 ambaye alikuwa vizuri kichwani

Je tunavyosoma huu uzi unajua kuna wanafunzi wa chuo kikuu hawajui kutofautisha Kati ya HERUFI NA TARAKIMU??
KONSONANTI NA ILABU?? Ukiwauliza eti siyo specialization yao,

Leo hii mambo ambayo sisi tuliyafanya tukiwa sekondari kabla ya kujiunga vyuo vikuu tuliyafanya hawawezi, mtafte mwanafunzi wa chuo kikuu akuchoree ramani ya Africa tu asiweke nchi achore boma tu, utaona maajabu,

Leo hiii muulize mwanafunzi wa chuo kikuu tofauti ya league of Nations na UNO hawezi, ambayo ni masuala ya form three ambayo kila mtu kayapitia hata kama hajayapitia angalau ayasome kwenye juhudi zake extra time ,lakin hawajui

Waulize Hata vitu simple tu kama UNO OAU ziliundwa mwaka gani,

Waulize tu wakwambie waziri mkuu wa kwanza wa Tanzania hawamjui kabisa,

Waulize tu vitu simple sana kwamba Thomas Sankara ni wa wapi hawana majibu

Waulize tu tofauti ya namba kuanzia na zero kwenye kuziorodhesha na kuanzia na moja ipo ni ipi na majina ya orodha hizo mbili ni yapi hawajui

Nimeshangaa sana kukutana na mwanafunzi wa chuo kikuu hajui hata Africa ina nchi ngapi hahaha hatari sana tena

Mwanafunzi wa chuo kikuu wa sasa anajaza simu bundle kufuatilia Tanthiliya za kifilipino akili zimezama uko,


Asante kwa kuendelea kutukumbusha. Hakika mwenye kuelewa hawezi pinga hoja yako, elimu yetu ina shida. Lakini, kwakuwa wewe mwenyewe umesema wahitimu wetu wa sasa hawajui mambo "madogo madogo", nikaanza kufuatilia uandishi wako. Baada ya kusoma mara kadhaa, na wewe nikaona upo kundi hili unalolishutumu (kutojua mambo madogo madogo). Sasa wewe unaekosoa huwezi kuandika neno HALAFU, pia huwezi kuandika neno IRABU. Na tatizo hili limekuwa kubwa zaidi kipindi hikihiki unachokizungumzia. Hivyo, kwa pamoja, tukiri tuna tatizo na ikibidi tulifanyie kazi.

Asante sana kwa kutukumbusha.

Admitting failure is quite cleansing, but never -pleasurable (Michael Morpurgo)
 
Acha upumbav.u, Hizo ni akili kisoda,nikariri historia zisizo na maana Za nini.
Watu wanawaza mambo ya karne ya 21 kuhusu artificial intelligence,bitcoin,fintech na mengineyo wewe unaleta habari za Sankara nyakati zao zilishapita.
Zeeka na ujinga wako.
Yale yaleeee
 
Siku hizi wanalipa pesa kuweka alama nzuri kwenye makaratasi (nyie mnaita vyeti) kisha wanakutana Club na Lecturer kuzichafua psychology zao
 
ukienda pale UDOM ndo hopeless kabisa. Kile Chuo cha kata lectures na wanafunzi wanakata kata tu viuno kitandani.
 
Nyie mliosoma zamani si ndio type za Polepole ,jpm (huyu ana phd ya UDSM kabisa), Lowasa aliyetufikisha hapa tulipo..

Hicho kizazi cha 2010 kurudi nyuma hamna cha kujivunia hata kidogo maana maisha tuliyoyakuta ni magumu tu .
Kujua kwenu tofauti ya UN na AU hakujabadirisha maisha kwa namna yoyote sana mlikua mnakariri mambo yasiyowasaidia kitu

Hata malecture wanaofundisha sasa hivi ni nyie nyie mliosoma zamani.
Sasa tatizo ni nani?? Tafakari
essay yako ina logic kubwa " sana .. in short imeusuta huu uzi vyema kabisa
 
Acha upumbav.u, Hizo ni akili kisoda,nikariri historia zisizo na maana Za nini.
Watu wanawaza mambo ya karne ya 21 kuhusu artificial intelligence,bitcoin,fintech na mengineyo wewe unaleta habari za Sankara nyakati zao zilishapita.
Zeeka na ujinga wako.
hahaa
 
ukienda pale UDOM ndo hopeless kabisa. Kile Chuo cha kata lectures na wanafunzi wanakata kata tu viuno kitandani.
Unaweza kukuta nyuma ya keyboard limekaa jamaa hata form 4 lilipata div 4 halafu unapata nguvu za kumponda professor wa UDOM.

maana mtu aliyesoma akaelimika hawezi kuandika kama wewe
 
Wewe kumjua waziri mkuu wa kwanza inakusaidia nini au inalisaidia nini taifa ? Kujua UN imeanzishwa mwaka gani kumekusaidiaje mpaka hapa ulipo ?

Duh! Wewe umefunika. Hahahahahha! Hii kauli yako si ajabu inathibitisha hoja ya mtoa hoja. Umenichekesha sanaaaa!
 
Back
Top Bottom