Tembelea hospitalini kuwaona na kuwajulia hali wagonjwa na walemavu na kujua wamepata matatizo gani. Wapelekee zawadi na kuwafariji watoto yatima pamoja na kuwa hoji waliyoyapitia mpaka hapo walipo wamepitia hatua gani.
Kuwa na utamaduni wa kutembea na kujifunza mbali japo kipindi cha likizo makumbusho, vijijini, wafungwa, kambi za wakimbizi nk
Sisi sote ni binadamu, asili yetu ni adam na hawa(eva), tumezaliwa na mama (mama yako wewe ndio mama yangu mimi) bila kujua wala kutegemea ni kiumbe gani atatoka na mapungufu gani..wapo waliozaliwa bila upeo wa macho(vipofu), viziwi, walemavu, wafupi, weusi, weupe, albino, wengine hawana miguu wala mikono.
jifunze upendo kwani kuna leo na kesho, tusiwabague kwa mapungufu yao hawakupenda kuwa hivyo.
Kuna maradhi, ajali hujafa hujaumbika