feyzal, Umemwambia kinadharia, watu wengi binafsi wanafungua zahanati na sana sana health centre, na wengi hawana uwezo wa kumwajiri MD hivyo CO huwa wana Soko sana kwasababu atleast cheap ukilinganisha na MD. Hata ajira za government utakuta CO 200 na MD 50 tu kwasababu ni rahisi kuwalipa.
Kwa mfano Health centre inatakiwa iwe na MD mmoja wakati CO 4, zahanati huko CO ndo wanatakiwa na CA, Kikubwa kinachompa CO ajira kirahisi na kama nilivyosema hapo juu, unafuu kwenye kuwalipa. So kama anataka ajira faster apige CO.
Ila kwa upande wangu ningemshauri apige diploma ya Lab, japo ajira zake sio nyingi kihivyo maana certificate wa hiyo kozi ndo wanachukuliwa wengi zaidi kwenye ajira. Faida yake ni moja, rahisi sana kupata chuo cha kufundisha, na pia kwasababu wengi wanafungua dispensary na health centre cheti cha mtaalamu wa maabara ni muhimu sana, so anaweza kupiga pesa.
Kuhusu pharmacy, labda uishi mjini, theoretically Inaonekana ni bonge la kozi ila practically sio rahisi hivyo kwenye ajira, ni kozi ambayo ili ikulipe unahitaji uwe na connection ya kutosha, maana ajira za kutangazwa kwa kozi hiyo sio nyingi sana na competition ni kubwa hasa kwa miaka ya hivi karibuni, but kama una connection utakula maisha.
Japo hujaitaja ila Nursing ni bonge la kozi ukitaka usisote mtaani piga hiyo kozi, iwe certificate au diploma, wew ni marketable, maana nurses ndo moyo wa hospital, na wanatakiwa sana, japo wanaume wengi hawaipendi hii kozi, ila mambo yamebadilika sana, Sio sawa na zamani. Watu wameelimika siku hizi.
Hizo zingine sizijui, so siwezi kuzizungumzia.
NB, ambacho nimekiandika ni from my experience sio blah blah za mitaani. Ni sehemu ambako nipo kwa miaka kadhaa sasa, so nilichoandika ndiyo hali halisi.
KARIBU....