Nisipokuambia wewe nimuambie nani?

Nisipokuambia wewe nimuambie nani?

Weee mpeeeee nakuambia mpeeee alafu mumewe atakusalimia kwa style ya kipekee hahahha mke ya mutu sumu ooohhh
 

Naombeni ushauri hii mizinga nimeichoka

Hiyo quote hapo juu ndo ilipasa umuambie huyo dada na si wana JF.

NB: Hata kama hii ishu umetunga ila kiukweli hii ipo na nina vivid example ambayo imenitokea mimi mwenyewe. Ni msichana ambae tulimaliza nae O-level na kwa kipindi hicho tulikuwa na mahusiano. Tukapotezana baada ya kumaliza shule. Mwaka huu mwezi wa 7 tukakutana bila ya kutarajia. Akanambia kuwa ameolewa na wana watoto wawili na mumewe na akanipeleka mpaka wanapoishi na mumewe na kunitambulisha.

Basi baada ya mda kidogo nikaona ameanza tabia ya kunieleza shida za kwao, kila siku shida zake. Mwanzo nilimsaidia ila nilivyoona inazidi ikabidi nianze kukaa nae mbali na pia kila akinipiga mzinga nilikuwa namuambia kuwa nina matatizo ya mshahara ofisini na bado halijatatuliwa, so hata mi mwenyewe nipo kwenye hali mbaya. Nikimwambia amwambia mumewe anasema eti hamjali. Kila akiniomba, namwambia bado ofisini hawajarekebisha..basi mwisho mwenyewe akaacha.
 
Sasa huyo si ameshakuwa mke wa mtu? Kama ni msaada unaweza kutoa kama kwa rafiki wa kawaida lakini siyo yeye kukufanya wewe ndo nyumba ndogo yake au ATM machine yake. Siku ukikamatwa ndo utajua ubaya wa kula vya watu!
Nakushauri, tafuta mwingine wa kwako, acha kupoteza muda na vya watu au kuwekeza sehemu ambayo hailipi, utakuja kujuta baadaye
 
wwe nawe utakua unamtaka huyo mwanamke, haiingii akilini ukaribu na mke wa mtu unautoa wapi!!! kaa mbali na mke wa mtu , afu inaonekana unajionyesha una pesa kwake!!
 
Back
Top Bottom