Nishaurini niweze kusahau

zema21

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
619
251
heshima zenu wakuu,
Ni mwaka wa tatu sasa kuna jambo linanisumbua saaana sijui kwanini nashindwa kulisahau...
Nakumbuka nikiwa chuo kuna binti fulani nilikuwa nampendaa mno kupita maelezo! Nilimuaproach na akanikubali..akawa ndo first lover wangu.. hatukupita muda mrefu yapata miezi 4 hv akaanza visa akawa anatafuta sababu mwisho wa siku bila sababu yoyote tukaachana tena kwa ugomvi na akanikashfu na kunipa maneno ya dharau mengi mno ya kutosha!!!!!
iliniuma mno lakini baada ya muda kupita nilitamani saana kuongea naye tu kwa ajili ya kutatua ugomvi japo tumeachana tusijengeane uadui!akakataaa
haikupita miezi 8 nikasikia ana jamaa mwingine pale pale chuo ila amechana nae tena kwa staili ile bila sababu.........
mwaka jana akaolewa.....
tatizo langu ni kwamba huwa namkumbuka sana nakaa nawaza jinsi alivyonifanyia, manake sikutegea wala kufikiria atanifanyia vile wala kunisaliti, nilimuamini mno nikampa moyo wangu 100%.. niliumia mno kupita maelezo manake nilipenda mno...
rafiki zangu, washkaji wakawa wamepata story za kuongea manake wabongo ndo tulivyo...
naomba wanajamvi (MMU), mnisaidie niweze kumsahau na kusahau yote yaliyotokea hata nikikutana nae nichukulie kama sikuwahi kumfahamu b4.. manake huwa tunakutana mara kwa mara...
 
kamuombe tena mkuu mechi nyingine!
wee miaka 3 bado unamuwaza mwanamke!
 
Potezea mkuu muone kama mzibua mitaro ya maji machafu usimvaliyu ukimpa samani na wewe ulikuwa unampenda kupita maelezo basi itakuumiza sana!!
 
Dah! Alikupa 0713 nn? We mwanaume bana acha hizo vitu.. Mbona wanawake wengi sana mkuu!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Ndio tatizo la kuanza mapenzi ukiwa chuo. Yan leo hii hadi watoto wadogo hawana stress kama zako, nao wanamega na kusepa. Tafuta mwanamke mwingine.
 
Wakuu nimewasoma, nimewaelewa! ila naomba niwashauri mtu anapokuwa na tatizo usimshauri kwa kumponda si vizuri.......
Afu tatzo la kupenda too much ndo hilo!!
But my problem is huyo mwanamke baada ya kuolewa imetokea kama bahati mbaya tunaishi naye mtaa mmoja hapa jijini
 
ni kawaida kabisa, sometimes kuongea naye mara moja moja hupunguza machungu.

Jipe muda tu.
 
Hebu fikiria alichofanywa kamanda barlow,hakika ni tiba tosha itakayokuondole maumivu na kusahau kabisa
 
Kweli moyo wako mgumu sana! Usijali tafuta mwingine anaweza kukusaidia kumsahau
 
concentrate na maisha yako,baada ya miaka 10 ijayo,utajiona mjinga kwa kumfikiria mtu ambae amekumwaga.pengine huyo baadae itakula kwake.maisha ni mzunguko,wewe hayo yachukulie ni moja ya safari ndefu ya maisha
 
dont fall in love with the dreamer again. but know that forgiveness is your desicion :smiling:
 
heshima zenu wakuu,
Ni mwaka wa tatu sasa kuna jambo linanisumbua saaana sijui kwanini nashindwa kulisahau...
Nakumbuka nikiwa chuo kuna binti fulani nilikuwa nampendaa mno kupita maelezo! Nilimuaproach na akanikubali..akawa ndo first lover wangu.. hatukupita muda mrefu yapata miezi 4 hv akaanza visa akawa anatafuta sababu mwisho wa siku bila sababu yoyote tukaachana tena kwa ugomvi na akanikashfu na kunipa maneno ya dharau mengi mno ya kutosha!!!!!
iliniuma mno lakini baada ya muda kupita nilitamani saana kuongea naye tu kwa ajili ya kutatua ugomvi japo tumeachana tusijengeane uadui!akakataaa
haikupita miezi 8 nikasikia ana jamaa mwingine pale pale chuo ila amechana nae tena kwa staili ile bila sababu.........
mwaka jana akaolewa.....
tatizo langu ni kwamba huwa namkumbuka sana nakaa nawaza jinsi alivyonifanyia, manake sikutegea wala kufikiria atanifanyia vile wala kunisaliti, nilimuamini mno nikampa moyo wangu 100%.. niliumia mno kupita maelezo manake nilipenda mno...
rafiki zangu, washkaji wakawa wamepata story za kuongea manake wabongo ndo tulivyo...
naomba wanajamvi (MMU), mnisaidie niweze kumsahau na kusahau yote yaliyotokea hata nikikutana nae nichukulie kama sikuwahi kumfahamu b4.. manake huwa tunakutana mara kwa mara...
Too obsessed ,stop stalking her ,how did you know she is married or she did breakup with somebody else.you need a therapist
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom