Nishauri pa kuhamia mkoani MBEYA

Darren2019

JF-Expert Member
Nov 23, 2019
1,112
2,379
Wasalaam, naomba kufahamishwa maeneo mazuri yaliyotulia yenye fursa ya kulima (kidogo) na kufuga katika wilaya zilizo karibu na Mbeya mjini.
 
Acha usotojo kuwa na maamuzi ya kiume,
Sikushauri kwa ushauri wa mkeo kwa sasa hutoona madhara ila badae utajua kwann nimekwambia acha usotojo......

Ukisikia huo ushauri wa mkeo utapotea miaka 20 mbeleni kurudi nyuma giza tupu na utapotea kwa kila kitu na huna pa kuweka jicho.

Nb:
Fanya maamuzi ya kiume kuweka familia sawa nasisitiza mkuu... Kila la heri bwana heri.

Sent using Mchepuko ni dawa kwa mwanamke mkorofi
 
Kwanza kuhamia ukweni ni sahihi?
Kuhamia ukweni ukiwa na maana ya mkoa walipo wakwe zako au nyumba ya wakwezo?

Kama ni mkoa haina tatizo isipokuwa jiandae kwa ugeni wa kila mara na kuletewa shida za hapa na pale zinazohitaji chapaa

Kama ni nyumbani kwa wakwezo, hebu achana na huo mpango

Maisha ya Mbeya yakoje?
Sehemu yoyote ya Tanzania hali ya maisha haipishani sana, muhimu uwe na shughuli ya kukuingizia kipato

Wapi pazuri pa kuhamishia familia na kuanzisha maisha kwa maana ya utulivu, usalama, huduma za kijamii, bei ya ardhi ubora wake hasa kwa kujenga kilimo na ufugaji n.k
Tatizo la Mbeya, sehemu kubwa ya maeneo karibu na mji watu walishanunua kama una mpango wa kujenga, labda ubahatike upate mtu anauza nyumba.

Otherwise, kuna maeneo pembezoni mwa mji kama Isyesye, Itua, Nsalagha, Uyole, Iyunga, Veta unaweza kupata kiwanja na maeneo hayo ni tulivu bado.
La hasha maeneo kama wataka kupanga basi jaribu kupita Block T, Sae, Nanenane, Iyunga na Jacaranda (sina hakika kama Jacaranda kuna nyumba za kupanga)

Au nikomae hukuhuku?

Sasa hata eneo ulilopo haujalitaja, sisi tutajuaje kama wapaswa kukokama huko huko au ushafikia wakati wa kuvunwa
 
Mkuu, wakati unaoa mbona haukuja kutuomba ushauri, embu acha mambo ya kipimbi.
 
Huyu katoka makambako anenda mbeA mpeni ushauri si kejeri hizo
 
Back
Top Bottom