Nisamehe Mwigulu Nchemba

Nisamehe Mwigulu Nchemba

kwa kweli Mwigulu amebadilika sana,kama ataendelea hivi sioni kwa nn tusimfikirie kumpa ofisi kuu 2020,sio mnafiki tena,anawafikiria maskini wa tanzania,mama wajane ,watoto wa wakulima,big up
Ni kweli mwigulu kaanza kubadilika aendelee hivyo hivyo.hao maescrow sio wa kukumbatia.
 
usiishie hapo.afuatilie viescrow vingine.vimejaa kwenye halimashauri zetu.
 
Kwa mtazamo wangu wala mwigulu haitaji kusifiwa,make katika mchango wake hakusema kama zile pesa niza umma au la.Alijikita ktk kudai vat tu.Inamaana watz wengi hatukumwelewa ndg yetu.Mtu kama Mwandonsa alituweka sawa watz kuwa pesa zile zikuwa za umma.Watanzania wenzangu tusipo kuwa makini na hiki chama kitatuingiza katika machafuko makubwa sana.DELETE FUTA KABISA CCM JIMBONI MWAKO.
 
Hakika leo nathubutu kumuomba msamaha ndg Nchemba kwa mawazo yangu hasi juu yake. Nilimdharau na kumzihaki!! Nilimuona kama kada maslahi kumbe sikuwa sahihi!Leo nadiriki kujitokeza hadharani na kukwambia SAMAHANI.

Mchango wako wa leo bungeni ndio ulionibadilisha mtazamo wangu hasi juu yako.Kweli mwanzo hatukukujua vizuri.

Mimi sio mtabiri,lakini kwa uzalendo na msimamo wako usio na chembe ya uoga wa kuwatetea walala hoi wa nchi hii,hakika utafika mbali sana katika medani hii ya kisiasa.

Kila la heri mzalendo.
Uzuri wa watanzania ni wepesi kubadilishwa mawazo. Maagizo yake mengi yalikuwa ya kisiasa hayatekelezeki. Mfanyabiashara kapewa pesa na msamaha wa kodi toka serikali wewe unasema akalipe. Pesa zenyewe zilipelekwa kwenye Akaunti ya kampuni isiyohusika na zimeshatokomezwa kusikojulikana!
 
Yeye ni mbwa mwitu kwa sasa amejivika ngozi ya kondoo ili aje aibuke kugombea urais, akiukosa ataivua ndipo mtakapo jua Mwigulu ni nani!
 
Mwigulu hana jipya watanzania,

jimbo lake vijana hawamtaki tena, kutokana na basi bovu alilopanda(ccm) ,

inasemekana jimboni kwaje vijana wamegombea ngazi zote kwa chama cha cdm, na haijawahi tokea huo vijijini!!! Na wana nguvu vibaya mno!!!!

Ametumia loop hole hii kujaribu kujinusuru tu!!!

Safari hii hawamchekei, labda ahame chama.
 
Kweli huyu Jamaa ni mtu makini sana!
 
Waliojaaliwa akili timamu na mtizamo wa mbali pekee ndio wanaotambua umahiri wa hoja za Mwigulu na uhodari wake wa kusimamia anachokiamini.

Viva Mwigulu,Viva Tanzania
 
Humjui vizuri mwigulu

Mwigulu amejitahidi sana japo simsifii asilimia mia

Taratibu mtakubali tu.

10731193_10152906990397938_3969227425189682687_n.jpg
 
Kwa hiyo unajisifu mwenyewe kwa account yake nyingine eeh? Urais 2015? Tutaona viroja vingi
 
Kwa hiyo unajisifu mwenyewe kwa account yake nyingine eeh? Urais 2015? Tutaona viroja vingi

Maneno kama hayo husemwa na watu waliojaa ushabiki usio na msingi na waliojaa chuki binafsi....
 
Anacheza na saikoloji ya walipa kodi. Anajua wa TZ wanataka kusikia nini sasa. Na yeye anasema hicho hicho. Ndio siasa lakini kiutendaji haiwezekani. Ngoja tusubiri hiyo deadline tuobe kama TRA watakusanya kodi.
 
Tumsamehe kwa yaliyopita, akiendelea hivi basi muelekeo wake ni mzuri.Tumtie moyo kuwa muelekeo ule wa zamani haulipi, bali huu wa sasa utamfikisha mbali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom