Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigullu Nchemba, ujue kuna kesho!

My Son drink water

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
4,932
13,283
Mwigulu Nchemba, Kaka yangu, shikamoo, natumaini u mzima wa Afya wewe na familia yako. Cheo ulichonacho ulipewa na Mungu na siyo mwanadamu kama wewe uonavyo ktk macho ya Damu na nyama (physical world) ktk ulimwengu wa Roho (Spiritual world) ni Mungu ndo alikufanya uwe Waziri.

Mungu alikupa hiyo nafasi ili umshauri vyema Rais ktk masuala ya kiuchumi ili ndugu zako Watanzania wasiteseke na ugumu wa maisha.

Badala yake ni kinyume kwako,unaitumia vibaya nafasi aliyokupa Mungu kuwatesa kiuchumi ndugu zako Watanzania.

Mikononi mwako Tozo ilizaliwa, mikononi mwako tangu juzi hakuna mtu mwenye uwezo wa kununua umeme Bila ya kukatwa Kodi ya jengo Tsh 700Ul

Uliona Transaction za simu hazikwepeki na zinatumiwa na maskini wengi, uliona umeme ni hitaji la muhimu hakuna wa kukwepa ukaona wanyonge wanyongewe hapo, hakika wewe ni mjanja.

Mh Waziri,sidhani kama umewahi kuishi maisha magumu,na Kama uliishi maisha magumu halafu unawa treat hivyo ndugu zako una Roho ngumu sTham

Thamani ya Pesa imeporomoka,kuna inflation kubwa ajabu na ajira hakuna.
Wasiojua mambo wanadhani kila kinachotokea ni Rais, hapana,Rais ni Taasisi yenye matawi yanayotenda kazi Kama wewe.

Nipo Rwanda kuhangaikia kimaisha,rafiki yangu ambaye Baba yake amewahi kuwa Waziri kwenye Serikali ya awamu ya kwanza,yupo anapigwa na visasi vya madhabahu.

Yaani aliniomba Kama naweza nimtumie hata Tsh 10,000 ili anunue umeme kwa sababu Tsh 500 imegoma,kwa sababu inatakiwa Kodi ya jengo.

This is crazy,uwe jengo au usiwe na jengo Kodi inakuhusu.

Mh Waziri, maisha mazuri unayoishi wewe na wenzako usidhani Watanzania wote wako hivyo,80% ya Watanzania wanaishi kwenye umaskini wa kutupwa.

Sasa machozi yao juu ya ugumu wa maisha yatawaacha salama nyie? Yaani kuipata Elfu moja mtaani ni ishu,na idadi kubwa ya watu ni jobless.

Mara Tozo,mara Kodi ya jengo,sipingi ulipaji wa Kodi, lakini Kodi isiyo na impact kwenye maisha ya watu ni mateso tupu.
Nimebahatika kuishi Ulaya kidogo,na Australia, kule Kodi ni kubwa mno lakini inaonekana kwenye maisha ya watu.

Tanzania Kodi ni kubwa halafu haina impact kwenye maisha ya watu, ukienda Hosp Pesa, Elimu Pesa, kila kitu gharama.
Kujenga Barabara, madaraja na shule ni wajibu wa Serikali na siyo maendeleo hayo.

Maendeleo ni kutengeneza ajira nyingi, Thamani ya Pesa, Elimu Bure, matibabu Bure hayo ndo maendeleo. Xmas kuna Watanzania wengi wamekula Dagaa badala ya nyama, yaani kg moja ya nyama ni Tsh Elfu kumi.

Tanzania ni ya pili baada ya Ethiopia Africa kuwa na ng'ombe wengi,iweje Bei ya nyama imekuwa Dhahabu? Mh Waziri, umesimama kutesa Watanzania, umemwasi Mungu, kumbuka kila matendo yana malipo chini ya jua.

Rafiki yangu Baba yake alikuwa Waziri kama wewe, Leo hii hana pa kushika, kasoma ila kazi hapati, kula yake ya taabu,kila jambo linalotokea Duniani, nyuma yake kuna sababu kwanini linatokea.

Machozi ya Watanzania maskini wa kutupwa ambao ni 80% yatakuacha salama kaka yangu Mwigulu Nchemba na wenzako?
 
Naunga mkono hoja. Bei za vitu zimepanda kwa kiwango ambacho hatujawahi kushuhudia.
Tatizo liko wapi?
 
Uzi wote huo ni kwa ajili ya mwiguru tu bora ungefunga na kuomba kesho asubuhi uokote Mihela 🤸🤸
 
Unazijua Esther luxury wewe, hawezi kuwa choka mbaya ,tatizo viongozi walishatupima wakaona hawa jamaa hata tufanyaje hawawezi kufanya lolote, acha tubaki kuwaangalia wala nchi
 
Mwigulu Nchemba, Kaka yangu, shikamoo, natumaini u mzima wa Afya wewe na familia yako. Cheo ulichonacho ulipewa na Mungu na siyo mwanadamu kama wewe uonavyo ktk macho ya Damu na nyama (physical world) ktk ulimwengu wa Roho (Spiritual world) ni Mungu ndo alikufanya uwe Waziri.

Mungu alikupa hiyo nafasi ili umshauri vyema Rais ktk masuala ya kiuchumi ili ndugu zako Watanzania wasiteseke na ugumu wa maisha.

Badala yake ni kinyume kwako,unaitumia vibaya nafasi aliyokupa Mungu kuwatesa kiuchumi ndugu zako Watanzania.

Mikononi mwako Tozo ilizaliwa, mikononi mwako tangu juzi hakuna mtu mwenye uwezo wa kununua umeme Bila ya kukatwa Kodi ya jengo Tsh 700Ul

Uliona Transaction za simu hazikwepeki na zinatumiwa na maskini wengi, uliona umeme ni hitaji la muhimu hakuna wa kukwepa ukaona wanyonge wanyongewe hapo, hakika wewe ni mjanja.

Mh Waziri,sidhani kama umewahi kuishi maisha magumu,na Kama uliishi maisha magumu halafu unawa treat hivyo ndugu zako una Roho ngumu sTham

Thamani ya Pesa imeporomoka,kuna inflation kubwa ajabu na ajira hakuna.
Wasiojua mambo wanadhani kila kinachotokea ni Rais, hapana,Rais ni Taasisi yenye matawi yanayotenda kazi Kama wewe.

Nipo Rwanda kuhangaikia kimaisha,rafiki yangu ambaye Baba yake amewahi kuwa Waziri kwenye Serikali ya awamu ya kwanza,yupo anapigwa na visasi vya madhabahu.

Yaani aliniomba Kama naweza nimtumie hata Tsh 10,000 ili anunue umeme kwa sababu Tsh 500 imegoma,kwa sababu inatakiwa Kodi ya jengo.

This is crazy,uwe jengo au usiwe na jengo Kodi inakuhusu.

Mh Waziri, maisha mazuri unayoishi wewe na wenzako usidhani Watanzania wote wako hivyo,80% ya Watanzania wanaishi kwenye umaskini wa kutupwa.

Sasa machozi yao juu ya ugumu wa maisha yatawaacha salama nyie? Yaani kuipata Elfu moja mtaani ni ishu,na idadi kubwa ya watu ni jobless.

Mara Tozo,mara Kodi ya jengo,sipingi ulipaji wa Kodi, lakini Kodi isiyo na impact kwenye maisha ya watu ni mateso tupu.
Nimebahatika kuishi Ulaya kidogo,na Australia, kule Kodi ni kubwa mno lakini inaonekana kwenye maisha ya watu.

Tanzania Kodi ni kubwa halafu haina impact kwenye maisha ya watu, ukienda Hosp Pesa, Elimu Pesa, kila kitu gharama.
Kujenga Barabara, madaraja na shule ni wajibu wa Serikali na siyo maendeleo hayo.

Maendeleo ni kutengeneza ajira nyingi, Thamani ya Pesa, Elimu Bure, matibabu Bure hayo ndo maendeleo. Xmas kuna Watanzania wengi wamekula Dagaa badala ya nyama, yaani kg moja ya nyama ni Tsh Elfu kumi.

Tanzania ni ya pili baada ya Ethiopia Africa kuwa na ng'ombe wengi,iweje Bei ya nyama imekuwa Dhahabu? Mh Waziri, umesimama kutesa Watanzania, umemwasi Mungu, kumbuka kila matendo yana malipo chini ya jua.

Rafiki yangu Baba yake alikuwa Waziri kama wewe, Leo hii hana pa kushika, kasoma ila kazi hapati, kula yake ya taabu,kila jambo linalotokea Duniani, nyuma yake kuna sababu kwanini linatokea.

Machozi ya Watanzania maskini wa kutupwa ambao ni 80% yatakuacha salama kaka yangu Mwigulu Nchemba na wenzako?
Tumekosa lile bunge lenye vuta ni kuvute
 
Back
Top Bottom