Nisamehe Mwigulu Nchemba

Nisamehe Mwigulu Nchemba

Mwigula alipima upepo akaona pa kusimamia na kuosha nyota
 
Mm sikubaliani na maamuzi ya Mh. Mwigulu,eti anasema waliogawana pesa za Escrow walipe kodi,kwani wamefanya biashara gani au wamefanya kazi gani? Hawa ni wahalifu yaani ni wezi wa mali ya umma kinachotakiwa ni kufilisiwa na kushtakiwa.
 
mi naomba mnisamehe tu kuhusu huyu mwigulu mnamkumbuka sita na mwakyembe tulivyowasifia walipokua wanapambana na serikali ya kikwete tuliwaona mashujaa wa mafukara lakini mwisho wameliuza taifa hili kwa laki 3 kwa siku pale dodoma siamini ccm yoyote
 
Hakika leo nathubutu kumuomba msamaha ndg Nchemba kwa mawazo yangu hasi juu yake. Nilimdharau na kumzihaki!! Nilimuona kama kada maslahi kumbe sikuwa sahihi.......!Leo nadiriki kujitokeza hadharani na kukwambia SAMAHANI.
Mchango wako wa leo bungeni ndio ulionibadilisha mtazamo wangu hasi juu yako......Kweli mwanzo hatukukujua vizuri.
Mimi sio mtabiri,lakini kwa uzalendo na msimamo wako usio na chembe ya uoga wa kuwatetea walala hoi wa nchi hii....hakika utafika mbali sana katika medani hii ya kisiasa.
Kila la heri mzalendo.

Umefanya vizuri sana kukiri makosa yako, bigup sana
 
Ni mapema sana! angalia hadiwe anacheza na akili zako!
 
Hakika leo nathubutu kumuomba msamaha ndg Nchemba kwa mawazo yangu hasi juu yake. Nilimdharau na kumzihaki!! Nilimuona kama kada maslahi kumbe sikuwa sahihi.......!Leo nadiriki kujitokeza hadharani na kukwambia SAMAHANI.
Mchango wako wa leo bungeni ndio ulionibadilisha mtazamo wangu hasi juu yako......Kweli mwanzo hatukukujua vizuri.
Mimi sio mtabiri,lakini kwa uzalendo na msimamo wako usio na chembe ya uoga wa kuwatetea walala hoi wa nchi hii....hakika utafika mbali sana katika medani hii ya kisiasa.
Kila la heri mzalendo.

Toka baraza la katiba hadi bunge la escrow huyu jamaa namkubali tatizo anaharibiwa na chama, cjui kwa nn yupo pale
 
Mwigulu amebadilika sana....nampongeza sana..ameacha uropokaji na anaongea kama kiongpzi
 
Mimi binafsi sijaona kwa nini Mwigulu anasifiwa kwenye hili suala kwa sababu zifuatazo:

1) kudai eti wote waliochuwa pesa walipe kodi ya income tax sio Sawa maana huwezi kutoza kodi kwenye pesa haramu.

2) kusema eti tra wamekwisha aanza kufuatilia kodi Yao pia nadhani hili Lina mashaka lakini pia Lina halalisha kuwa fedha za umma zilikuwepo! Mashaka yangu nipale kodi inapodaiwa baada ya tukio! Vat ilipaswa kulipwa kabla na sio baada
 
Bado ni mapema sana kumwamini huyu mwengulu,bado namuona kama ni chui aliyevaa ngozi ya kondoo kwa vitendo vya kishetani alivyoshiriki kupanga mikakati ya kuua raia na kuwasingizia CHADEMA,cmwamini hata kidogo.
 
Mitanzania ndio maana inaibiwa......kudanganywa kidogo tu mshaanza kumsifia huyu gaidi....hamjui wanasiasa nyie hasa wa CCM
 
Comrade Othomorine; Ok ni uungwana kukubali kosa na kuomba msamaha; lakini mtazamo wako dhidi ya Mwigulu Nchemba ulikuwa SAHIHI 100%; kwa sababu haiba ya mtu inawakilishwa na maneno na matendo yake! Mwigulu yule alikuwa wakala wa shetani!! nathubutu kukuhakikishia kwamba hukuwa peke yako kwenye mtazamo hasi dhidi ya the Then Mwigulu kada wa CCM; tulikuwa wengi sana; hata hivyo mmoja wa waasisi wa mapinduzi ya Zanzibar; hayati Shk Thabiti kombo alituasa kuwa na "Akiba ya maneno" nakubali Mwigulu amezisoma alama za nyakati na amebadilika lakini nmasita kumuomba msamaha sasa hivi; it is too early; wahenga walisema "Maji hayasahau asili; hata uyachemshe kiasi gani; shurti yatarudi yatakuwa baridi tu!!!!; tuwe na akiba ya maneno tusije kuwa disappointed; tusisahau kwamba kubadilika kwa Mwigulu tunakokusifia sisi; tayari ameshaanza kupata "maadui" ndani ya Chama Cha Majambazi; wanamuona kama Yuda Iskariot; ameanza kuwasaliti wakati walikuwa wanamuona kama jembe lao mahiri nla kuusakama upinzani; na leo hii sina hakika kama umemsikia mbunge wa sikonge Saidi Mbumba; kwenye mjadala wa escrow; ametamka bayana kwamba alishaanza kumuona Mwigulu kama amepotoka kutokana na msimamo wa Mwigulu kuhusu Bunge la katiba baada ya UKAWA kutoka nje.

Time will tell if mwigulu has indeed changed for the better and forever; tuendelee kumfuatilia; none the less hata mimi leo nimempa 110%. #bringbackourmoney

mkuu hongera umenena kwa hekma ya hali ya juu. Bravoo.!
 
hata akibadilika na kuwa mwema zaidi ya YESU mim abadan sitomwamin hadi atoke ccm na awaombe radhi wale aliowaulia ndugu zao!
 
mi naomba mnisamehe tu kuhusu huyu mwigulu mnamkumbuka sita na mwakyembe tulivyowasifia walipokua wanapambana na serikali ya kikwete tuliwaona mashujaa wa mafukara lakini mwisho wameliuza taifa hili kwa laki 3 kwa siku pale dodoma siamini ccm yoyote

Nikweli unachosema hata mm nashindwa kuamini CDM yeyote.ila hata CCM siwaamini wote. kwa mwigulu mia mia.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom