Nisamehe Mpenzi

Nisamehe Mpenzi

Madame S

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2015
Posts
17,190
Reaction score
34,526
NISAMEHE MPENZI
Mtunzi:Juma Hiza
0712988278

Hali ya hewa ilikuwa shwari katika jiji la Daresalaam. Ndani ya chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM kilichokuwepo maeneo ya Posta mtaa wa Shaaban Robert, msichana mrembo aliyejulikana kwa jina la Evelyne alionekana akitoka darasani huku akiwa anakimbia, machozi yalikuwa yakimdondoka kwa wakati huo.
“Evelyne! Evelyne! Evelyne,” ilisikika sauti ya msichana mwingine ambaye alikuwa akimfuata nyuma Evelyne baada ya kutoka darasani.
Evelyne aliongoza moja kwa moja mpaka kwenye kimbweta, alipofika hapo aliketi na kuanza kulia huku akiwa amejiinamia.
“Evelyne kuna nini mbona sikuelewi?” aliuliza msichana huyo aliyekuwa akimfuata nyuma Evelyne, alionekana kutoelewa chochote kilichokuwa kikiendelea kwa wakati huo.
“Hapana Happy siwezi kuendelea kuwa eneo hili acha niondoke zangu,” alisema Evelyne kwa sauti iliyoandamana na kilio cha kwikwi.
“Unaondoka unaenda wapi sasa na wakati darasani kuna kipindi?” aliuliza Happy huku akimtazama Evelyne ambaye aliendelea kulia muda wote huo.
“Narudi zangu nyumbani,” alijibu Evelyne.
“Unajua sikuelewi Evelyne,” alisema Happy lakini kabla ya Evelyne kumjibu lolote aliinuka na kuondoka eneo hilo la chuo, Happy alibaki akimtazama Evelyne huku asijue ni nini kilichokuwa kikiendelea.
Evelyne na Happy walikuwa ni marafiki wakubwa sana katika chuo hicho, walikuwa wakisaidiana mambo mengi sana, walishiriki kusaidiana katika masomo na hata katika mipango yao ya kimaisha pia walishirikishana. Happy alikuwa akimfahamu vyema rafiki yake huyo tangu walipoanza kusoma katika chuo hicho mpaka kufikia mwaka wao wa mwisho wa Degree ambao ndiyo walikuwa wameubakiza. Walikuwa wakisomea Uhasibu.
Kila kitu kilichokuwa kikiendelea katika maisha ya Evelyne, Happy alikifahamu na kila kitu kilichokuwa kikiendelea katika maisha ya Happy, Evelyne naye alikifahamu, kwa kifupi walikuwa ni marafiki waliyoshibana. Walikuwa wakiishi pamoja katika chumba kimoja walichokuwa wamepanga maeneo ya Kigamboni.
Wakati Happy akiwa bado amesimama eneo lile ghafla! aliisikia sauti ya kiume ikimuita nyuma yake, haraka aligeuka na kukutana na mtu aliyekuwa akimuita. Alikuwa ni Richard.
“Niambie Shem.”
“Poa tu! vipi mbona Evelyne ametoka darasani kuna nini?”
“Sijui.”
“Yuko wapi?”
“Ameondoka, ameniambia anarudi nyumbani hawezi kuendelea kuwa eneo hili.”
“Mbona unanichanganya?”
“Richard kwani kuna kitu gani kimetokea kati yenu?”
“Hakuna kitu.”
“Mbona sasa Evelyne amebadilika ghafla! baada ya kukuona.”
“Mimi mwenyewe sielewi chochote.”
“Una uhakika?”
“Ndiyo Happy inamaana huniamini?”
“Nakuamini sana,” alijibu Happy.
Richard alikuwa ni mvulana aliyekuwa akitokea katika familia ya kitajiri sana, alikuwa ni mtanashati, mwenye mwili uliyojengeka vyema kimazoezi uliyosindikizwa na muonekano nadhifu ambao ulimpagawisha kila msichana aliyemuona katika chuo hicho.
“There’s something I want to tell you,” (Kuna kitu nataka kukuambia Richard,) ilikuwa ni sauti ya msichana mmoja aliyejulikana kwa jina la Monalisa ambaye alimuita Richard chemba na kuzungumza naye.
“What’s that Monalisa?” (Kitu gani hicho Monalisa?) aliuliza Richard huku akimtazama Monalisa ambaye alikuwa akijing’atang’ata kucha za vidole vyake kwa wakati huo.
“But I feel like I’m going to make a mistake,” (Lakini nahisi kama nitakukosea,) alisema Monalisa huku akijishtukia, macho yake alikuwa ameyalegeza.
“No, tell me do not be afraid,” (Hapana niambie usiogope,) alisema Richard huku akiwa makini kumsikiliza. Kwa muonekano ambao aliuona kwa Monalisa akilini mwake alikwisha fahamu ni kitu gani ambacho msichana huyo alitaka kumueleza lakini hakutaka kuwa na papara ya kukurupukia mambo, alihitaji kumpa muda msichana huyo wa kujieleza ili asahili kile alichokuwa kikifikiria.
“Richard to say the truth I love you so much and I’m ready to do anything for you, please say yes do not let my kid,” (Richard kusema kweli mimi nakupenda sana na nipo tayari kufanya lolote kwa ajili yako, tafadhali sema ndiyo usinikatalie ombi langu,) alisema Monalisa huku akianza kumsogelea Richard kwa lengo la kumbusu.
“No, don’t do that,” (Hapana usifanye hivyo,) alisema Richard huku akimzuia Monalisa, kitendo hicho kikamkwaza Monalisa, akahisi kukataliwa, alijisikia vibaya mno.
Monalisa hakuwa msichana wa kwanza na wa mwisho kumsumbua Richard, kila msichana alitamani kuwa naye kimapenzi na huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kupokea usumbufu kila kukicha lakini hakukuwa na msichana aliyewahi kuipata nafasi hiyo kwa Richard.
Moyo wa Richard ulizama kimapenzi kwa msichana mmoja ambaye ndiye alikuwa ameishikilia nafasi hiyo ya kimapenzi na kuwazibia wasichana wengine wote waliyokuwa wakiitamani kuipata. Hakukuwa na mtu ambaye alitaka kuamini kuwa Evelyne msichana aliyeonekana kuwa na uzuri wa kawaida ndiye ambaye alifanikiwa kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Richard, wengi wao waliamini kuwa kwa muonekano wa kuvutia aliyokuwa nao Richard pamoja na kutokea katika familia ya kitajiri basi ni lazima angekuwa na msichana ambaye alitikisa chuo kizima kwa uzuri wake au aliyetokea katika familia ya kitajiri lakini haikuwa hivyo.
“Huyu kinyago ndiyo anatuzibia riziki yetu,” alisema Monalisa huku akiwaambia wasichana wenzake watatu walipokuwa hostel wameketi kitandani, wote walikuwa wakimtamani Richard.
“Nani ndiyo huyu Evelyne?” aliuliza mmoja wao.
“Ndiyo hivi ana uzuri gani yule msichana mpaka wa kutembea na Richard kama sio uchawi,” alisema Monalisa huku akiwa ameubetua mdomo wake.
“Atakuwa mwanga yule sio bure,” alisema msichana mwingine maneno yaliyowafanya wote wakacheka kwa sauti kubwa huku wakigongeana.
Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kuibuka kwa chuki kati ya wasichana hao na Evelyne, walitokea kumchukia sana pale chuoni baada ya kugundua kuwa alikuwa akijihusisha na mahusiano ya kimapenzi na Richard, hilo lilizidi kumuumiza kila msichana ambaye aliwahi kumtamkia neno NAKUPENDA Richard au kuibuka kwa chembechembe zozote za kimapenzi kwa mvulana huyo aliyetokea kuipagawisha mioyo ya wasichana wengi pale chuoni.

Je, ni nini kitaendelea katika maisha ya wasichana hao?
Na nini kimemkuta Evelyne?
Vipi kuhusu Richard?
 
NISAMEHE MPENZI-02
Mtunzi:Juma Hiza
0712988278

ILIPOISHIA.....

Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kuibuka kwa chuki kati ya wasichana hao na Evelyne, walitokea kumchukia sana pale chuoni baada ya kugundua kuwa alikuwa akijihusisha na mahusiano ya kimapenzi na Richard, hilo lilizidi kumuumiza kila msichana ambaye aliwahi kumtamkia neno NAKUPENDA Richard au kuibuka kwa chembechembe zozote za kimapenzi kwa mvulana huyo aliyetokea kuipagawisha mioyo ya wasichana wengi pale chuoni.

SONGA NAYO.....

Monalisa ndiye msichana ambaye alionekana kumpenda zaidi Richard kuliko wasichana wengine pale chuoni, licha ya Richard kumkatalia ombi lake la kuwa wapenzi lakini bado hakutaka kukubali hilo, aliamini kwa vyovyote iwezekanavyo ni lazima mvulana huyo angefanikiwa kummiliki.
Kuna kipindi kichwani mwake yalimjia mawazo ya jinsi ambavyo alivyofanikiwa kumpata Richard kisha wakawa wanayafurahia mapenzi yao katika ufukwe wa bahari ya Hindi, alizidi kulifurahia hilo katika moyo wake maradufu na hata pale mawazo hayo yalipomtoka kichwani alionekana kukasirika mno, hakutaka kuamini kama kweli alikuwa akiwaza kwa wakati huo.
Moyo wa mapenzi ukazidi kumuendesha vilivyo, alikuwa amezama katika dimbwi la mapenzi ya Richard mvulana ambaye na yeye moyo wake ulikuwa umekufa umeoza katika mapenzi ya msichana mwingine chuoni pale.
“Kwanini Richard anashindwa kunikubalia hivi inamaana sina uzuri wa kumvutia au?” aliuliza Monalisa huku akiwatizama wale mashoga zake watatu walipokuwa hostel.
“Sio kwamba humvutii isipokuwa Richard ameshatekwa na Evelyne,” alijibu msichana mmoja huku akionekana kuwa bize na simu yake.
“Sitaki kumsikia huyo mpumbavu tena nitamkomesha mwanaharamu yule,” alisema Monalisa huku akionekana kuchukia mno baada ya kulisikia jina la Evelyne likitajwa na rafiki yake huyo aliyejukana kwa jina la Penina.
“Shoga yangu mimi nimeshachoka kumfuatilia huyo Richard kwani hakuna wavulana wengine hapa chuo kwani yeye nani?” aliuliza Mary.
“Jamani Richard ni Handsome mimi mwenyewe bado sijaona mvulana anayemfikia kwa uzuri hapa chuoni,” alisema Adela msichana aliyeikamilisha hesabu yao pale ndani, walikuwa wanne.
“Lakini lazima nitampata tu,” alisema Monalisa huku akijiapiza kumpata kwa vyovyote iwezekanavyo.
“Utatumia njia gani?” aliuliza Mary huku akimtazama Monalisa.
“Nitajua tu lakini lazima nimpate, nitahakikisha Richard anakuwa mali yangu,” alisema Monalisa.
Hakukuwa kuna kitu kingine alichokuwa akikihitaji Monalisa zaidi ya kuona anafanikiwa kummiliki Richard mvulana ambaye alitokea kuuteka moyo wake. Kila kitu alichokuwa akikifanya, aliamua kukifanya huku malengo yake makubwa yakiwa ni siku moja atafanikiwa kummiliki Richard.
Miongoni mwa wasichana ambao waliwahi kumtamani Richard kimapenzi kutokana na muonekano wake kuwa mzuri alikuwa ni Adela, Mary pamoja na Penina. Wasichana hawa wote mioyo yao iliwahi kufa na kuoza kwa Richard lakini kutokana na msimamo aliyokuwa nao mvulana huyo hawakuwepa kuambulia hata busu bandia.
Kila mmoja alishaanza kukata tamaa ya kufanikiwa kulipata penzi la mvulana huyo, walitumia kila aina ya njia walizoziona zinafaa kumteka Richard kimapenzi lakini hakukuwa na njia hata moja iliyomkamata mtegoni.
Hilo lilizidi kuwasononesha mioyo yao mno, ilifikia kipindi hata wakati wa kula chakula kila mmoja alishindwa kula kwa nafasi yake, moyo wake ulikuwa ukiumia kwa sababu ya kulikosa penzi la Richard.
“Sitaki kuamini na sitaamini kama nimelikosa penzi la Richard,” alisema Monalisa.
“Hutaki kuamini nini sasa wakati mwenzako ameshapendwa,” alisema Penina huku akimcheka Monalisa wakati huo walikuwa darasani, tukio hilo lilizidi kumuumiza mno moyo wa Monalisa, hakutaka kuamini licha ya kuupoteza muda wake wote katika kumfukuzia Richard lakini mwisho wa siku aliambulia patupu.
“Nadhani kuna kitu natakiwa kufanya,” alisema Monalisa.
“Kitu gani?” aliuliza Penina.
“Ni mapema mno kukuambia.”
“Niambie usinifiche.”
“Usijali muda ukifika nitakuambia,” alisema Monalisa huku akionekana kutawaliwa na mawazo.
Kichwani mwake lilimjia wazo, lilikuwa ni wazo la kufanya kitu maalumu kwa ajili ya Richard ili afanikiwe kumpata kimapenzi na ni katika wazo hilo hakutaka kuywaza au kuyapima maumivu ambayo angeweza kumpa Evelyne msichana ambaye tayari alikuwa akijihusisha kimapenzi na Richard.
****
Moyo wake bado uliendelea kumuuma mno, kila alipokuwa akimuona Richard darasani alijihisi kuwa na sababu milioni mia moja za kuwa naye kimapenzi.
Kuna kipindi alipokuwa akimtazama Richard pamoja na muonekano wake mzuri alijaribu kumlinganisha na Evelyne msichana ambaye alimuona kuwa na uzuri wa kawaida sana, hakustahili kabisa kuwa na Richard kimapenzi. Lilipokuja suala la uzuri kati yake na Evelyne alipokuwa akijiremba kwenye kioo alikiri fika alimzidi msichana huyo kwa uzuri wala hakukuwa na upinzani katika hilo.
“Sasa kwanini Richard asinipende mimi?” alijiuliza swali ambalo lilizidi kumfanya ajione kuwa na mapungufu mengi katika mwili wake, kuna muda pia alijiona kuwa miongoni mwa wajinga na wapumbavu wa kumkosa Richard.
“ Lazima nifanye kitu kwa ajili yako Richard, sitokubali na siwezi kamwe kukubali kuona ukiendelea kuutesa moyo wangu kila siku, nakupenda sana na ninahitaji ulifahamu hilo,” alisema Monalisa siku moja usiku alipokuwa amelala hostel, usiku wa siku hiyo ulikuwa mrefu sana kwake na aliutumia katika kumfikiria Richard tu, kichwani mwake jina la Richard lilitawala sehemu kubwa sana.

Je, ni nini kitaendelea?
 
NISAMEHE MPENZI-03
Mtunzi:Juma Hiza
0712988278

ILIPOISHIA.....

“ Lazima nifanye kitu kwa ajili yako Richard, sitokubali na siwezi kamwe kukubali kuona ukiendelea kuutesa moyo wangu kila siku, nakupenda sana na ninahitaji ulifahamu hilo,” alisema Monalisa siku moja usiku alipokuwa amelala hostel, usiku wa siku hiyo ulikuwa mrefu sana kwake na aliutumia katika kumfikiria Richard tu, kichwani mwake jina la Richard lilitawala sehemu kubwa sana.

SONGA NAYO.....

Alichokuwa amepanga kukifanya Monalisa ni kutengeneza mazingira ambayo yangeweza kumuonyesha kuwa yeye na Richard kuwa ni wapenzi, alilifikiria wazo hilo huku akiamini kama kweli angeweza kufanikiwa kuyatengeneza mazingira hayo basi ni lazima Evelyne angeingiwa na wivu kiasi cha kuumia sana moyoni mwake, hilo ndilo alilokuwa anahitaji kuliona likitokea kwa msichana huyo, hakumpenda wala hakutaka kumuona akiendelea kuwa karibu na Richard mvulana ambaye tayari alikuwa ameshauteka moyo wake wa kimapenzi.
“You must be mine,” (Lazima utakuwa wangu,) alijisemea Monalisa huku akitabasamu, ulikuwa ni wakati ambao wazo hilo lilimjia kichwani mwake.
Maisha ya chuo yaliendelea huku Monalisa kila siku akizidi kuumia, kuna kipindi alitamani kutengeneza mazingira ya kumfanya Evelyne afukuzwe chuo na yote hayo aliwaza ilimradi afanikiwe kumpata Richard.
Siku moja Monalisa alijaribu kutafuta nafasi ya kuzungumza na Richard mpaka akafanikiwa kuipata.
“Kwanini hutaki kuwa na mimi?”
“Hapana siwezi.”
“Kwanini?”
“Nipo katika mapenzi tayari.”
“Richard mbona unapenda kunifanyia hivyo, kwanini unautesa moyo wangu kiasi hiki?”
“Sio kama nakutesa ila tatizo tayari moyo wangu upo kwa msichana mwingine.”
“Hunipendi?” aliuliza Monalisa.
Lilikuwa ni swali gumu mno lililomfanya Richard ashindwe kutoa jibu la haraka, alibaki akimtazama Monalisa huku asijue ni nini alitakiwa kumjibu kwa wakati huo. Macho yake yalipotazamana na ya Monalisa kuna kitu alikigundua kilikuwa kikiendelea kwa wakati huo, aliyashuhudia machozi yakianza kumbubujika Monalisa mashavuni mwake, hakutaka kuamini kile alichokuwa akikishuhudia, kitendo cha kumuona msichana mrembo kama yule akiyadondosha machozi mbele yake hakika kilimuumiza mno, kuna muda alianza kujiona kuwa na makosa makubwa mno kwa kuendelea kuutesa moyo wa msichana ambaye alionekana kumpenda kuliko kitu chochote kile.
Alichoamua kukifanya alikitoa kitambaa katika mfuko wa suruali yake kisha akamfuta machozi Monalisa, kitendo hicho kilimfanya Monalisa ashangae, hakutaka kuamini kama machozi yake yalimgusa Richard kiasi kwamba akafikia hatua ya kumfuta.
“Richard,” alimuita.
“Niambie,” alisema Richard.
“Unaweza kweli kuendelea kuishuhudia nafsi ambayo inateseka, inasononeka, inaumia kila siku kwa sababu yako?” aliuliza Monalisa.
“Hapana siwezi,” alijibu Richard.
“Sasa kwanini hutaki kunifikiria hata mara moja, nimekusumbua sana, nimetumia kila njia ilimradi niwe na wewe lakini imeshindikana basi naomba unisaidie kitu kimoja tu kama hutojali,” alisema Monalisa kwa sauti ya utulivu.
“Kitu gani hicho?” aliuliza Richard huku akimtazama Monalisa.
“Nalihitaji penzi lako, naomba nitumie kuwa na wewe ndani ya usiku mmoja nahisi nitakuwa nimeuridhisha moyo wangu maana kila siku unaishi kwa kuteseka kwa sababu yako,” alisema Monalisa.
Maneno ya Monalisa yalimuweka Richard kuwa katika wakati mgumu sana, hakutaka kuamini kile alichokuwa akikisikia kutoka kwa msichana huyo ambaye alikuwa na kila sifa za kumteka mwanaume rijali, bado hakutaka kuamini kile alichokuwa amekisikia kutoka kwa msichana huyo, ilibidi amuulize ni nini alichokuwa amefikiria lakini kabla hajafanya hivyo ghafla! Monalisa aliweza kumzuia asizungumze lolote kwa kumuwekea kidole katika lips zake.
“Don’t say no please say yes,” (Usiseme hapana tafadhali sema ndiyo,) alitamka maneno haya Monalisa wakati ambao alikuwa amemuwekea kidole kwenye lips Richard.
Richard alishindwa la kufanya, alikosa la kuamua kwa wakati huo. Ni kweli Monalisa alikuwa na sifa zote za kumchanganya mwanaume rijali na kupitia udhaifu huo aliweza kumchanganya Richard mwisho akajikuta akili yake ikianza kumfikiria.
“Ok right but let’s make it a secret between us,” (Sawa ila naomba tufanye iwe ni siri kati yetu,) alisema Richard huku akionekana kukosa uvumilivu kabisa.
“Don’t worry about it I will keep that secret,” (Usijali kuhusu hilo nitaitunza siri hiyo,) alisema Monalisa huku akimtoa hofu Richard.
“Don’t go against our agreement,” (Usiende kinyume na makubaliano yetu,) alisema Richard.
“Don’t worry,” (Usijali,) alisema Monalisa huku akitabasamu.
Monalisa hakutaka kuamini kama kweli alifanikiwa kwa asilimia zote mpango wake, aliamini huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kumpa maumivu Evelyne, maumivu ambayo alikuwa akiyapitia kila siku.
Siku hiyo aliporudi hostel hakukuwa na kazi nyingine aliyoifanya zaidi ya kuwasiliana na Richard, alisahau mpaka kusoma kwasababu ya Richard mvulana aliyeutesa sana moyo wake lakini mwisho wa siku alifanikiwa kuwa naye.
“Mbona unafuraha sana leo?” aliuliza Penina wakati huo alikuwa akisoma kitabu.
“We acha tu shosti yani huwezi kuamini,” alisema Monalisa huku furaha ikionekana kumtawala.
“Kuhusu nini?” aliuliza Penina.
“Kuhusu Richard,” alijibu Monalisa.
“Amefanyaje?”
“Amekubali kuwa na mimi.”
“Unasemaje?”
“Ndiyo amekubali kuwa na mimi,” alijibu Monalisa jibu lililowashangaza wasichana wote pale ndani, kila mmoja hakutaka kuamini kama kweli Monalisa aliweza kukubaliwa na mvulana huyo.
****
Yalikuwa ni majira ya saa tatu za usiku, Richard alikuwa nyumbani kwao maeneo ya Mikocheni B, wakati huo alikuwa chumbani kwake amejilaza kitandani. Akili yake bado iliendelea kumfikiria Monalisa, hakujua ni kwanini msichana huyo alianza kumuingia kwa kasi katika kichwa chake, kuna kipindi alianza kujilaumu kwa kumkubalia ombi lake lakini alipotaka kuchukua simu yake na kutaka kumuandikia ujumbe wenye lengo la kughairi uamuzi huo alishindwa, alijikuta vidole vyake vikiwa vizito kuandika ujumbe wa aina hiyo mwisho akajikuta akimtumia ujumbe wa salamu na huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kuchat na msichana huyo. Alisahau kumjulia hata hali Evelyne msichana ambaye alikuwa katika mahusiano naye, alichokuwa amekiona ni cha umuhimu kwa wakati huo ni kuwasiliana na Monalisa ili aweze kuzikidhi haja za moyo wake, alipanga kushiriki kufanya mapenzi naye halafu huo ndiyo uwe mwisho wa uhusiano wao, hakupanga kumuumiza Evelyne na ndiyo sababu aliomba iwe siri ili msichana wake huyo asiweze kugundua lolote.
 
NISAMEHE MPENZI-04
Mtunzi:Juma Hiza
0712988278

ILIPOISHIA.....

Alisahau kumjulia hata hali Evelyne msichana ambaye alikuwa katika mahusiano naye, alichokuwa amekiona ni cha umuhimu kwa wakati huo ni kuwasiliana na Monalisa ili aweze kuzikidhi haja za moyo wake, alipanga kushiriki kufanya mapenzi naye halafu huo ndiyo uwe mwisho wa uhusiano wao, hakupanga kumuumiza Evelyne na ndiyo sababu aliomba iwe siri ili msichana wake huyo asiweze kugundua lolote.

SONGA NAYO.....

Kila kitu kilichokuwa kikiendelea katika moyo wa Richard aliamini ilikuwa ni siri nzito mno na hakukuwa na mtu mwingine ambaye alikuwa akikifahamu zaidi yake na Monalisa.
Wakati alipokuwa akiendelea kuwasiliana na msichana huyo ndivyo ambavyo Monalisa na yeye alizidi kuwatambia wasichana wenzake mule hostel jinsi ambavyo alikuwa msichana shupavu ambaye hakukubali kushindwa kirahisi kwa kumkosa Richard.
Hilo lilizidi kuwaumiza wasichana wenzake mno, walianza kuingiwa na wivu baada ya kusikia kuwa Richard na Monalisa walikuwa ni wapenzi kwa wakati ule, kuna kipindi hawakutaka kukubali kabisa lakini huo ulibaki kuwa ni ukweli. Richard na Monalisa walikuwa katika mapenzi.
“Unafikiri nitakubali kirahisi kuachana naye, nitahakikisha anabaki kuwa wangu tu,” alisema Monalisa huku akiwaambia Penina, Mary na Adela, walionekana kuingiwa na wivu mno, hawakutaka kuamini kabisa.
“Sijui Evelyne atakuwa katika hali gani akisikia kuwa wewe na Richard ni wapenzi?” aliuliza Mary swali la kinafki ambalo jibu lake lilikuwa wazi kabisa, swali hilo likawafanya wote watokwe na kicheko halafu wakagongeana kama ilivyokuwa kawaida yao.
“Evelyne ndiyo mdudu gani?” aliuliza Monalisa huku akiendelea kucheka.
Hakutaka kuona msichana huyo akiendelea kuyafurahia mapenzi na Richard, kitu pekee alichokuwa amepanga kukifanya ni kuhakikisha anafanikiwa kumpokonya Richard mikononi mwake na kisha anakuwa mali yake peke yake tu.
Hakuacha kuendelea kuwasiliana na Richard, walikuwa wakifanya mawasiliano kila siku huku moyoni akizidi kujiapiza kumteka mvulana huyo kimapenzi.
“Nahitaji kukuona Richard.”
“Lini?”
“Leo.”
“Usiku huu?”
“Ndiyo, Kwani kuna tatizo gani mpenzi?”
“Hapana, hakuna tatizo.”
“Sasa kwanini hutaki?”
“Sio sitaki ila si upo hostel na kesho tunakipindi asubuhi?”
“Ndiyo najua hilo.”
“Sasa huoni hilo ni tatizo?”
“Richard mimi siwezi kusoma ukweli bila kuonana na wewe usiku wa leo, kama ni kipindi kuingia tutaingia tu kwanza kipindi chenyewe hakina umuhimu zaidi yako, tafadhali naomba kukuona japo sekunde moja, nitauridhisha moyo wangu.”
“Sawa nakuja kukufuata muda huu hostel ila tafadhali naomba kila kitu kinachoendelea kibaki kuwa ni siri kati yetu.”
“Nilikuahidi na ninarudia kukuahidi, siwezi kuitoa siri hii, shida yangu kubwa ni kuwa na wewe tu basi.”
“Sawa nakuja.”
Yalikuwa ni mazungumzo kati ya Monalisa na Richard waliyokuwa wakizungumza kwenye simu majira ya jioni, baada ya kumaliza kuzungumza Richard alijiandaa, alipomaliza aliwaaga wazazi wake kuwa anakwenda chuoni kwenye kipindi, wazazi wake walimkubalia kisha akaondoka kwa usafiri binafsi kama ilivyokuwa kawaida yake, siku hiyo aliamua kutembelea gari aina ya Toyota prado new model lenye thamani ya shilingi milioni 65.
Safari yake iliishia nje ya chuo cha IFM ambapo ndipo zilipokuwa hostel za chuo hiko, aliposimamisha gari aliamua kumtumia ujumbe mfupi Monalisa wa kumtaarifu kuwa tayari alikuwa eneo lile la chuo na kwa wakati huo alikuwa akimsubiria nje.
Haikuchukua dakika nyingi Monalisa aliweza kutoka nje ya chuo hiko na kuanza kuyaangaza macho yake huku na kule, Richard aliamua kupiga honi baada ya kumuona Monalisa akiwa katika hali hiyo, tabasamu mwanana lilichanua katika uso wa Monalisa ambaye alikuwa amevalia mavazi yaliyompendezesha kupita kawaida, baada ya kumuona Richard akiwa ndani ya gari alilifuata gari lile, alipolifikia Richard alimpa ishara ya kukaa kiti cha mbele, akafungua mlango wa gari hilo na kuingia.
“Umependeza sana,”alisema Richard huku akimtazama Monalisa.
“Asante Mpenzi na uzuri nao unachangia,” alisema Monalisa maneno yaliyowafanya wote wakatokwa na kicheko.
“Kwahiyo tunaenda wapi?” aliuliza Richard.
“Popote pale mpenzi utakapopapenda wewe,” alijibu Monalisa.
“Sehemu gani itakuwa na utulivu,” alisema Richard huku akionekana kutafakari jambo.
“Pale Serena vipi hapafai kwani?” aliuliza Monalisa swali lililomtoa Richard katika ile hali ya kutafakari.
“Yeah! pako vizuri sana, twende huko,” alijibu Richard kisha akawasha gari na kuondoka eneo hilo.
Walifika katika hoteli hiyo ya kifahari ya Serena kisha wakakodisha chumba, Monalisa bado alikuwa haamini kama kweli siku hiyo alikuwa anafanikiwa kulala na Richard kitanda kimoja, alionekana kuwa mwenye furaha mno.
Walipoingia ndani ya chumba cha hoteli hiyo Richard bado aliendelea kuisisitiza siri ambayo ilitakiwa kuendelea kubaki kati yao, moyoni mwake alimpenda sana Evelyne na hakupanga kumsaliti wala kumpa maumivu yoyote ya kimapenzi, aliamini baada ya kumaliza kufanya mapenzi na Monalisa basi huo ndiyo ulikuwa mwanzo na mwisho wa penzi hilo la dharura.
Waliagiza chakula na baada ya kuletewa na muhudumu wa hoteli hiyo walianza kula taratibu huku wakitazamana kwa macho ya kuibiana.
Baada ya kumaliza kula chakula hakukuwa na tukio lingine ambalo lilitakiwa kuendelea kati yao zaidi ya kuanza kushikanashikana huku midomo yao ikiwa imekutana na kuanza kubadilishana mate, walitumia muda kama wa dakika kumi na tano katika kuchezeana miili yao na baada ya hapo kitendo kilichofuata waliamua kuvunja amri ya sita.
****
Evelyne aliendelea kuishi na matumaini ya kumpenda Richard siku zote, aliamini alikuwa ni mwanaume wa maisha yake hivyo hakukuwa na udanganyifu wowote uliyokuwa ukiendelea.
Kipindi hicho ambapo Monalisa alikuwa amefanikiwa kuwa na Richard kimapenzi zilianza kuvuma tetesi za chinichini pale chuoni kuwa wawili hao walikuwa wakitoka kimapenzi, Evelyne baada ya kuzisikia tetesi hizo aliamua kuzipuuzia, alimuamini sana Richard hivyo kila kitu ambacho alikuwa akiambiwa kibaya kilichomuhusu mwanaume wake huyo aliweza kukikanusha, hakutaka kuishi na wasiwasi.
“Why don’t you want to believe everything you’re told about Richard?” (Kwanini hutaki kuamini kila kitu kibaya unachoambiwa kuhusu Richard?) aliuliza Happy.
“No, one loves him so much, he loves me so much so I know he can’t do any harm to me,” (Hapana, ninampenda sana, ananipenda pia hata hivyo najua hawezi kunifanyia ukatili wowote,) alijibu Evelyne.
Evelyne alizidi kuishi na imani hiyo ya kumpenda sana Richard kuliko mwanaume yoyote chuoni pale, aliwakataa wanaume wengi sana, kila kitu alichokuwa anakifanya alikifanya kwa ajili ya Richard.
Kipindi ambapo zilianza kuvuma tetesi chuoni kuwa Richard na Monalisa walikuwa wakitoka kimapenzi alizikataa, hakutaka kuamini kirahisi bila kujua kuwa huo ndiyo ukweli uliyokuwa ukiendelea nyuma ya pazia.

Je, ni nini kitaendelea?
Evelyne atafanya nini baada ya kuujua ukweli kuwa Richard amemsaliti?
 
NISAMEHE MPENZI-05
Mtunzi:Juma Hiza
0712988278

ILIPOISHIA.....

Kipindi ambapo zilianza kuvuma tetesi chuoni kuwa Richard na Monalisa walikuwa wakitoka kimapenzi alizikataa, hakutaka kuamini kirahisi bila kujua kuwa huo ndiyo ukweli uliyokuwa ukiendelea nyuma ya pazia.

SONGA NAYO.....

Katika mapenzi hakuna kitu kibaya kama kumpenda mtu ambaye hakupendi, kumthamini mtu ambaye hakuthamini, Kumjali mtu ambaye hakujali, hatambui thamani yako kwake baada ya kukutumia.
Hakuna maumivu makali ya moyo kama kuwa na mapenzi ya dhati na mtu ambaye nyuma ya pazia anakusaliti. Huo ndiyo huwa mwanzo wa maumivu ya mapenzi, kuna muda unaweza ukafikia mtu usitamani kabisa kupenda, moyo ukajenga chuki ukamuona kila mwanaume au mwanamke ni adui yako.
Waliyosema mapenzi ni upofu hawakukosea na hivi ndivyo ambavyo ilikuwa kwa Evelyne, licha ya kuzisikia tetesi juu ya Richard lakini hakutaka kuziamini, alimuamini mno mwanaume huyo.
Adela, Mary pamoja na Penina hawa ndiyo walikuwa wasichana wa kwanza kumpa taarifika hizo Evelyne, walitumia kila njia ya kumueleza ukweli uliyokuwa ukiendelea kati ya Richard na Monalisa lakini Evelyne hakuwaamini.
“Huo ndiyo ukweli shosti Richard sasa hivi sio wako tena,” alisema Mary, wakati huo walikuwa kwenye kimbweta, ulikuwa ni muda ambao hawakuwa na kipindi darasani.
“Umemaliza?” aliuliza Evelyne huku akionekana kuyapuuzia maneno ya Mary, hakutaka kuyaamini.
“Monalisa sasa hivi ndiyo ameichukua nafasi yako, huna chako tena,” alisema Penina kwa sauti ya juu kidogo.
“Lakini mimi naona tumuache, tusiendelee kumlazimisha auamini ukweli ambao siku si nyingi utakuwa wazi,” alisema Adela huku akionekana kumkomoa Evelyne.
Kila neno alilokuwa akiambiwa Evelyne hakutaka kuliamini, alipuuzia na mwisho wa siku aliendelea kusoma kama ilivyokuwa kawaida yake. Alikuwa ni msichana mwenye mapenzi ya dhati mno kwa mpenzi wake huyo ambaye tayari alikuwa ameshamsaliti.
“Siwezi kuamini kama Richard anaweza akanisaliti, siamini,” alisema Evelyne alipokuwa ndani ya chumba chake, wakati huo Happy alikuwa akimtazama.
“Evelyne hivi unajua kuwa lisemwalo lipo na kama halipo basi jua linakuja,” alisema Happy huku akiendelea kumtazama Evelyne ambaye alionekana kuwa amekufa ameoza kwa Richard.
“Happy nafikiri unamfahamu Richard vizuri, sio mgeni kwako, nadhani unajua ni wapi nilipotoka naye hivi unaweza ukaamini hiki ninachokisikia kuwa ananisaliti?”
“Lakini wanaume sio watu wa kuwaamini kiasi hiko.”
“Sio kwa Richard lakini.”
“Umemuuliza?”
“Kuhusu nini?”
“Kuhusu hizi habari?”
“Hapana.”
“Halafu mbona yeye na Monalisa leo hawajaingia chuo?”
“Aliniambia anajisikia vibaya hivyo ameshindwa kuja.”
“Na Monalisa?”
“Sijui kuhusu habari zake.”
“Mmh!” aliguna Happy.
Alichoamua kukifanya Evelyne ni kuichukua simu yake ya mkononi kisha akampigia Richard, alihitaji kufahamu hali yake kwa wakati huo lakini kitu cha kushangaza simu ya Richard ilikuwa ikiita bila kupokelewa, alianza kuingiwa na hofu kubwa moyoni, hakujua ni nini kilichokuwa kimemkuta mpenzi wake ambaye alimuambia kuwa anaumwa.
“Mungu wangu.”
“Nini?”
“Richard hapokei simu.”
“Umejaribu kupiga namba zake zote?”
“Ndiyo nimepiga lakini hapokei,” alijibu Evelyne huku hofu ikiwa tayari imemuingia, alianza kujiwa na hisia mbaya kwa mpenzi wake huyo kuwa pengine alikuwa amezidiwa kiasi cha kulazwa hospitalini. Kichwani mwake wazo la kuwa pengine Richard alikuwa na mwanamke mwingine na hiyo ndiyo sababu ya yeye kutopokea simu hakutaka kuliwazia.
****
Moyo wa Richard ulikuwa katika hofu kubwa mno, hakutaka kuamini kama kweli alikuwa amemsaliti Evelyne tena katika mazingira ambayo hakuyategemea.
“Nadhani biashara yetu imeishia hapa,” alisema Richard alipoamka asubuhi na kumkuta Monalisa akiwa tayari ameshajiandaa na kwa wakati huo alikuwa ameketi kitandani huku akiiperuzi simu yake.
“Itaisha vipi wakati mimi na wewe tayari ni wapenzi?” aliuliza Monalisa huku akijibebisha.
“Monalisa unajua unanichanganya kwani haya ndiyo yalikuwa makubaliano yetu?”
“Mimi sijui ila fahamu kuwa sisi tumeshakuwa wapenzi.”
“Acha utani Monalisa.”
“Tangu lini nimeanza utani na wewe?”
“Monalisa lakini si unajua kuwa mimi nina mpenzi wangu na ninampenda sana.”
“Hilo silijui kama kweli ulikuwa unampenzi na unampenda kwanini umekubali kumsaliti, kwanini umekubali kunikubaliana ombi langu.”
“Unasemaje?”
“Tayari umeshakuwa mpenzi wangu,” alijibu Monalisa huku akitabasamu.
Richard alikurupuka pale kitandani kisha akaanza kuitafuta simu yake, hakuiona ilibidi amuulize Monalisa.
“Simu yangu iko wapi?”
“Ninayo.”
“Naiomba.”
“Siwezi kukupa,” alijibu Monalisa kisha akaamka pale kitandani akatoka nje huku akiwa anakimbia, Richard alishindwa kumfuata Monalisa kwani kwa wakati huo alikuwa uchi wa mnyama, alibaki pale kitandani huku akilalamika, alijilaumu mno kwa kufanya kosa la kumsaliti mpenzi wake ambaye aliamini kwa vyovyote alikuwa anaenda kumpoteza katika maisha yake huku sababu kubwa ikiwa ni Monalisa msichana ambaye tayari alionekana kuwa sumu ya penzi hilo.

Je, ni nini kitaendelea?
Monalisa amedhamiria kufanya nini kuondoka na simu ya Richard?
 
NISAMEHE MPENZI-06
Mtunzi:Juma Hiza
0712988278

ILIPOISHIA.....

Richard alishindwa kumfuata Monalisa kwani kwa wakati huo alikuwa uchi wa mnyama, alibaki pale kitandani huku akilalamika, alijilaumu mno kwa kufanya kosa la kumsaliti mpenzi wake ambaye aliamini kwa vyovyote alikuwa anaenda kumpoteza katika maisha yake huku sababu kubwa ikiwa ni Monalisa msichana ambaye tayari alionekana kuwa sumu ya penzi hilo.

SONGA NAYO.......

Muda ambao Evelyne alikuwa akimpigia simu Richard ndiyo muda huohuo ambao Monalisa alikuwa na simu ya Richard. Hakutaka kuipokea simu baada ya kuona mpigaji alikuwa ni Evelyne, alipokuwa hostel kuna muda alitamani kuipokea lakini alisita kufanya hivyo, hakutaka kuwa na haraka ya kumpa maumivu Evelyne katika moyo wake mwisho aliamua kuizima kabisa.
Alichokuwa akikifikiria katika kichwa chake kwa wakati huo ni jinsi gani angeweza kumuumiza Evelyne, alifahamu fika alikuwa akimpenda sana Richard na hakutaka kusikia kitu chochote kuhusu mpenzi wake huyo.
“This will be the end of your love for Richard,” (Huu ndiyo utakuwa mwisho wako wa kumpenda Richard,) alijisemea Monalisa maneno aliyoyasindikiza na tusi zito.
Aliichukua simu yake kisha akaiwasha, kitu cha kwanza aliingia katika sehemu ya kuhifadhi picha na video, alianza kutabasamu baada ya kuziona picha alizokuwa amejipiga akiwa pamoja na Richard kitandani, wakati huo Richard alikuwa amelala, hakuishia hapo pia aliamua kuingia katika sehemu ya video na hapo aliweza kuitazama video aliyoirekodi kipindi alipokuwa amelala na Richard, wote walikuwa uchi wa mnyama.
Aliamini kwa asilimia kubwa ni lazima video ile pamoja na zile picha alizopiga na Richard kitandani ni lazima zingeweza kuyasambaratisha mapenzi ya wawili hao.
“Your dangerous,” (Wewe ni hatari.)
“I told you that I can’t never fail,” (Nilikuambia kuwa kamwe siwezi kushindwa.)
“So what you are going to do?” (Kwahiyo nini unakwenda kukifanya?)
“I must make sure I destroyed this love,” (Lazima nihakikishe naliangamiza penzi hili.)
“About those photos and videos Richard has he seen?” (kuhusu hizo picha na video Richard ameziona?)
“Everything I did in secret so they did not know anything,” (Kila kitu nilikifanya kwa siri hivyo hajui lolote.)
Yalikuwa ni mazungumzo kati ya Monalisa na Adela, wakati huo Monalisa alikuwa akimuonyesha picha na video aliyojirekodi kipindi alipokuwa amelala na Richard. Adela alishikwa na butwaa baada ya kuziona picha hizo pamoja na video iliyokuwa ikimuonyesha Monalisa akiwa juu ya kifua cha Richard.
“Itabidi uzifiche maana italeta picha mbaya endapo kila mtu akaziona,” alisema Adela huku akionekana kuogopa.
“Siogopi lolote ila ninachokitaka kuona nilichokipanga kinatimia,” alisema Monalisa.
“Unamaanisha nini?” aliuliza Adela.
“Nitamtumia hizi picha pamoja na hii video WhatsApp.”
“Nani?”.
“Evelyne.”
“Ataumia sana.”
“Nataka aumie zaidi yangu, nimeteseka sana katika kumpata Richard na huu ndiyo utakuwa mwanzo wa moyo wake kupokea maumivu ya kimapenzi,” alisema Monalisa huku akionekana kutokujali lolote.
Alidhamiria kufanya kila aliwezalo ilimradi afanikiwe kuliangamiza penzi hilo ambalo hakupendezewa nalo hata kidogo, alitamani yeye ndiye awe mpenzi wa Richard hivyo kwake kufanya lolote kwa ajili ya penzi hilo bila kujali maumivu ambayo angeweza kuyasababisha kwa Evelyne.
Hakutaka kupoteza muda alichoamua kukifanya usiku wa siku hiyo aliamua kuwasha data kweye simu yake kisha akaingia WhatsApp, alianza kuitafuta namba ya Evelyne ambayo alikuwa ameisevu kwa jina la “Vomiting” (Matapishi.) alipoliona jina hilo alilibonyeza kisha akaingia moja kwa moja katika uwanja wa kuandika ujumbe na kutuma chohote na kama alivyokuwa amepanga alianza kumtumia zile picha pamoja na video ambayo ilikuwa ikimuonyesha yeye akiwa kitandani pamoja na Richard.
Hakuishia hapo baada ya kumaliza kumtumia aliamua kuandika maneno machache ambayo pia alimtumia Evelyne, maneno hayo yalisomeka kwa herufi kubwa “YOUR HUSBAND.” (MUME WAKO.)
****
Richard alikuwa chumbani kwake huku akionekana kutokuwa sawa kabisa, hakutaka kuamini kwa kile kilichokuwa kimetokea siku hiyo alipokuwa hotelini.
Kichwani kwake mawazo ya Monalisa ndiyo yalikuwa yamemtawala, alikumbuka kila kitu kilichokuwa kimetokea lakini hakutaka kuamini hata kidogo, kuna muda alihisi labda alikuwa katika ndoto lakini haikuwa hivyo, alizidi kuchanganyikiwa baada ya kukumbuka kuwa simu yake aliichukua msichana huyo na kukimbia nayo.
Muda mwingine alimkumbuka mpenzi wake Evelyne, aliamini kwa vyovyote ni lazima alikuwa akimtafuta na kwa muda huo simu yake alikuwa nayo Monalisa.
“Mungu wangu sijui Monalisa akipokea atamuambia nini?” alijiuliza swali hili katika mawazo yake.
Hakufahamu ni nini alichokuwa amedhamiria kukifanya Monalisa, alibaki katika hali ya sintofahamu huku asijue nini alitakiwa kukifanya kwa wakati huo.
Wakati akiendelea kuwaza mambo yote hayo lilimjia wazo kichwani, lilikuwa ni wazo la kumtafuta Evelyne kwa njia yoyote ili aweze kuzungumza naye, alipokumbuka umbali uliyokuwepo kati ya Mikocheni na Kigamboni alighairi kuchukua maamuzi hayo.
Alikumbuka kuwa Evelyne alikuwa akijulikana na Mama yake na alikuwa akipenda kuwasiliana naye mara kwa mara, hakutaka siku hiyo iweze kupita bila ya kuzungumza naye. Alichoamua kukifanya ni kwenda kumuomba Mama yake simu kisha akampigia, simu ya Evelyne ilikuwa ikiita bila ya kupokelewa.
“Mbona hapokei simu ni nini kimemkuta?” alijiuliza Richard baada ya kumpigia simu Evelyne zaidi ya mara tatu bila kupokelewa.
Hakutaka kukata tamaa, aliendelea kupiga huku akitegemea kuna muda Evelyne angeweza kuipokea simu hiyo lakini tukio hilo halikuweza kutokea.
****
“Punguza wasiwasi Richard yuko salama.”
“Nitapunguzaje na wakati hapokei simu yangu.”
“Labda yupo mbali na simu yake.”
“Sio rahisi.”
“Sasa unahisi atakuwa wapi?”
“Embu ngoja nijaribu kumpigia tena,” alisema Evelyne kisha akaamua kuipiga simu ya Richard kwa mara nyingine tena, safari hii simu ilikuwa haipatikani, akahisi labda mtandao ulikuwa unasumbua hivyo akarudia kupiga tena huku akijaribu kuzunguka huku na kule mule chumbani lakini majibu yalikuwa ni yaleyale.
“Hapatikani,” alisema kwa sauti ya unyonge.
“Hapatikani?” aliuliza Happy kwa mshangao.
“Ndiyo,” alijibu Evelyne kisha akakaa chini, nguvu zilikuwa zimeanza kumuishia kwa wakati huo.
“Mbona alikuwa anapatikana lakini?”
“Mimi sijui ni nini kilichomkuta Richard wangu jamani.”
“Embu ngoja nijaribu na mimi kumpigia,” alisema Happy kisha akaichukua simu yake halafu akampigia Richard, hakukuwa na jibu lingine alilojibiwa kwa wakati huo zaidi ya kuisikia sauti ya msichana ikimuambia “ Mtumiaji wa simu unayempigia kwa sasa hapatikani, tafadhili jaribu tena baadae.
Evelyne aliendelea kuwa ni mwenye wasiwasi mkubwa baada kuona Richard hapatikani, tukio hilo lilizidi kumnyima furaha kabisa katika moyo wake, alikosa amani muda wote alikuwa akimfikiria Richard.
“Kwanini nakufikiria muda wote Richard utakuwa umepatwa na nini?” alijiuliza kwa sauti mpaka Happy akamsikia.
“Usiwaze hayo kama Richard angekuwa amepatwa na tatizo ni lazima ungepata taarifa.”
“Nani angeniambia?”
“Mama yake,” alijibu Happy kisha akamfanya Evelyne apunguze wasiwasi kidogo, alianza kuyaamini maneno ya rafiki yake baada ya kukumbuka alikuwa akifahamiana na Mama yake Richard, alimuheshimu sana Mama mkwe wake mtarajiwa na hii ndiyo sababu iliyomfanya ashindwe kumpigia simu.
Usiku wa siku hiyo Evelyne alishindwa kulala kabisa, hakutaka kuamini kama siku hiyo alikuwa analala bila kuzungumza wala kuchati na Richard. Japo aliambiwa na Happy apunguze wasiwasi lakini hakutaka kukubaliana na jambo hilo. Wakati Happy alipokuwa amelala usingizi yeye aliamka kisha akaanza kumpigia simu Richard lakini bado alikuwa hapatikani.
Baada ya kuona ameshindwa kupata usingizi kabisa aliamua kuwasha data simu yake kisha akaingia WhatsApp kwa lengo la kujibu jumbe za watu waliyokuwa wamemtumia kwa siku hiyo, alianza kuzipitia moja baada ya nyingine.
Hakutaka kuamini macho yake baada ya kuona ujumbe kutoka kwa Monalisa, haraka aliufungua na ni hapo ambapo alishikwa na bumbuwazi baada ya kukutana na picha pamoja na video iliyokuwa ikimuonyesha Richard na Monalisa wakiwa kitandani. “YOUR HUSBAND” (MUME WAKO.) aliyasoma maneno haya mara mbilimbili, hakutaka kuamini hata kidogo kile alichokuwa akikiona kwa wakati huo.

Je, nini kitaendelea?
 
NISAMEHE MPENZI-07
Mtunzi:Juma Hiza
0712988278

ILIPOISHIA.....

Hakutaka kuamini macho yake baada ya kuona ujumbe kutoka kwa Monalisa, haraka aliufungua na ni hapo ambapo alishikwa na bumbuwazi baada ya kukutana na picha pamoja na video iliyokuwa ikimuonyesha Richard na Monalisa wakiwa kitandani. “YOUR HUSBAND” (MUME WAKO.) aliyasoma maneno haya mara mbilimbili, hakutaka kuamini hata kidogo kile alichokuwa akikiona kwa wakati huo.

SONGA NAYO.....

Kitendo cha kuziona picha za mpenzi wake akiwa amelala kitandani na Monalisa hakika zilimuumiza mno moyo wake, alihisi kupata maumivu makali asiyoyatarajia kwa wakati huo.
Kila kitu alichokuwa akikiona katika picha hizo kilimfanya abaki katika wakati wa maumivu mno. Machozi yalianza kumbubujika mashavuni mwake, akajaribu kuyafuta lakini huo haukuwa ndiyo mwisho wa kuyamaliza, yalizidi kumbubujika mfululizo bila kukoma.
Hakukuwa na kitu kingine kilichokuwa kikimuumiza moyo wake zaidi ya usaliti, alisalitiwa na mpenzi wake ambaye alikuwa akimpenda sana. Alikumbuka mambo mengi waliyowahi kuyafanya na Richard katika mapenzi yao lakini mambo yote hayo yalibaki kuwa hayana mashiko yoyote.
Muda huo ambao alikuwa katika maumivu ghafla! simu yake ikawa inaita, alipaitazama mpigaji wa simu hiyo aliliona jina la Mama Richard, hakutaka kupokea, aliamini Richard ndiye aliyekuwa akimpigia. Hakutaka kuzungumza naye lolote hivyo aliamua kuiacha simu iendelee kuita mpaka pale ilipokata. Aliendelea kulia huku akiwa ameukumbatia mto pale kitandani.
****
Monalisa alikuwa katika furaha isiyokuwa na kifani, muda wote alikuwa ni mtu wa kucheka peke yake baada ya kufanikiwa kumtumia picha Evelyne. Aliamini picha hizo lazima zingeweza kuliua penzi kati ya Richard na Evelyne na hiyo ndiyo sababu iliyomfanya azidi kubaki akiwa ni mtu mwenye furaha muda wote.
Aliamini hakuwa na sababu ya kuendelea kulia au kuumia tena kwani mwanaume aliyekuwa akimuhitaji tayari alikuwa ni wake, hilo lilizidi kumfurahisha mno.
“Amekujibu lolote mpaka sasa baada ya kumtumia hizo picha?” aliuliza Adela.
“Hapana bado hajanijibu ila amezipokea tayari,” alijibu Monalisa huku akitabasamu.
“Hivi umejiamini nini mpaka ukaamua kuzipiga hizo picha?”
“Nampenda sana Richard, nimeshindwa kujizuia kwa kweli imenibidi nifanye hivyo,” alijibu Monalisa.
Monalisa aliendelea kuushikilia msimamo wake wa kumpenda Richard, muda mwingine aliamini kwa tukio alilokuwa amelifanya la kumtumia picha za utupu Evelyne ni lazima zingeweza kuwagombanisha wawili hao na huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kulifaidi penzi la Richard kwa uhuru. Alichokuwa anakihitaji ni kuwa na Richard bila kujali maumivu ambayo alikuwa anaenda kuwapa wawili hao waliyokuwa wanapendana kwa dhati.
Adela ndiye alikuwa msichana pekee ambaye alifahamu kila kitu kilichokuwa kikiendelea kuhusiana na picha ambazo alikuwa amezipiga Monalisa na Richard.
Monalisa aliamua kumuonyesha Adela picha hizo huku akiwaficha Penina na Mary, hakutaka wafahamu lolote zaidi ya uhusiano wake na Richard tu.
“Kwanini nisiwaambie?” aliuliza Adela huku akionekana kushangazwa mno.
“Sitaki uwaambie lolote kuhusiana na hizi picha nilizozipiga,”alijibu Monalisa huku akimtazama kwa macho ya msisitizo Adela.
“Kuna kitu gani kinachoendelea kati yenu?”
“Hakuna.”
“Sasa kwanini hutaki niwaambie?”
“Nimeamua tu kwani picha ni zangu au za kwao?”
“Una uhakika hakuna tatizo?”
“Ndiyo hakuna,” alijibu Monalisa.
Waliendelea kuzungumza wakati huo Penina na Mary hawakuwepo hostel, mpaka kufikia muda huo Adela hakujua ni nini kilichokuwa kikiendelea mpaka Monalisa aamue kuwaficha Penina na Mary na wakati wote walikuwa ni marafiki na kila jambo ambalo alikuwa akilifanya ilikuwa ni lazima awaambie, hilo lilizidi kumchanganya kichwa chake.
****
Siku iliyofuata ndiyo ilikuwa ile siku ambayo Evelyne alishindwa kuendelea kubaki darasani baada ya kumuona Richard akiwa ameingia, alishindwa kuyavumilia maumivu ambayo moyo wake tayari ulikuwa umshayapata, alimchukia mno Richard na hakutaka kuendelea kumtazama katika mboni za macho yake.
Alichoamua kukifanya ni kuondoka kabisa eneo hilo la chuo huku akiamini kwa kufanya hivyo angeweza kuyapooza maumivu na machungu ambayo moyo wake ulikuwa ukipitia.
Rafiki yake Happy hakuwa anafahamu lolote lile lililokuwa limetokea, alibaki katika wakati mgumu baada ya Evelyne kushindwa kumuelezea ni nini kilichokuwa kimetokea na kwa wakati huo aliamua kuondoka zake.
Alitamani sana kufahamu ni nini kilichokuwa kimetokea na mtu pekee ambaye aliamini angeweza kumueleza ukweli wa mambo yote hayo alikuwa ni Richard lakini na yeye alishindwa kumueleza ukweli, alibaki akiwa haelewi ni nini kilichokuwa kimetokea baada ya kumuona mpenzi wake akiwa ameondoka.
“Unasema amerudi nyumbani?” aliuliza Richard huku akionekana kuwa mwenye wasiwasi.
“Ndiyo,” alijibu Happy.
“Kigamboni au?” aliuliza Richard.
“Richard inamaana hujui Evelyne anapoishi?” aliuliza Happy huku akionekana kumshangaa Richard kwa wakati huo.
“Hapana, nafahamu ila nimechanganyikiwa,” alijibu Richard.
“Halafu mbona jana ulikuwa unapigiwa simu hupatikani?” aliuliza Happy.
Richard alianza kukumbuka tukio la Monalisa kuichukua simu yake, alishindwa kutoa jibu la haraka, alibaki mithili ya mtu ambaye alikuwa akitafakari jambo na mwisho lilimjia jibu la kudanganya.
“Nimeibiwa,” alijibu.
Happy alianza kuingiwa na wasiwasi baada ya kumuona Richard akionekana kuficha ukweli wa jambo ambalo alihitaji kulifahamu, aliamini Richard alikuwa akifahamu kila kitu kilichokuwa kikiendelea lakini alishindwa kujua alitakiwa aanzie wapi kumuhoji ili aweze kumwambia.
“Una uhakika na unayonieleza?”
“Ndiyo nina uhakika,” alijibu Richard huku kijasho chembamba kikianza kumtoka mwilini.
Richard alishindwa kuzungumza ukweli kwasababu mpaka kufikia wakati huo hakujua ni nini kilichokuwa kimetokea, kuna muda alianza kuhisi labda Monalisa aliamua kumueleza ukweli Evelyne wa kile kilichokuwa kimetokea kati yao na hiyo ndiyo ilikuwa sababu iliyomfanya mpaka abadilike. Lilipomtoka wazo hilo liliingiwa wazo lingine hivyo alishindwa kabisa kuelewa ni nini ambacho alitakiwa kuzungumza.
“Unajua Richard sikuelewi unachokizungumza?”
“Hunielewi nini?”
“Mimi nahisi utakuwa unafahamu kila kitu kwasababu haiwezekani Evelyne halafu abadilike bila sababu.”
“Kama ningekuwa ninafahamu ukweli ningekueleza sasa kwanini nikufiche na kwanini nikufiche?”
“Namfahamu sana Evelyne mimi naamini kuna kitu kati yenu kimetokea.”
“Kitu gani?”
“Sikifahamu,” alijibu Happy.
Wazo lililomjia Richard kwa wakati huo ilikuwa ni kwenda Kigamboni nyumbani alipokuwa akiishi Evelyne na Happy, hakutaka kuendelea kubaki katika mabishano na Happy, alitamani kufahamu ni nini kilichokuwa kimemtokea mpenzi wake bila kujua kuwa kumbe yeye ndiye alikuwa sababu ya mambo yote hayo kutokea.
“Let’s go.” (Twende zetu.)
“Where?” (Wapi?)
“I say let’s go.” (Nasema twende.)
“Where?” (Wapi?)
“Kigamboni.”
“Okay, but let me then I take a bag to class,” (Sawa ila ngoja basi nikachukue begi darasani.”
“Hurry up,’ (Fanya haraka,) alisema Richard kisha Happy akafanya kama alivyoomba, aliporudi safari ya kwenda kigamboni ikaanzia hapo. Richard hakutaka kwenda na gari lake ili kuepuka usumbufu ambao wangeweza kukutana nao kivukoni, waliamua kupanda bajaji ambayo iliweza kuwafikisha mpaka kivukoni.
Mpaka kufikia muda huo Richard alitamani sana kumuona mpenzi wake ili aweze kuzungumza naye, moyoni aliamini katika mapenzi ya dhati ambayo aliahidi kamwe yasingeweza kufa.
Alimpenda sana Evelyne na aliamini hakukuwa na msichana mwingine ambaye angeweza kuiziba nafasi hiyo katika moyo wake, wakati ambao alikuwa akiendelea kuyawaza hayo nyuma ya pazia hakujua kuwa kumbe alikuwa amepigwa picha za utupu na Monalisa ambazo zilitumwa kwa Evelyne na picha hizo ndizo ambazo zilimfanya abadilike kiasi cha kuondoka kabisa eneo la chuo.

Je, ni nini kitaendelea?
 
NISAMEHE MPENZI-08
Mtunzi:Juma Hiza
0712988278

ILIPOISHIA.....

Alimpenda sana Evelyne na aliamini hakukuwa na msichana mwingine ambaye angeweza kuiziba nafasi hiyo katika moyo wake, wakati ambao alikuwa akiendelea kuyawaza hayo nyuma ya pazia hakujua kuwa kumbe alikuwa amepigwa picha za utupu na Monalisa ambazo zilitumwa kwa Evelyne na picha hizo ndizo ambazo zilimfanya abadilike kiasi cha kuondoka kabisa eneo la chuo.

SONGA NAYO.......

Walipokuwa wamepanda kwenye panton Richard alitamani liongeze mwendo ili aweze kufika haraka nyumbani alipokuwa akiishi Evelyne, alitamani kumuona mpenzi wake na kuzungumza naye kwa wakati huo. Alipokuwa ameketi alipaona kuwa kama kuna misumari iliyomchoma hivyo hakutaka kuendelea kuketi sehemu hiyo, alisimama na kuanza kuzunguka huku na kule kama mtu aliyeanza kuchanganyikiwa, kitendo hicho kiliwafanya baadhi ya watu waliyokuwemo kwenye panton hiyo waanze kumshangaa Richard.
Kichwani alikuwa akimuwaza Evelyne tu, hakutaka kuzungumza lolote na Happy, kimoyomoyo alikuwa akiomba wawahi kufika haraka ili aweze kuzungumza na mpenzi wake huyo.
Baada ya kupita dakika kadhaa waliweza kuvuka salama kisha wakaianza safari ya kuelekea nyumbani alipokuwa akiishi Evelyne pamoja na Happy, palikuwa na umbali kidogo hivyo waliamua kutumia usafiri wa bajaji ambao uliweza kuwafikisha kwa haraka sana.
Baada ya bajaji hiyo kuwafikisha walishuka kisha Richard akamlipa dereva wa bajaji kiasi cha pesa alichokuwa anawadai, alipomalizana na dereva huyo walitembea kidogo mpaka kufika katika chumba ambacho alikuwa anaishi Evelyne pamoja na Happy.
Walipoingia ndani ya chumba hicho walimkuta Evelyne akiwa amejilaza kitandani huku akiwa analia, alionekana kutochukua muda mrefu tangu alipoweza kuingia katika chumba hicho. Alipohisi kuna watu wameingia ndani aliamka na kuwatazama.
Hakutaka kuamini macho yake baada ya kumuona Richard akiwa ndani ya chumba hicho, hasira zilizidi kumpanda, alihisi kumuona adui mkubwa wa maisha yake ambaye alimchukia sana.
Alichokuwa anakihitaji Richard kwa wakati huo ni kupewa nafasi ya kuzungumza na Evelyne ili aweze kujua ni nini kilichokuwa kimetokea mpaka akaamua kuondoka chuoni lakini nafasi hiyo ilikuwa ngumu mno kupatikana. Evelyne hakuwa tayari kuzungumza naye lolote.
“Happy naomba umtoe huyu ibilisi nje, sitaki kumuona katika macho yangu,” alisema Evelyne huku akiendelea kulia.
“Kuna nini kimetokea Eve mbona sikuelewi?” aliuliza Happy huku akizidi kuchanganywa na maneno ya rafiki yake, hakuelewa ni nini kilichokuwa kimetokea mpaka kikamfanya Evelyne abadilike kiasi kile.
“Nimesema sitaki kumuona Richard katika macho yangu, naomba utoke Richard, sikutaki kukuona,” alisema Evelyne kisha akaanza kumfukuza Richard.
“Lakini Richard si mpenzi wako?” aliuliza Happy.
“Alikuwa mpenzi wangu lakini sio sasa naomba umtoe,” alijibu Evelyne kwa sauti ya kilio iliyo sanjari na maumivu pamoja na hasira.
Richard hakutaka kuamini kile alichokuwa akikisikia kutoka kwa mpenzi wake huyo, aliamini hakukuwa na tatizo lolote lile hivyo bado alizidi kuomba kupewa nafasi ya kuzungumza naye.
“Mpenzi wangu naomba unipe nafasi ya kuzungumza na wewe, niambie nini kimetokea mbona unanichukia bila sababu?” aliuliza Richard huku akimtazama Evelyne ambaye alikuwa akilia kwa wakati huo, hakutaka kuendelea kuyashuhudia machozi ya mpenzi wake yakiendelea kumbubujika mfululizo, alichoamua kukifanya akakitoa kitambaa mfukoni mwake kisha akahitaji kumfuta machozi lakini kabla hajamsogelea kwa lengo la kumfuta machozi alishtukia akipigwa kibao na Evelyne.
“Naomba utoke Richard sitaki kuzungumza lolote na wewe,” alisema Evelyne kisha akamfukuza Richard, wakati huo alikuwa akilia.
Richard alishindwa kabisa kuamua nini la kufanya kwasababu kila alilokuwa anahitaji litokee kwa muda huo lilishindikana, alimbembeleza sana mpenzi wake huyo ili aweze kumuambia ni nini ambacho kilikuwa kimetokea lakini hakuwa tayari kuzungumza lolote.
Hakutaka kuondoka kirahisi wakati alipokuwa akifukuzwa lakini mwisho ilibidi Happy amuombe aondoke eneo hilo kwani ilikuwa ni kawaida ya Evelyne kutozungumza lolote kipindi ambapo alikuwa katika hasira. Alimuahidi kipindi ambapo hasira za Evelyne zitakapokuwa zimeisha ndipo angeweza kupata muda wa kuzungumza naye.
****
Tukio zima la kuondoka Evelyne darasani pamoja na Happy akifuatiwa na Richard kila mtu aliliona, siku hiyo wanachuo hawakuwa na stori nyingine zaidi ya kuwajadili wawili hao. Kila mtu alizungumza lake huku wale marafiki wa wakaribu wa wahusika hao wakijaribu kuwatetea.
“Yule jamaa anafeli asipoangalia yani demu anamchanganya kiasi kile,” alisema mwanachuo mmoja mvulana alipokuwa kwenye kundi la wavulana wenzake.
“Unajua hata Lecture hajapenda kabisa walivyoondoka ameona kama wamemdharau,” alisema mwanachuo mwingine ambaye alionekana kumuunga mkono mwenzake.
Kila mtu alisikika akisema lake lakini kwa upande ambao alikuwa amekaa Monalisa, Penina, Mary pamoja na Adela mazungumzo yao yalikuwa tofauti kidogo.
“Na bado huu ndiyo mwanzo tu,” alisema Monalisa.
“Yani mpaka nakuonea wivu?” alisema Mary.
“Richard lazima atabaki mikononi mwangu, mimi ndiyo Mona mwingine fotokopi,’ alisema Monalisa huku akijishebedua.
“Nakuaminia shosti huwezi kuniangusha,” alisema Penina kisha wakagongeana huku wakicheka kwa sauti kubwa.
Kila kitu kilichokuwa kikiendelea kati ya Evelyne na Richard, Monalisa alifahamu yeye kuwa ndiye chanzo hivyo hakuonekana kujali lolote. Muda wa furaha ndiyo ulikuwa umetawala katika maisha yake, aliamini kwa asilimia zote kuwa ule ndiyo ulikuwa mwanzo wa kushiriki mapenzi na Richard tena kwa uhuru baada ya kufanikiwa kumpa maumivu Evelyne.
Kwa upande wa Adela hakuonekana kupendezewa na kitendo kile alichokuwa amekifanya Monalisa japo alikuwa ni rafiki yake waliyeshibana chuoni pale lakini alimuona kuwa kama binadamu katili, mwenye roho mbaya mithili ya mnyama.
Kila alipokuwa akimtazama alishindwa kummaliza, wakati ambao Monalisa, Penina na Mary walipokuwa wakifurahia tukio hilo yeye alibaki akimuhurumia Evelyne.
Licha ya kuwa kipindi cha nyuma aliwahi kumpenda Richard na kuhitaji kuwa naye kimapenzi lakini baada ya kugundua kuwa Evelyne ndiye msichana pekee ambaye alikuwa akijihusisha kimapenzi na Richard aliamua kubadili mawazo yake, hakutaka kuliingilia penzi hilo ambalo wasichana wengi chuoni pale walitamani kuliingilia.
Aliamini kwa vyovyote ni lazima Evelyne alikuwa katika maumivu makali sana baada ya kutumiwa picha za utupu zilizokuwa zikimuonyesha mpenzi wake akiwa pamoja na Monalisa kitandani.
Hakutaka kuendelea kuushuhudia ukatili huo wa kimapenzi aliyokuwa akiufanya Monalisa, alipanga kufanya lolote lile ilimradi aweze kulirudisha penzi la wawili hao ambalo tayari lilikuwa limeshapotea.
****
Richard alirudi chuoni na aliamua kumtafuta Monalisa, alihitaji kuzungumza naye, alihisi alifahamu kila kitu kilichokuwa kikiendelea lakini kabla ya mazungumzo yao kuanza Monalisa alimrudishia simu yake.
“Nini umefanya Monalisa?” aliuliza Richard kwa sauti ya ukali baada ya kuipokea simu yake ambayo ilikuwa imezimwa, aliiwasha.
“Nimefanya nini kuhusu nini?” aliuliza Monalisa kisha akaanza kucheka kwa sauti ya kinafki.
“Umemuambia nini Evelyne mbona amenichukia ghafla?” aliuliza Richard.
“Kuna kitu gani ambacho hukifahamu kinachoendelea kati yetu.”
“Mona kama kuwa katika mahusiano mimi na wewe tulizungumza na siku ile ndiyo ilikuwa mwisho kwanini lakini unataka kuniharibia mapenzi yangu, kwanini unataka kunigombanisha na mpenzi wangu.”
“Nikugombanishe mara ngapi?”
“Unasemaje?”
“Richard nimeamua kuuweka ukweli wazi kuwa mimi na wewe ni wapenzi na tena kama ulikuwa hujui nilikupiga picha za utupu wakati ulipokuwa umelala na nimemtumia,” alijibu Monalisa huku akionekana kujiamini, hakuishia kuzungumza kwa maneno bali alichoamua kukifanya ni kuiwasha simu yake na kuanza kumuonyesha picha hizo.
Richard hakutaka kuamini kile alichokuwa akikiona kwa wakati huo, alihisi kuchanganyikiwa.
“Richard wewe ni mwanaume gani usiyeelewa kuwa nakupenda, kila siku nateseka kwa ajili yako, naishi kwa wasiwasi kwasababu yako na nimeamua kufanya yote haya kwasababu yako nakupenda mno na kama tatizo ni huyo kinyago wako Evelyne nimeshamkomesha,” alijibu Monalisa maneno ambayo aliyatamka kwa hisia, muda huo machozi yalikuwa yakimdondoka.
Richard alizidi kuchanganyikiwa baada ya kusikia kuwa picha hizo ziliweza kutumwa kwa mpenzi wake. Hilo lilizidi kumuweka katika wakati wa mawazo sana, kama kumsaliti ni kweli alikuwa tayari ameshamsaliti mpenzi wake japo hakupenda lakini kibaya kilichozidi kumuumiza ni kitendo cha kupigwa picha za utupu bila kujijua, hilo lilizidi kumuumiza mno moyo wake.
“Lakini kwanini umefanya haya Mona?”
‘”Kwasababu nakupenda Richard hivi ulitaka nifanye nini ili ujue kuwa nakupenda, nakupenda nakupenda Richard mno,”alijibu Monalisa huku akijaribu kumkumbatia Richard lakini hakuweza kufanikiwa.
Richard hakutaka kuendelea kubaki eneo hilo, aliamua kupanda kwenye gari lake kisha akaondoka zake. Alipokuwa barabarani kichwa chake kilitawaliwa na mawazo sana, alikuwa akimfikiria mpenzi wake lakini kikubwa zaidi alichokuwa akikiwaza ni juu ya picha za utupu ambazo alipigwa bila kujijua na kibaya zaidi aliweza kutumiwa mpenzi wake.

Je, ni nini kitaendelea?
 
NISAMEHE MPENZI-09
Mtunzi:Juma Hiza
0712988278

ILIPOISHIA........

Richard hakutaka kuendelea kubaki eneo hilo, aliamua kupanda kwenye gari lake kisha akaondoka zake. Alipokuwa barabarani kichwa chake kilitawaliwa na mawazo sana, alikuwa akimfikiria mpenzi wake lakini kikubwa zaidi alichokuwa akikiwaza ni juu ya picha za utupu ambazo alipigwa bila kujijua na kibaya zaidi aliweza kutumiwa mpenzi wake.

SONGA NAYO.....

Moyo wake bado uliendelea kumuuma, alijilaumu sana kwa kitendo alichokuwa amekifanya cha kumsaliti mpenzi wake ambaye kwa wakati huo alikuwa akifahamu kila kitu kilichokuwa kimetokea. Hakutaka kuamini hata mara moja kila alipokuwa akiyakumbuka maneno ya Monalisa na jinsi ambavyo alikuwa akijitamba, kuna muda alianza kumchukia lakini huo haukuwa ndiyo mwisho wa suluhisho wa kile kilichokuwa kimetokea.
Alipokuwa barabarani simu yake ilianza kuingia jumbe nyingi sana, alipozifungua na kuzisoma zilikuwa ni za mpenzi wake Evelyne ambazo zilimtaarifu kuwa alikuwa akimpigia simu kipindi ambapo alikuwa hapatikani. Hilo lilizidi kumuumiza mno.
Alipofika nyumbani siku hiyo hakuonekana kuwa sawa kama ilivyokuwa siku nyingine, ilibidi wazazi wake wamuulize baada ya kumuona mtoto wao akiwa katika hali hiyo, wakati huo walikuwa mezani wakila chakula cha usiku.
“Nini kinachokusumbua mwanangu?” aliuliza Mama yake aliyekuwa akijulikana kwa jina la bibi Magreth.
“Hakuna kitu Mama nipo sawa,” alijibu Richard.
“Sema kinachokusumbua sisi wazazi wako bado tupo hai usitufiche, kama tatizo ni pesa sema tunauwezo wa kukusaidia,” alisema Baba yake aliyekuwa akijulikana kwa jina la Mzee Gombanila.
“Baba na Mama sina tatizo lolote linalonisumbua,” alisema Richard.
Richard hakutaka kuwaeleza ukweli wazazi wake wa kile kilichokuwa kimetokea kati yake na mpenzi wake ambaye tayari walikuwa wakimfahamu.
“Umegombana na Evelyne?” aliuliza Mama yake.
“Hapana,” alijibu Richard.
“Sasa nini tatizo?” aliuliza tena Mama yake.
“Hakuna kitu Mama,” alijibu Richard.
“Unaonekana kuna kitu unajaribu kukificha lakini moyo wako unakataa, tuambie sisi wazazi wako tunaweza tukakusaidia,”alisema Baba yake.
“Hapana Baba sidhani kama kuna msaada ninauhitaji kutoka kwenu kwa sasa ila kama ikitokea nitakuwa nikiuhitaji nitafanya hivyo,” alisema Richard.
Baada ya kuona maswali ya wazazi wake yamezidi kuwa mengi pale mezani aliamua kuacha kuendelea kula kisha akaenda chumbani kwake, alipofika humo alijifungia. Moyo wake bado uliendelea kumuuma mno, hakutaka kuamini kama ule ndiyo ulikuwa mwisho wa mapenzi yake na Evelyne.
“No, Evelyne siamini kama huu ndiyo mwisho wa mapenzi yetu sitaki kuamini hata mara moja kama naenda kukupoteza katika maisha yangu, sitakubali tukio kama hili linitokee, nitahakikisha unabaki kuwa wangu peke yangu,” alijisemea Richard, wakati huo alikuwa akiitazama picha ya Evelyne.
****
Evelyne alikuwa ni mtu wa kulia muda wote, Happy alipata kazi ya kumbembeleza rafiki yake bila mafanikio. Mpaka kufikia muda huo hakufahamu ni nini kilichokuwa kimetokea. Baada ya kuona Evelyne anazidi kulia bila kuwepo mafanikio yoyote ya kunyamaza aliamua kuichukua simu yake na ndipo hapo alipoweza kuziona picha za utupu za Monalisa pamoja na Richard.
Picha hizo zilimshtua sana, hakutaka kuamini kile alichokuwa akikiona katika picha hizo, kuna muda alianza kuhisi labda pengine alimfananisha mwanaume aliyekuwa akimuona katika picha hiyo na Richard lakini ukweli ulibaki kuwa mwanaume huyo hakuwa mwingine isipokuwa ni Richard.
“Mungu wangu ni nini hiki?” alijikuta akiuliza swali ambalo hakutegemea kama angeliuliza, hakukuwa na mtu wa kumjibu zaidi ya sauti ya kilio cha kwikwi kutoka kwa Evelyne ndiyo ilikuwa imetawala ndani ya chumba hicho.
Mapenzi yaligeuka kuwa maumivu makali mno katika moyo wa Evelyne, alijutia mambo mengi sana ambayo aliwahi kuyafanya na Richard, licha ya kuwa alitokea katika maisha ya kimasikini lakini shina la mapenzi halikuacha kuchipua kati yake na Richard mwanaume aliyeanzisha mahusiano naye tangu mwaka wa kwanza wa degree yake chuoni.
Katika mapenzi yao walifanya starehe nyingi sana, walienda sehemu mbalimbali lakini kubwa ni kiapo ambacho waliwahi kuwekeana katika mapenzi yao kuwa hawatoweza kusalitiana wala kupeana maumivu ya aina yoyote ile ya kimapenzi.
Muda ambao Evelyne alikuwa akilia ulikuwa ndiyo muda ambao moyo wake tayari umeshapokea maumivu ya kimapenzi, hakutaka kuamini kama Richard yule ambaye aliwahi kula kiapo mbele yake kuwa hatoweza kumsaliti wala kumpa maumivu yoyote ya kimapenzi ndiye ambaye alikuwa amemsababishia maumivu katika moyo wake, hilo lilizidi kumuumiza.
“Siamini kama kweli Richard ameweza kunifanyia hivi, yani mapenzi yangu yote niliyompa bado amenisaliti ama kweli wanaume wabaya sana,” alisema Evelyne kwa sauti iliyoandamana na kilio.
“Kumbe kweli anatembea na Monalisa?” aliuliza Happy.
“Mwanzoni sikutaka kuamini niliposikia kuwa wanamahusiano, nilimuamini sana lakini katika hili siwezi tena kumuamini, ameuvunja uaminifu wangu kwake, namchukia sana,” alisema Evelyne.
Huo ulikuwa ni ukweli wenye kuuma mno tena mara zote alipomkumbuka mpenzi wake hakutaka kuamini, machozi yalikuwa yakimtoka.

Je, ni nini kitaendelea?
 
NISAMEHE MPENZI-10
Mtunzi:Juma Hiza
0712988278

ILIPOISHIA......

“Mwanzoni sikutaka kuamini niliposikia kuwa wanamahusiano, nilimuamini sana lakini katika hili siwezi tena kumuamini, ameuvunja uaminifu wangu kwake, namchukia sana,” alisema Evelyne.
Huo ulikuwa ni ukweli wenye kuuma mno tena mara zote alipomkumbuka mpenzi wake hakutaka kuamini, machozi yalikuwa yakimtoka.

SONGA NAYO....

Richard alizidi kuchanganyikiwa, kila alilokuwa akiliwaza kulifanya kama ishara ya kumuomba mpenzi wake msamaha aliona kama anakosea. Alizidi kuwa katika wakati mgumu sana kipindi ambacho alikuwa akimuona Evelyne darasani, kuna muda alitamani kuzungumza naye kisha amuombe msamaha lakini Evelyne hakuwa tayari, alimchukia mno Richard tena chuki za waziwazi.
Hakuwa na njia nyingine ya kufanya zaidi ya kumfuata Happy na kuamua kuzungumza naye, alihitaji kumuomba msamaha Evelyne lakini aliamini ilikuwa ni vigumu sana kwa yeye kuweza kueleweka, alijua kuwa alifanya makosa sana kwa kumsaliti mpenzi wake lakini bado hakutaka kuamini kuwa huo ndiyo mwisho wa mapenzi yake kwa Evelyne.
“Najua nimemkosea sana Evelyne lakini tafadhali mwambie asinichukie moyo wangu bado unampenda,” alisema Richard huku akimtazama Happy kwa macho ya huruma.
“Richard hivi kwanini umeamua kumsaliti Evelyne?” aliuliza Happy.
“Sijui hata niseme nini? Nashindwa kujielezea Happy, nashindwa nimejikuta tu namsaliti,” alijibu Richard.
“Richard embu acha kunifanya mimi mtoto mdogo wakati picha zako za uchafu na huyo mchepuko wako nimeziona yani sikutegemea kama ungeweza kumfanyia ukatili huu rafiki yangu, Richard wewe ni mbaya sana unatembea na Monalisa?” aliuliza Happy.
“Hapana usiseme hivyo narudia tena moyo wangu bado unampenda Evelyne na ninahitaji anisamehe, najua ananichukia sana lakini tafadhali jaribu kuzungumza naye pengine anaweza akabadili mawazo yake,” alisema Richard.
“Unadhani ni kazi rahisi kama unavyodhani?” aliuliza Happy.
“Najua ni ngumu lakini naomba unisaidie,” alijibu Richard kisha akampatia Happy kiasi cha shilingi 200,000 za kitanzania.
Baada ya mazungumzo hayo kumalizika Happy alimuahidi Richard kumsaidia katika hilo japo ilikuwa ni kazi ngumu ya kuzungumza na Evelyne lakini alijipa imani kufanikiwa kumshawishi mpaka akubali kumsamehe.
Aliporudi nyumbani siku hiyo Happy aliamua kuzungumza na Evelyne juu ya Richard. Evelyne baada ya kulisikia jina la Richard likitajwa mbele yake alibadilika, alimchukia sana mwanaume huyo.
“Rafiki yangu najua ni jinsi gani unavyomchukia Richard lakini kuna muda inabidi ukumbuke ni wapi mlipotoka, rudisha moyo wako nyuma,” alisema Happy.
“Unamaanisha nini?”aliuliza Evelyne.
“Richard bado anakupenda sana na anaomba umsamehe sana, anajutia kosa alilolifanya.”
“Kwahiyo?”
“Kwanini usimsamehe halafu maisha yakaendelea?”
“Siwezi kufanya hivyo hata mara moja halafu kuanzia leo naomba iwe ndiyo mwanzo na mwisho kusikia ukitamka jina la Richrd mbele yangu.”
“Msamehe tu.”
“Siwezi Happy, mwambie siwezi kumsamehe,” alisema Evelyne.
Alichokuwa akihitaji kukiona Happy ni Evelyne kukubali kumsamehe Richard lakini kila alipokuwa akijaribu kuzungumza naye ilishindikana, hakuwa tayari kumsamehe mpenzi wake.
****
Richard alikosa raha kabisa, alishindwa kula vizuri, alishindwa kulala pia muda wote aliutumia katika kumfikiria mpenzi wake. Licha ya utajiri wa familia yao, muonekano wake, urijali pamoja na wingi wa wasichana waliyokuwa wakimsumbua lakini alihisi kupoteza kitu cha thamani katika maisha yake.
Kitendo cha kumkosea Evelyne kiasi cha kushindwa kabisa kumsamehe alihisi kuipoteza nuru katika maisha yake. Alimjua vizuri Evelyne, alikuwa ni msichana wake ambaye aliyemuonyesha uvumilivu sana, alimuonyesha mapenzi ya dhati na mapenzi hayo ndiyo alikuwa ameyakumbuka.
****
Baada ya Monalisa kufanikiwa kulisambaratisha penzi kati ya Richard na Evelyne, hakutaka kuona wawili hao wakirudiana tena, alipanga kumdhibiti Richard, alihitaji kuona anakuwa mali yake hata hivyo hakukuwa na ugumu katika hilo, alipokumbuka kuwa bado zile picha pamoja na video alizozirekodi za utupu alikuwa nazo aliamua kuzitumia kama udhaifu wa kumnyanyasa kimapenzi Richard.
Licha ya kuwa kila siku Richard alijitahidi kumbembeleza Evelyne amsamehe kwa kosa alilokuwa amelifanya la usaliti lakini bado aliendelea kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Monalisa, aliamua kufanya hivyo hii ni kutokana na vitisho alivyokuwa akivipata kutoka kwa msichana huyo ambaye alimwambia kuwa kama wasingeweza kuendelea kuwa na mahusiano ya kimapenzi basi picha hizo angekuzisambaza katika mitandao ya kijamii.
Richard alihofia utajiri wa baba yake pamoja na heshima aliyokuwa nayo, Baba yake Mzee Gombanila alifahamika kama mfanyabiashara mwenye utajiri mkubwa sana hapa Tanzania hivyo hakuwa tayari kuona picha hizo zinamchafua yeye pamoja na Baba yake.
****
Happy alijitahidi kadri ya uwezo wake katika kumshawishi rafiki yake akubali kumsamehe Richard lakini jambo hilo lilikuwa ni gumu mno kutokea, kila mbinu aliyokuwa akiitumia iligonga mwamba.
Ilibidi afanye mawasiliano na Richard kisha wakapanga sehemu ya kukutana kwa ajili ya mazungumzo yao, walipanga kukutana Mlimani City, Samaki Samaki na sehemu hiyo ndipo walipopanga kufanya mazungumzo yao.
“Rich, Evelyne anakuchukia sana yani hataki kulisikia jina lako hata mara moja,” alisema Happy.
“Nalijua hilo lakini amesemaje?”
“Amekataa kabisa kukusamehe.”
“Umekumbuka kumueleza kuwa ninampenda?”
“Ndiyo ila kwa kifupi hataki kusikia habari zako,”alisema Happy kisha Richard akaonekana kuwa mwenye mawazo.
“Rich naweza kukuuliza kitu?”
“Ndiyo niulize.”
“Kwani bado unaendelea kuwa na mahusiano na Monalisa?” aliuliza Happy swali ambalo lilimchukua muda Richard kuweza kulijibu.
“Hapana sipo naye,” alijibu Richard baada ya kumaliza kutafakar.
Richard hakuona sababu ya kumueleza ukweli Happy, aliamua kumficha lakini moyo wake bado ulizidi kuumia, alimpenda sana Evelyne, hakuwa tayari kumpoteza.
****
Wakati wa mawazo bado uliendelea kumtawala, alipokuwa nyumbani kwao usiku aliuona kuwa mrefu, kichwa chake kiliendelea kimfikiria mpenzi wake ambaye mpaka kufikia muda huo alikataa kumsamehe.
Aliwaza kumnunulia zawadi kama gari, kumpangishia nyumba kama ishara ya kumuomba msamaha lakini alipokumbuka uzito wa kosa alilokuwa amelifanya aliona zawadi hizo zisingeweza kufidia maumivu ambayo alikuwa amempa mpenzi wake.
Wakati akiendelea kuwaza hayo aliamua kuichukua simu yake kisha akaamua kumtumia ujumbe Evelyne, ujumbe huo uliweza kujibiwa kwa haraka sana.
“Mambo mpenzi.”
“Sorry nachat na nani?”
“Ina maana namba yangu umeifuta?”
“Hujajibu swali, nimekuuliza nachat na nani?”
“Mimi Richard.”
“Nikusaidie nini?”
“Evelyne mpenzi wangu mbona hivyo?”
“Umesahau nini tena kwangu.”
“Sijasahau kitu ila naomba unisamehe mpenzi.”
“Nimeshakusamehe tangu siku ya kwanza uliyonipa maumivu ila kurudiana na wewe siwezi.”
“Kwanini?”
“Endelea na Monalisa nadhani yeye ndiye anayeweza kuliziba pengo langu kwako.”
Kila ujumbe aliyokuwa akitumiwa na Evelyne alipousoma ulizidi kumuumiza sana, alitamani mpenzi wake asahau mambo yote yaliyotokea kisha amsamehe lakini tukio hilo lilikuwa gumu mno kutokea.

Je,ni nini kitaendelea?
 
NISAMEHE MPENZI-11
Mtunzi:Juma Hiza
0712988278

ILIPOISHIA...

Kila ujumbe aliyokuwa akitumiwa na Evelyne alipousoma ulizidi kumuumiza sana, alitamani mpenzi wake asahau mambo yote yaliyotokea kisha amsamehe lakini tukio hilo lilikuwa gumu mno kutokea.

SONGA NAYO...

Siku zilizidi kukatika huku moyo wa Evelyne ukiendelea kuhifadhi chuki kwa Richard, hakutaka kumsamehe kirahisi kama Richard alivyokuwa akihitaji.
Maisha ya chuo yaliendelea huku maelewano kati yake na Richard yakiwa bado sio mazuri, wafikia kipindi wakawa hawazungumzi lolote zaidi ya salamu ambayo muda mwingine haikuweza kujibiwa. Hilo lilizidi kumuumiza sana Richard, kila siku alikuwa ni mtu wa kulilia penzi la Evelyne bila mafanikio yoyote.
Moyo wake uliendelea kumpenda Evelyne lakini kwa upande mwingine penzi la Monalisa lilizidi kuwa kikwazo, alitamani kuwa mbali na msichana huyo lakini alionekana kuwa na nguvu kubwa ya kuendelea kuwa naye.
Kichwa chake kilizidi kutafakari mambo mengi sana juu ya msichana huyo ambaye alikuwa ndiye sumu ya penzi lake, alizikumbuka picha ambazo alikuwazo na ndizo zilizokuwa zikimfanya akose maamuzi ya kumpenda msichana mmoja.
Alichowaza kukifanya ni kumpigia simu Monalisa kisha akamwambia kuwa siku hiyo alihitaji kuonana naye kwani alikuwa ana mazungumzo naye ya umuhimu sana, alimwambia muda ambao alihitaji kuonana naye kisha wakapanga kukutana katika hoteli ya kifahari ya Golden Tulip.
muda wa kukutana ulipofika waliweza kukutana na kuyaanza mazungumzo yao.
“Sitaki niendelee kukudanganya.”
“Kwanini?”
“Umeulazimisha moyo wangu ukupende lakini hisia zangu hazipo kwako.”
“Una maanisha nini Richard?”
“Hisia zangu zipo kwa msichana mwingine, moyo wangu unampenda msichana mmoja tu na si mwingine bali ni Evelyne.”
“Richard umeshachelewa.”
“Kivipi?”
“Nina ujauzito wako Richard hivyo usijidanganye kuwa unaweza ukaniacha kirahisi.”
“Unasemaje?”
“Natembea na damu yako.”
Yalikuwa ni mazungumzo mafupi yaliyofanyika ndani ya chumba cha kifahari cha hoteli hiyo, Richard hakutaka kuamini aliposikia kuwa Monalisa alikuwa amebeba ujauzito wake, ilikuwa ni taarifa ya ghafla! ambayo ilimshtua sana, moyo wake haukumpenda hata kidogo msichana huyo na kwa wakati huo alikuwa tayari ameshaubeba ujauzito wake, hilo lilizidi kumchanganya.
“Umebebaje ujauzito lakini?” aliuliza Richard kwa ghadhabu.
“Kwani ukiingia unaingiaje inamaana umesahau jinsi ulivyokuwa umelala na mimi?” alijibu Monalisa.
Richard alishikwa na kigugumizi mara baada ya kusikia maneno hayo kutoka kwa msichana huyo, hakutaka kumuamini alihisi labda alikuwa akimdanganya ili asiweze kumuacha lakini kitu cha kushangaza Monalisa alipoona Richard hamuamini aliamua kutoa cheti cha majibu ya dakatri ambayo yalikuwa yakimuonyesha kweli kuwa ni mjamzito.
****
Mapenzi yaligeuka kuwa mwiba wa maumivu kwa upande wa Evelyne, licha ya moyo wake kumpenda Richard lakini mwanaume huyo tayari alikuwa ameshamsaliti, hilo liliendelea kuwa tukio lililozidi kumuumiza sana, alikosa raha ya maisha, alishindwa kusoma, ulimwengu wa mapenzi alichukia.
Maumivu ya kimapenzi hayakuishia kwa kusalitiwa tu bali alizidi kuumia mara baada ya kusikia kuwa Monalisa alikuwa amebeba ujauzito wa Richard na ujauzito huo ndiyo ulizidi kumfanya azidi kumchukia mwanaume huyo.
“Sidhani kama nitakuja kupenda tena katika maisha yangu,” alisema Evelyne huku akijiapiza.
“Usiusemee moyo huwezi kujua nini kitakachotokea baadae,” alisema Happy.
“Sijui Happy kama nitapenda tena moyo wangu unakidonda na sijui kama kitapona na hata kama kikipona bado kitaniachia jeraha la maisha,” alisema Evelyne huku machozi yakianza kumdondoka.
Kipindi ambacho moyo wa Evelyne uliweza kupata maumivu ya kimapenzi, alijikuta akiwa ni mpenzi wa kuperuzi mtandao wa kijamii wa Instagram, aliuamini mtandao huo na ndiyo ambao uliweza kumsahaulisha maumivu yote ya kimapenzi ambayo moyo wake ulikuwa umeyapata.
Ndani ya mtandao huo wa Instagram katika kipindi asichokitarajia alikutana na mvulana aliyejulikana kwa jina la Fredick na kama utani alijikuta akianzisha urafiki na mwanaume huyo na baadae urafiki huo uliweza kuibua penzi kati yao.
Aliendelea na masomo yake ya chuo huku penzi hilo jipya likionekana kumbadilisha kwa kiasi fulani, hakuonekana kuwa mtu wa kuumizwa tena na mapenzi, moyo wake tayari ulikuwa umepata tumaini lingine, alimpenda sana Fedrick kwake mwanaume huyo alimuona kuwa sawa na malaika ambaye alikuja kipindi asichokitarajia.
****
Richard hakuwa tayari kuona Monalisa anaendelea kuubeba ujauzito, alichoamua kukifanya ni kumshauri autoe ujauzio huo lakini hilo lilikuwa ni jambo gumu mno kuweza kufanyika, Monalisa hakuwa tayari kufanya kitendo hicho.
Alizidi kuchanganyikiwa baada ya kusikia kuwa Evelyne alikuwa ameshampata mwanaume mwingine, hakutaka kuamini ilibidi atafute nafasi ya kuzungumza na msichana huyo ambaye moyo wake ulikuwa bado unampenda sana.
"Naomba uniache na maisha yangu," alisema Evelyne.
“Siwezi kufanya hivyo hata mara moja nakupenda Evelyne," alisema Richard.
“Upendo wako hauna faida tena kwangu."
“Kwanini unasema hivyo kwanini unauumiza moyo wangu?"
“Siamini kama kweli ninauumiza moyo wako ila jaribu kuchunguza sababu ya maumivu yako."
“Evelyne nataka urudi kuwa wangu."
“Kwasasa haitawezekana kwasababu moyo wangu anaumiliki mwanaume mwingine."
“Yupi."
“Fredrick.”
“Hapana Evelyne, Hapana."
“Huo ndiyo ukweli."
“Nakupenda Evelyne."
“Nilikupenda Richard," alisema Evelyne kisha akaondoka eneo hilo.

Je, nini kitaendelea?
 
NISAMEHE MPENZI-12
Mtunzi:Juma Hiza
0712988278

ILIPOISHIA......

“Naomba uniache na maisha yangu,” alisema Evelyne.
“Siwezi kufanya hivyo hata mara moja nakupenda Evelyne,” alisema Richard.
“Upendo wako hauna faida tena kwangu.”
“Kwanini unasema hivyo kwanini unauumiza moyo wangu?”
“Siamini kama kweli ninauumiza moyo wako ila jaribu kuchunguza sababu ya maumivu yako.”
“Evelyne nataka urudi kuwa wangu.”
“Kwasasa haitawezekana kwasababu moyo wangu anaumiliki mwanaume mwingine.”
“Yupi.”
“Fredrick.”
“Hapana Evelyne, Hapana.”
“Huo ndiyo ukweli.”
“Nakupenda Evelyne.”
“Nilikupenda Richard,” alisema Evelyne kisha akaondoka eneo hilo.

SONGA NAYO....

Moyo wa Evelyne ulihamisha mapenzi kutoka kwa Richard kwenda kwa mwanaume mwingine ambaye alikuwa ni Fredrick, hakutaka kusikia lolote kutoka kwa mwanaume huyo ambaye alizidi kuiteka akili yake, alimuona kuwa kama Malaika ambaye alishushwa kwa ajili ya kumfariji kwa maumivu aliyokuwa ameyapata.
Mpaka kufikia kipindi hicho alikuwa bado hajaonana na Fredrick, aliishia kumuona kwenye mtandao wa Intagram na kuwasiliana naye kwenye simu, muda mwingine walikuwa wakitumiana picha WhatsApp.
Fredrick alikuwa akiishi Daresalaam maeneo ya Tabata Segerea lakini pia alikuwa ni mfanyakazi katika kampuni moja binafsi iliyokuwa ikijihusisha na mambo ya Bima.
Alizidi kuiteka akili ya Evelyne bila kujijua na kila siku penzi lao lilizidi kuota mizizi. Katika moyo wa Evelyne hakukuwa na nafasi ya mwanaume mwingine zaidi ya Fredrick mwanaume ambaye alitokea kumpenda bila kujua sababu.
“Nitakuona lini mpenzi?”
“Usijali utaniona tu.”
“Lini?”
“Wikiendi hii.”
“Kweli?”
“Ndiyo uhakika.”
“Nitafurahi bebi.”
“Hata mimi nitafurahi pia.”
“Kwanini?”
“Kwasababu nitakuona kiuhalisia, nitaushuhudia uzuri wako kwa macho lakini pia nitapata nafasi ya kukushika.”
“Nakupenda Fredrick natamani hata kesho nikuone jamani.”
“Usijali tumuombe Mungu atufikishe salama Jumamosi hii tuonane.”
“Ameen.”
Walimaliza kuzungumza kwenye simu huku kila mmoja wao akionekana kutawaliwa na furaha kwa kuzungumza na mwenzake. Walipanga wikiendi ya wiki hiyo wakutane na ndiyo ilikuwa siku yao ya kwanza ambayo walikuwa wanaenda kuonana tangu walipoanzisha mahusiano yao ya kimapenzi mtandaoni.
Japo hawakuwahi kuonana lakini walipendana sana, walifarijiana, walishauriana, waliahidiana mambo mengi sana kama wapenzi. Picha za Fredrick alizomtumia Evelyne pamoja na sauti yake ya upole iliyosanjari na maneno yake ya faraja yalitosha kabisa kumteka Evelyne, kila alipokuwa akizitazama picha za mwanaume huyo aliona alikuwa na kila sababu ya kumpenda.
“Kwahiyo Richard hana lake tena?” aliuliza Happy.
“Ndiyo naweza kusema hivyo,” alijibu Evelyne.
“Lakini kwanini umeshindwa kumsamehe huoni kama utakuwa umemuhukumu bure?” aliuliza Happy.
“Nimeshamsamehe lakini siwezi kurudiana naye,” alijibu Evelyne.
“Huyo Fredrick atakusaidia nini, kwanini usirudiane na Richard ambaye umetoka naye mbali na amekiri makosa yake?”
“Siwezi Happy.”
“Mapenzi ya mtandaoni hayadumu, huyo Fredrick atakuchezea mwisho wa siku akuache.”
“Siamini kama anaweza kunifanyia hivyo.”
“Kwani umeshaonana naye?”
“Hapana ila wikiendi hii nakwenda kuonana naye.”
“Unamjua?”
“Ndiyo amenitumia picha zake.”
“Unaamini vipi kuwa ndiyo yeye je, kama amekudanganya?”
“Ndiyo yeye nina uhakika.”
“Kuwa makini,” alisema Happy.
Licha ya mambo yote yaliyokuwa yametokea lakini bado Happy alitamani Evelyne arudiane na Richard, hakutaka kuona wawili hao wakitengana, mwanzoni alihisi labda zilikuwa ni hasira za Evelyne na mwisho wa siku zingeisha na kuweza kurudiana na mpenzi wake lakini hilo halikuweza kutokea. Evelyne alikuwa tayari ameanzisha mahusiano na mwanaume mwingine.
Hatimaye siku ya Jumamosi iliweza kufika, Fredrick alimpigia simu Evelyne na kumwambia kuwa siku hiyo walitakiwa kuonana nyumbani kwake, Evelyne hakutaka kuamini siku hiyo alikuwa anaenda kuonana na mwanaume aliyekuwa anampenda.
Hakutaka kupoteza muda alijiandaa haraka, alipomaliza kujiandaa safari ya kuelekea Tabata Segerea akaianza. Moyo wake ulikuwa na furaha muda wote kila alipomkumbuka Fredrick, katika mawazo yake aliunda taswira ya Fredrick ambaye alikuwa akizungumza. Mapigo ya moyo wake yalikuwa yanamuenda mbio, hakutaka kuamini hata kidogo kama alikuwa anaenda kukutana na mwanaume huyo.
Baada ya kupita dakika arobaini alikuwa tayari ameshafika Tabata Segerea, alimpigia simu Fredrick kumjulisha kuwa tayari alikuwa ameshafika, haikuchukua dakika chache Fredrick aliweza kufika, walipoonana kwa mara ya kwanza walikumbatiana, Evelyne hakuamini macho yake kama aliweza kumuona Fredrick mwanaume ambaye aliishia kumuona Instagram na kuzungumza naye kwenye simu. Ilikuwa ni zaidi ya furaha kwa wawili hao kuweza kukutana.
Fredrick alimpeleka Evelyne nyumbani kwake alipokuwa anaishi, siku hiyo Evelyne kila kitu alichokuwa akikiona kwa Fredrick kiliweza kumshangaza, licha ya umri mdogo aliyokuwa nao mwanaume huyo lakini alikuwa tayari ameshajipanga kimaisha.
“Hapa ni kwako?” aliuliza Evelyne alipoingia nyumbani kwa Fredrick.
“Hapana ni kwako pia,” alijibu Fredrick huku akimtazama Evelyne ambaye kwa muda huo alikuwa akitazama samani zilizokuwa ndani ya nyumba hiyo.
Fredrick hakutaka kumuacha Evelyne aendelee kumuuliza maswali mengi kwa wakati huo, alichoamua kukifanya ni kumuuliza aina ya kinywaji ambacho alikuwa anatumia baada ya kuketi katika sofa.
“Unatumia Juisi, maziwa au soda?” aliuliza Fredrick huku akimtazama Evelyne.
“Niletee chochote,” alijibu Evelyne kwa sauti ya aibu.
“Ndiyo maana nikakutajia inabidi uchague kimoja wapo hapo,” alisema Fredrick.
“Ok basi niletee juisi.”
“Unapenda ya tunda gani?”
“Lolote lile mimi natumia,” alijibu Evelyne kisha Fredrick akaenda kumletea.
Evelyne hakutaka kuamini kama kweli mwanaume huyo alikuwa peke yake siku zote hizo, huo ulikuwa ni wasiwasi uliyoanza kumuingia mara baada ya kuyaona mazingira ya nyumba hiyo jinsi yalivyokuwa mazuri.
“Karibu,” alisema Fredrick baada ya kurudi, mikononi alikuwa amebeba glass mbili, moja ilikuwa ni ya juisi na nyingine ilikuwa ni ya maziwa. Alipomkaribia Evelyne alimpatia ile glass ya juisi halafu na yeye akaketi pembeni yake, mkononi alikuwa amebakiwa na glass ya maziwa. Wakaanza kunywa taratibu huku wakitazamana kwa macho ya kuibianaibiana.
“Nikuulize kitu?” aliuliza Evelyne.
“Ndiyo niulize,” alijibu Fredrick.
“Kwani unaishi na nani hapa?”
“Mwenyewe.”
“Una uhakika?”
“Ndiyo.”
“Hauna mwanamke mwingine kweli?”
“Atokee wapi wakati tayari nipo na wewe.”
“Fredrick niambie ukweli usinidanganye.”
“Niamini upo peke yako katika moyo wangu,” alisema Fredrick.
Kila maneno aliyokuwa akiyasema Fredrick yalizidi kumteka Evelyne, alijikuta akikosa la kusema, alibaki akimtazama mwanaume huyo ambaye alitofautiana mambo mengi sana na Richard.
****
Monalisa hakuishia kumpenda Richard pale chuoni, kila mwanaume mwenye pesa na muonekano mzuri ambaye alijitokeza mbele yake alikuwa akianzisha mahusiano naye na hiyo ndiyo ilikuwa tabia yake. Hakukuwa na watu waliyokuwa wakifahamu hilo zaidi ya marafiki zake Penina, Adela pamoja na Mary.
Tabia yake hiyo ya kuwachanganya wanaume ndiyo iliyosababisha mpaka akapata mimba ambayo hakuwa anamfahamu baba halisi, hakuwa na njia nyingine ya kufanya zaidi ya kumsingizia mimba hiyo Richard mwanaume ambaye tayari alikuwa ameshafanya naye mapenzi.
Richard baada ya kupewa taarifa hizo za ujauzito hakutaka kukataa, alikubali huku akiamini ulikuwa ni ujauzito wake.

Je, ni nini kitaendelea?
 
NISAMEHE MPENZI-13
Mtunzi:Juma Hiza
0712988278

ILIPOISHIA.....

Tabia yake hiyo ya kuwachanganya wanaume ndiyo iliyosababisha mpaka akapata mimba ambayo hakuwa anamfahamu baba halisi, hakuwa na njia nyingine ya kufanya zaidi ya msingizia mimba hiyo Richard mwanaume ambaye tayari alikuwa ameshafanya naye mapenzi.
Richard baada ya kupewa taarifa hizo za ujauzito hakutaka kukataa, alikubali huku akiamini ulikuwa ni ujauzito wake.

SONGA NAYO.....

Hakutaka kuamini kama kweli alikuwa amempa ujauzito msichana huyo ambaye moyo wake haukumpenda, alizidi kujilaumu mno baada ya kukumbuka kuwa msichana huyo ndiye alikuwa sababu ya kumgombanisha na mpenzi wake na kwa wakati huo tayari alikuwa ameanzisha mahusiano na mwanaume mwingine.
Tukio hilo bado liliendelea kumuumiza sana moyo wake, hakutaka kuamini kile kilichokuwa kimetokea, alihisi alikuwa katika ndoto lakini haikuwa hivyo, kila kitu kilichokuwa kimetokea ndiyo ulikuwa ukweli halisi.
Alitamani kuwaeleza ukweli wazazi wake kwa kile kilichokuwa kimetokea kuhusu Monalisa mpaka kufikia hatua ya kumpa ujauzito lakini alipokumbuka maswali ambayo angeweza kuulizwa na Mama yake kuhusu Evelyne alighairi kufanya hivyo.
Alipokuwa akimuona Monalisa chuoni moyo wake ulizidi kumchukia, alimuona kuwa msichana aliyeyaharibu mahusiano yake na mpenzi wake, kitu kibaya zaidi alikuwa ameubeba ujauzito wake na hilo ndilo lilizidi kumchanganya akili yake bila kujua kuwa alisingiziwa ujauzito huo haukuwa ni wake.
****
Penzi kati ya Fredrick na Evelyne lilizidi kupamba moto, hakukuwa na tatizo lolote kati yao, tangu walipoweza kukutana siku ya kwanza mapenzi yao yalizidi kuongezeka.
Fredrick alikuwa ni mwanaume wa tofauti sana, alifanya kila awezalo ilimradi ahakikishe msichana huyo anapata furaha, hakutaka kuona anakuwa sababu ya kumuumiza bila sababu, hakutaka kuona tukio hilo linatokea hata mara moja, alihakikisha anamtimizia kila kitu alichokuwa akikihitaji katika mapenzi, hata hivyo mbali na yote hayo ndoto yake kubwa ilikuwa ni siku moja kuja kufunga pingu za maisha na msichana huyo pale pindi ambapo angeweza kumaliza chuo na kufanikiwa kupata kazi.
Evelyne alizidi kutekwa na mapenzi ya Fredrick, muda wote furaha ndiyo ilikuwa imemtawala, hakuona sababu ya kuyachukia tena mapenzi, aliyapenda na moyo wake ulikuwa ukimpenda Fredrick tu.
“Una nini wewe mbona unacheka mwenyewe?” aliuliza Happy.
“Hakuna kitu,” alijibu Evelyne.
“Umeanza kuchanganyikiwa?”
“Hapana kuna kitu nimekikumbuka ndiyo kimefanya nimecheka.”
“Kitu gani?”
“Ni kuhusu Fredrick.”
“Mwenzetu ndiyo tayari umeshakolea kiasi hicho?”
“Yeah! nampenda sana na ninaimani hata yeye pia ananipenda.”
“Unajua siku hizi umebadilika sana tofauti na siku zote.”
“Nimekuwaje?”
“Umekuwa ni mtu wa kufurahi tu kila wakati.”
“Nimeipata furaha, nimeipata amani sasa kwanini nisifurahie?”
“Kweli huyo mwanaume amekuteka,” alijibu Happy.
****
Adela alifahamu kila kitu kilichokuwa kikiendelea katika maisha ya Monalisa, hakuipenda tabia ya rafiki yake huyo ambaye kila mwanaume mwenye pesa na muonekano mzuri aliyejitokeza mbele yake alikuwa akianzisha mahusiano naye. Alikuwa ametembea na wanaume wengi sana na mpaka kufikia wakati huo alikuwa amepata ujauzito na hakujua ulikuwa ni wa nani zaidi alichoamua kukifanya nikumsingizia Richard kwa kuwa tayari alikuwa ameshalala naye, alihitaji kutumia pesa zake.
Alichoamua kukifanya Adela ni kutafuta muda wa kukutana na Richard kisha akahitaji kumueleza kila kitu kilichokuwa kikiendelea.
“Kuna nini?” aliuliza Richard.
“Nahitaji kuzungumza na wewe,” alijibu Adela.
“Ni mazungumzo ya umuhimu?” aliuliza Richard.
“Ndiyo ni muhimu sana,” alijibu Adela.
Baada ya kujibiwa hivyo Richard hakutaka kupoteza muda alichoamua kukifanya ni kumpa nafasi msichana huyo ya kumsikiliza kile alichokuwa amedhamiria kumwambia kwa wakati huo.
“Ok, nakusikiliza niambie,” alisema Richard.
“Richard najua unatembea na rafiki yangu, hilo sio jambo la siri tena ila kuna kitu kimoja nahisi haukifahamu na kinaniumiza sana,” alisema Adela.
“Kitu gani?” aliuliza Richard.
“Monalisa hakupendi isipokuwa amekutamani, tamaa zake za kimwili ndiyo zimempelekea mpaka akakuharibia mahusiano yako,” alijibu Adela huku akionyesha msisitizo wa maneno yake.
“Mbona sijakuelewa ni nini unachokimaanisha?” aliuliza Richard.
“Monalisa sio msichana sahihi kwako, hastahili kuwa mpenzi wako ni muuaji yule,” alijibu Adela.
“Bado sijakuelewa.”
“Ninachotaka kukuambia ni kwamba ule ujauzito wa Monalisa sio wako,” alisema Adela.
Maneno hayo yalimchanganya sana Richard, alishindwa kuelewa ukweli wa maneno yale, kama ule haukuwa ujauzito wake ulikuwa ni wa nani. Hili ndilo lilikuwa swali pekee lililokuwa linamuumiza kichwa chake, hakujua nyuma ya pazia kama alishiriki mapenzi na msichana ambaye kwake kitendo cha kuwabadilisha wanaume kama nguo kilikuwa ni cha kawaida.
“Unasemaje?” aliuliza kwa mshangao.
“Huo ndiyo ukweli,” alijibu Adela lakini kama haitoshi aliamua kumsimulia kila kitu kilichokuwa kikiendelea nyuma ya pazia.
****
Taarifa za ujauzito wa Monalisa zilisambaa kila sehemu, hatimaye chuo kizima kilifahamu kuhusu habari hizo, hakukuwa na siri juu ya uhusiano wake na Richard, kila mtu alifahamu kuhusu habari za wawili hao. Waliyomfahamu Richard walimlaumu sana kwa kitendo alichokuwa amekifanya cha kumsaliti mpenzi wake kisha akaanzisha mahusiano na msichana mwingine ambaye tayari alikuwa amembebesha ujauzito. Jambo hilo lilizidi kumfanya achukiwe na baadhi ya watu.
“Jamaa karuka mkojo kakanyaga mavi,” alisema mwanachuo mmoja.
“Hili ndilo tatizo letu sisi wanaume hatuwezi kutulia na msichana mmoja,” alisema mwanachuo mwingine.
Hakukuwa na kitu kilichokuwa kikiwakasirisha watu kama kusikia kuwa msichana huyo aliyelisambaratisha penzi la Evelyne alikuwa amebeba ujauzito.
Baada ya kuzisikia taarifa hizo Happy na yeye alianza kumchukia Richard, hakutaka kuzungumza naye, aliamua kuwa upande wa rafiki yake na kuanzia siku hiyo alimuunga mkono kwa uamuzi aliyokuwa ameuchukua wa kuanzisha mahusiano na Fredrick.
Alifahamu ni maumivu kiasi gani aliyokuwa ameyapata hivyo kwa uamuzi aliyokuwa ameuchukua aliamini uliweza kumpunguzia maumivu hayo.
“Yaani pamoja na uchafu aliyoufanya ameona haitoshi ameamua bora ampe ujauzito kabisa,” alisema Happy.
“Wanaume ndivyo walivyo hawaridhiki,” alisema Evelyne.
“Nimemchukia sana.”
“Sio wewe tu hata mimi sitaki kuzungumza naye,” alisema Evelyne.
Mpaka kufikia hapo hakukuwa na mtu aliyefahamu ni nini kilichokuwa kikiendelea, wanachuo walimchukia sana Richard kwa ujinga aliyokuwa ameufanya wa kumsaliti mpenzi wake.
Ilikuwa imebakia miezi miwili ili waweze kufanya mitihani ya kumaliza degree yao, kila mwanachuo alionekana kuwa bize na kusoma kwa ajili ya kujiandaa na mitihani hiyo.
Kwa upande wa Richard hali ilikuwa tofauti, alijitahidi kujisomea lakini badala ya kuelewa alichokuwa akikisoma ndiyo kwanza mawazo yake yalikuwa yakitafakari ukweli aliyoelezwa na Adela kuhusu ujauzito wa Monalisa.

Je, ni nini kitaendelea?
 
NISAMEHE MPENZI-14
Mtunzi:Juma Hiza
0712988278

Ilikuwa imebakia miezi miwili ili waweze kufanya mitihani ya kumaliza degree yao, kila mwanachuo alionekana kuwa bize na kusoma kwa ajili ya kujiandaa na mitihani hiyo.
Kwa upande wa Richard hali ilikuwa tofauti, alijitahidi kujisomea lakini badala ya kuelewa alichokuwa akikisoma ndiyo kwanza mawazo yake yalikuwa yakitafakari ukweli aliyoelezwa na Adela kuhusu ujauzito wa Monalisa. Alihisi kuchanganyikiwa kila alipokuwa akiyakumbuka maneno ya Adela, alitumia pesa nyingi mno kwa ajili ya Monalisa, hakutaka kuamini kama msichana huyo aliyedai kuwa anaujauzito wake hakuwa muaminifu, alishiriki mapenzi na wanaume wengi na mpaka kufikia wakati huo ujauzito haukuwa ni wake. Hilo liliendelea kumuumiza sana moyo wake, alijiona kuwa mwanaume mwenye mikosi kila kukicha.
****
Mwezi wa kwanza ulikatika huku wanachuo wakiendelea kujiandaa na mitihani yao, mwezi wa pili nao ukakatika, hatimaye wiki ya kwanza ya mitihani ikaanza. Wanachuo wakaanza kuifanya mitihani yao ambayo iliwachukua takribani mwezi mzima kuweza kuimaliza.
Ilikuwa ni furaha kwa kila mwanachuo kuweza kumaliza salama mitihani hiyo, kila mwanachuo alimshukuru Mwenyezi Mungu kutokana na hatua waliyokuwa wameifikia. Kama kawaida pia hawakuacha kupongezana, sherehe mbalimbali ziliandaliwa kama ishara ya kupongezana kwa kufanikiwa kumaliza masomo yao.
Wiki moja baadaye Richard aliamua kumueleza ukweli Monalisa juu ya taarifa alizozisikia kuhusu ujauzito kuwa haukuwa ni wake, alipokuwa akimueleza hayo macho yake yalikuwa yakitoa machozi. Alishindwa kuyavumilia maumivu ambayo moyo wake ulikuwa ukipitia.
Monalisa alibaki kinywa wazi baada ya kusikia maneno hayo kutoka kwa Richard, hakutaka kuamini kama alifahamu kila kitu kilichokuwa kikiendelea, siri ambayo aliamini ilikuwa ni vigumu kufichuka kwa wakati huo ilikuwa tayari imeshafichuka. Swali ambalo alianza kujiuliza ni rafiki yake gani ambaye alimgeuka na kumueleza Richard kila kitu, hakupata jibu hata alipoamua kumuuliza Richard hakuwa tayari kumuweka wazi. Hilo lilizidi kumshangaza sana, alichanganyikiwa, hakutaka kuamini kama alikuwa ameshagundulika.
“Sidhani kama nitakuwa ninanafasi ya kuendelea kuwa na wewe, naomba huu ndiyo uwe mwisho wetu, umeniharibia mahusiano yangu vya kutosha, please naomba uniache, niache Mona na maisha yangu,” alisema Richard kwa sauti ya uchungu, machozi yalikuwa yakimbubujika.
“Hapana Richard usiseme hivyo, nakupenda, nakupenda tena sana na ndiyo maana nimefanya yote haya kwasababu yako, sikutaka nikupoteze kirahisi kiasi hiki. Richard ni kweli huu ujauzito sio wako lakini naomba unisamehe bado naamini nina nafasi ya kufanya kitu kwa ajili yako,” alisema Monalisa.
Kila alipokuwa akimtazama Richard alivyokuwa akilia mbele yake alijisikia vibaya mno, alimkosea sana, alimfanyia kila aina ya uhuni, alimchanganya na wanaume wengi sana ambao alikuwa akitembea nao kwa ajili ya kuwachuna, hakuwa na mapenzi ya dhati, huo ndiyo ulikuwa ukweli lakini alipogundua kuwa siri hiyo ilifichuka alizidi kujisikia vibaya.
Hakuwa na kitu kingine cha kufanya zaidi ya kumuomba msamaha na kumuahidi kufanya kitu kwa ajili yake, licha ya mambo yote aliyokuwa ambayo alikuwa amemfanyia lakini hakutaka kuona akimpoteza mwanaume huyo, aliendelea kuushikilia msimamo wa kumpenda zaidi ya kila kitu katika dunia hii.
Richard alipomuona Monalisa mbele yake pamoja na maneno ambayo alikuwa akiyazungumza yalizidi kumuweka katika wakati wa hasira mno, alimuona kuwa adui mkubwa sana wa maisha yake, alimchukia mno.
“Sijui nikuambie nini mpenzi?”
“Usiniambie kitu, sitaki kusikia lolote kutoka kwako ni bora uendelee kukaa kimya.” “Hapana Richard usiseme hivyo utazidi kuumiza moyo wangu.”
“Mona kwa uliyonifanyia inatosha, nashindwa kuvumilia, moyo wangu haukuhitaji.”
“Richard hunipendi?”
“Ndiyo sikupendi Mona,” alijibu Richard.
Monalisa alizidi kuchanganyikiwa baada ya kuyasikia majibu hayo, hakutaka kukubaliana na ukweli wa kile kilichokuwa kimetokea. Alijitahidi sana kumbembeleza, muda mwingine alikuwa akimlilia lakini yote hayo bado hayakuweza kuwa sababu iliyomfanya Richard akubali kuendelea kuwa naye. Alimpenda sana mwanaume huyo, alitamani kumuona kila wakati akiwa naye. Baada ya kuona Richard ameshindwa kumsamehe uamuzi ambao ulimjia kichwani mwake ni wa kuutoa ujauzito huo, aliamini ujauzito huo ndiyo ulikuwa sababu ya yeye kuchukiwa na Richard.
Hakutaka kupoteza muda haraka alipanga mipango ya kuutoa na hatimaye aliweza kufanikiwa katika hilo. Furaha ilizidi kumtawala, aliamini huo ndiyo ulikuwa muda wake muafaka wa kuweza kumuomba msamaha Richard kisha akaweza kumsamehe, hilo lilikuwa ni jambo gumu mno kwa Richard kuweza kutokea licha ya msichana huyo kuwa ni mzuri.
****
Baada ya kupita miezi kadhaa hatimaye Evelyne pamoja na Happy walifanikiwa kuajiriwa katika moja ya kampuni iliyokuwa ikiwalipa wazuri. Richard na yeye kutokana na utajiri aliyokuwanao baba yake aliweza kuachiwa kampuni aiongoze na kwa upande wa Monalisa pamoja na marafiki zake na wao pia walifanikiwa kuajiriwa katika kampuni nyingine hapa mjini.
****
Fredrick aliamua kujitambulisha kwa wazazi wake Evelyne pamoja na kumtambulisha mpenzi wake, hakutaka kufanya utani hata mara moja, baada ya kufuata taratibu zote aliamua kumvalisha pete ya uchumba na baadae kufunga naye ndoa kabisa.
Evelyne hakuamini kama aliweza kupata mwanaume ambaye alimpenda na kumthamini kiasi kile, alizidi kumpenda sana mwanaume huyo ambaye kila kitu alichokuwa akikifanya hapa duniani alikifanya kwa sababu ya mapenzi yake. Taarifa hizo za Evelyne kuolewa na Fredrick ziliweza kumfikia Richard, alipoambiwa kwa mara ya kwanza mapigo ya moyo wake yalimuenda mbio, hakutaka kuamini, alihisi kutaniwa. Alibaki katika simanzi baada ya kuthibitisha ukweli wa taarifa hizo, zilizidi kumuumiza mno moyo wake.
Kila alipomkumbuka Evelyne wakati alipokuwa ofisini machozi yalikuwa yakimbubujika muda wote, taswira ya msichana huyo ikajijenga upya akilini mwake, akaanza kumuwaza kwa kifupi alishindwa kufanya kazi kabisa siku hiyo.

Je, ni nini kitaendelea?
 
NISAMEHE MPENZI:15
Mtunzi:Juma Hiza
0712988278

Hisia za mapenzi bado ziliendelea kumuumiza, kichwa chake kilikataa kabisa kumsahau Evelyne.
Muonekano wake mzuri uliendelea kuwatesa wasichana waliyokuwa katika kampuni yake hiyo, wote walimtetemekea. Kama kulikuwa kuna uwezekano wa kutokea walau siku moja kila moyo wa msichana katika kampuni hiyo kusema chochote, hakika sauti za maombi ya kumuhitaji Richard ndiyo zingesikika ndani ya ofisi nzima, hakukuwa na msichana ambaye alipomuona Richard moyo wake haukuacha kushtuka, ulimuhitaji mno mwanaume huyo.
Kama kawaida maneno na mabifu ya chinichini hayakuacha kuwepo kwa wasichana hao, walijikuta wakiingia katika ugomvi na chuki kila wakati, sababu ikiwa ni Richard. Msichana aliyepata bahati ya kutolewa lunch na Richard aliitumia nafasi hiyo katika kuwaumiza roho wafanyakazi wenzake, hilo lilizidi kutengeneza chuki kati yao.
Licha ya kuwepo na mambo yote hayo ofisini lakini hakukuwa na msichana aliyebahatika kuumiliki moyo wa Richard, kila siku waliishia kumpelekea zawadi na mialiko mingi ambayo haikuweza kuzaa matunda yoyote.
"Ni Mzuri ndiyo tena anavutia mno ila sijakuelewa kwani nini unachokitaka hasa kwa Boss?" Aliuliza msichana mmoja.
"Sijui niseme nini, sijui nianzie wapi kukuelezea ila kwa kifupi nampenda sana, natamani siku moja ajue ni jinsi gani moyo wangu unavyomuhitaji," alijibu msichana mwingine ambaye alizungumza kwa hisia.
Kitendo cha wasichana kuamini siku moja kufanikiwa kulimiliki penzi la Richard kilibaki kuwa ndoto, ulikuwa ni ukweli uliyowaumiza mno.
Maisha ya Richard yalikuwa mazuri kwa upande wake lakini upande mwingine alijiona kukosa bahati, licha ya kuwa alifanikiwa kununua nyumba maeneo ya Mbezi, kumiliki pesa, kutembelea gari la kifahari lakini tukio la kumpoteza Evelyne kilimuacha na pigo kubwa mno.
Alifahamu kwa wakati huo msichana huyo alikuwa ni mke wa mtu lakini bado alijipa matumaini ya kuwa naye siku moja, moyoni hakutaka kukubaliana na ukweli, alijiapiza kufanya lolote ili aweze kulirudisha penzi lake.
"Nitatumia kila nilichonacho, kama ni pesa, nguvu hata kwa kumwaga damu ilimradi urudi kwangu, sikubali na siwezi kuvumilia maumivu na mateso haya ninayoyapata katika moyo wangu," alijisemea Richard alipokuwa nyumbani kwake, wakati huo alikuwa akiitazama picha ya Evelyne kwenye simu. Ilizidi kumuumiza mno.
Alijitahidi kuvumilia, kuficha kwa kipindi kirefu lakini kuna muda uzalendo ulimshinda. Akatamani kuwaeleza wazazi wake ukweli kwani katika kipindi hicho tayari walishaanza kumuuliza kuhusu mipango yake ya kufunga ndoa na Evelyne.
Alihisi kuchanganyikiwa kila alipokuwa akiulizwa kuhusu Evelyne, wazazi wake hawakufahamu kilichokuwa kimetokea hivyo walionekana kumuhitaji sana msichana huyo.
Baada ya kuona wazazi wake wamezidi kumsumbua sana kuhusu suala hilo la kumuoa Evelyne ilibidi awaeleze ukweli wa kilichotokea kati yake na msichana huyo ambaye kwa wakati huo alikuwa ni mke wa mtu, zilikuwa ni taarifa zilizowashtua wazazi wake, hawakutaka kuamini walichokuwa wakiambiwa.
"Umefanya ujinga gani mwanangu?" Aliuliza Mama yake, hakuishia kuuliza swali tu isipokuwa alianza kumlaumu kwa kosa alilokuwa amelifanya hata kwa upande wa baba yake Mzee Gombanila na yeye alimlaumu pia.
Richard alipoona lawama zimezidi kuwa nyingi aliamua kuondoka nyumbani kwao, alipokuwa barabarani kichwa chake bado kilitawaliwa na mawazo mengi sana, hakujua ni kwa jinsi gani angeweza kuyatatua. Kuna kipindi alijikuta akilipa faini kwa kosa la uzembe wake mwenyewe barabarani.
Licha ya kuwa na maisha mazuri, kutamaniwa na wasichana lukuki lakini alipokumbuka yaliyomtokea katika maisha ya kimahusiano hakutaka kumkabidhi msichana mwingine moyo wake, aliogopa mno.
****
Fredrick na Evelyne walizidi kuyafurahia maisha ya ndoa yao, kila wakati furaha iliendelea kushika hatamu, baada ya kupita miezi miwili, siku moja majira ya jioni Fredrick alipokuwa akirudi nyumbani kwake Tabata, alipata ajali mbaya sana maeneo ya Ubungo mataa, gari yake ndogo aina ya Toyota Harrier lenye rangi nyeusi iligongana uso kwa uso na lori.
Ilikuwa ni ajali mbaya sana ambayo kila mtu aliyeishuhudia hakutaka kuamini kama angeweza kupona mtu.
Mwili wa Fredrick haukuweza kutambuliwa kwa haraka kutokana na damu zilizokuwa zimetapakaa kila sehemu, wasamaria waliyojitokeza wakamsaidia kumtoa ndani ya gari hiyo iliyokuwa imebondekabondeka na kupoteza umbo lake la kawaida, walijitahidi kadri ya uwezo wao na hatimaye walifanikiwa kumtoa lakini alikuwa amepoteza fahamu.
Baada ya kupita dakika kadhaa polisi waliweza kufika eneo la tukio, kama ilivyokuwa kawaida yao walianza kuwatawanyisha watu, walihitaji kuona usalama wa eneo hilo ukiendelea kuwepo. Wakati polisi wakiendelea kufanya kazi yao ghafla! Ving'ora vya gari la kubebea wagonjwa (Ambulance) viliweza kusikika na ndani ya dakika chache liliweza kufika eneo la ajali kisha wakamchukua Fredrick ambaye alikuwa katika hali mbaya sana.
Walipomfikisha hospitali taratibu za kuyaokoa maisha yake zilianza kufanyika, wakati huo Evelyne alishapigiwa simu na kwa wakati huo alikuwa njiani akielekea katika hospitali ya Muhimbili, alipofika alionekana kuchanganyikiwa, hakuamini kama Fredrick alikuwa amepata ajali na kwa wakati huo alikuwa katika chumba cha upasuaji akiendelea kupatiwa matibabu.
Baada ya masaa kadhaa kupita, hatimaye majibu yaliweza kutolewa na daktari, kutokana na ajali aliyoipata Fredrick ilimsababishia matatizo katika kizazi chake pamoja na mshtuko aliyoupata ulimpelekea kupooza hivyo katika maisha yake angeshindwa kuamka na kufanya shughuli zake kama ilivyokuwa kawaida na badala yake maisha yake yalibadilika na kuwa ni ya kitandani.

Je, ni nini kitaendelea?
 
NISAMEHE MPENZI:16
Mtunzi:Juma Hiza
0712988278

Fredrick alikuwa amelala kitandani, uso wake ulikuwa umetawaliwa na furaha, alizidi kuonekana kuyafurahia maisha yake.
Alimtazama mke wake ambaye machozi yalikuwa yakimdondoka kwa muda huo, Evelyne kila alipokuwa akimtazama mume wake jinsi alivyokuwa amelala kitandani alihisi maumivu makali mno ndani ya moyo wake. Alimpenda sana mume wake, hakutaka kumuona akiendelea kuteseka, alipanga kufanya kila awezalo ili aweze kuyaokoa maisha yake lakini alipoyakumbuka majibu ya daktari kuwa asingeweza kupona, alizidi kuumia mno.
Hakuna maumivu makali kama kumuona yule umpendae akiteseka kwa ugonjwa katika dunia hii, ni zaidi ya maumivu makali mno.
Machozi yaliendelea kumbubujika Evelyne pale hospitalini, hakutaka kuamini kama mume wake alikuwa amepooza na kibaya zaidi alipoteza uwezo wa kupata mtoto. Hilo liliendelea kumuumiza sana moyo wake.
Ilikuwa imepita miezi kadhaa tangu walipofunga ndoa yao, kabla ya kufika hata mwaka tayari ndoa hiyo ilikuwa imeingiwa na tatizo.
Ndugu wa mume wake walipozipata taarifa za ajali hiyo hawakutaka kuelewa chochote, waliamini ilikuwa ni ajali ya kupangwa na ilisababishwa na Evelyne ambaye walidai alizitamani mali za ndugu yao.
Mwanzo wa maneno na vitisho vikaanzia hapo, hakukuwa kuna ndugu upande wa mume aliyekuwa upande wa Evelyne, wote walimchukia.
Kuna muda Evelyne alikuwa akikufuru Mungu, alihisi kuonewa, hakutaka kuamini kama yeye ndiye alikuwa binadamu mwenye makosa mengi zaidi hapa duniani mpaka akafikia hatua ya kupewa matatizo hayo.
"Usilie mke wangu, usilie futa machozi yako," alisema Fredrick.
"Nashindwa kufanya hivyo mume wangu," alijibu Evelyne huku machozi yakiendelea kumdondoka.
Alipokuwa akiendelea kumtazama mume wake pale kitandani machozi yalizidi kumbubujika tu, kila kitu kilibadilika katika maisha yake, alipowakumbuka ndugu wa mume wake alizidi kujisikia vibaya mno, alijua fika hawakumpenda, walimtenga hivyo kila kitu alichokuwa akikifanya kilionekana kuwa kibaya.
Aliamua kuwapigia simu wazazi wake na kuwaeleza kila kitu kilichokuwa kikiendelea, alihitaji msaada wao lakini walionekana kuchukizwa na taarifa hizo, hawakutaka kuona akiendelea kuteseka wakati bado walikuwa hai. Maamuzi ambayo waliamua kuyachukua ni kumuhitaji binti yao arudi nyumbani haraka iwezekanavyo.
"Naomba upande basi kesho uwe umeshafika hapa nyumbani," alisema baba yake kwa sauti ya ukali.
"Nitaondokaje baba halafu nitamuacha Mume wangu na nani?" Aliuliza Evelyne.
"Muache na ndugu zake wewe rudi zako nyumbani," alijibu baba yake kwa msisitizo.
"Hapana baba bado itakuwa ni vigumu kwani nitahitajika pia kazini," alisema Evelyne.
Yalikuwa ni mazungumzo mafupi ambayo yalihitajika utekelezaji wa haraka sana lakini Evelyne hakutaka kukubaliana nayo. Hakutaka kuona akiondoka na kumuacha mume wake akiendelea kuteseka kitandani. Alikumbuka siku yao ya harusi jinsi alivyokula kiapo mbele za watu na kuahidi kuishi naye katika shida na raha, aliamini katika kipindi hicho kilikuwa ni cha shida hivyo hakuwa na jinsi ya kufanya ilibidi amvumilie mume wake.
Rafiki yake Happy hakumtupa mkono katika kipindi hicho, alikuwa na yeye bega kwa bega katika kila hali, alionyesha msaada mkubwa sana. Alipokuwa akimuona Evelyne akiteseka na mume wake hospitalini alimuonea huruma sana, alizidi kumfariji kwa maneno ya matumaini ambayo yalizidi kumpa nguvu. Ndoto yake kubwa aliamini siku moja mume wake angeweza kuinuka kitandani na maisha yakaendelea lakini hilo lilikuwa ni jambo lisilowezekana.
Siku ziliendelea kukatika huku Fredrick na yeye akizidi kuteseka hospitalini, alianza kupoteza matumaini ya kuishi baada ya afya yake kuanza kudhoofika, aliamini ule ndiyo ulikuwa mwisho wa maisha yake, mwisho wenye mateso makali mno.
"Hapana usijiwazie kifo, huwezi kufa mume wangu," alisema Evelyne.
"Angalia ninavyoteseka hapa kitandani mke wangu, madaktari wameshindwa kunitibu hivi unafikiri nitapona kweli?"aliuliza Fredrick huku machozi yakimbubujika.
"Hapana huwezi kufa," alisema Evelyne.
Yalikuwa ni maneno machache lakini aliamua kuishi ndani yake, hakutaka kumpoteza Fredrick, alichoamua kukifanya ni kuanza kuhangaikia matibabu yake.
Madaktari walimshauri ampeleke nchini India kwani huko ndipo palipokuwa na uwezekano mkubwa wa mume wake kutibiwa na kupona kabisa.
Alipoambiwa hivyo hakutaka kupoteza muda, alianza kupanga mipango wa kumsafirisha mume wake nchini humo na baada ya kufanyiwa matibabu iligundulika kuwa Fredrick asingeweza kupona.
Hilo lilizidi kumuumiza sana, hakutaka kuamini maneno hayo hata kidogo.
Aliporudi nchini Tanzania bado aliendelea kuhangaika na mume wake.
Ilifikia wakati akaanza kuwaamini wachungaji, alipokuwa akisikia palikuwa na mchungaji ambaye aliweza kumuombea kilema kisha akapona aliamua kwenda, kila kanisa alilokuwa akienda kwa ajili ya maombezi ya mume wake hakuna miujiza iliyoweza kutendeka.
****
Richard alifahamu kila kitu kilichokuwa kikiendelea katika maisha ya Evelyne, alimpenda mno msichana huyo, kutokana na hali aliyokuwa nayo aliamini ulikuwa ndiyo muda wake muafaka wa yeye kujitokeza kwa mara nyingine, hakutaka kumuomba msamaha ila alichoamua kukifanya ni kurudi kama rafiki ambaye aliguswa na matatizo yaliyompata Evelyne katika ndoa yake.
Alijitoa katika kila hali na mali, hakutaka kuonekana adui kwa msichana huyo, kila alilokuwa akilifanya alilifanya kwa kuonyesha moyo wa msaada.
Baada ya kupita miezi miwili Fredrick aliweza kupoteza maisha, kilikuwa ni kifo ambacho kilimuacha Evelyne na maumivu makali mno, ndugu zake Fredrick waliamua kumshtaki Evelyne polisi na kisha wakamfungulia kesi ya mauaji, ilikuwa ni kesi nzito ambayo ilimuweka Evelyne na hatia ya mauaji lakini kutokana na uwezo wa kifedha aliyokuwa nao Richard alihakikisha anapigana mpaka anafanikiwa kumuweka huru Evelyne.
Richard alimuomba msamaha Evelyne na kumuahidi kuwa muaminifu katika maisha yake yote. Evelyne hakuwa na kipingamizi chochote, aliamua kumsamehe Richard kisha mapenzi yao yakarudi kuwa kama zamani.
Walifanikiwa kufunga ndoa na baada ya mwaka mmoja kupita walifanikiwa kupata mtoto wa kiume, alikuwa ni mtoto mzuri sana, aliyekuwa na afya njema. Evelyne aliamua kumpa jina la Fredrick ikiwa ni kama kumbukumbu ya kumuenzi mwanaume huyo huko alipo.
Maisha yao yalizidi kutawaliwa na furaha huku mtoto wao akiendelea kukuwa vizuri bila matatizo yoyote.

MWISHO.
 
Back
Top Bottom