Nisaidieni neno hili,,,

Jitihada

Senior Member
Feb 6, 2011
155
10
Habari wana jamvi hasa mlio wazawa! naombeni mnisaidie kinyume cha neno hili la kiswahili "UPANA".
 
Ndugu Jitihada,
Ni vyema tukaelewa kuwa jibu la swali lako linategemea muktadha (context) wa utumizi wa neno hilo. Hii ni kwa sababu neno "pana" au "upana" linaweza kuwa na maana zaidi ya moja kulingana na muktadha wa matumizi.

Kwa mfano, sentensi zifuatazo zitaeleza vema:
(1) "Upana wa barabara ya Mandela umesababisha kuvunjwa kwa nyumba nyingi za wakazi wa eneo la karibu". Hapa muktadha wa neno "upana" ni ule wa vipimo (malathaan vya metriki mf. mita n.k). Katika muktadha huu kinyume cha neno Upana ni WEMBAMBA. (wiide-narrow).
(2) "Suala la uraia wa nchi mbili litazamwe kwa upana wake, yaani madhara na faida zake". Hapa utaona kuwa neno "upana" halina uhusiano wowote na vipimo kama hapo juu. Limetumika katika muktadha mwingine kabisa. Hapa kinyume chake ni "Ufinyu". (broad-narrow)

Kwa hiyo: Ingekuwa bora ukitaka msaada kama hivyo utoe na muktadha wa matumizi kama ikibidi. Vinginevyo unaweza ukapewa majibu katika muktadha ambao hukutaarajia.
Asante.
 
Asanteni kwa mawazo yenu PRETA na SENEOR BACHELOR kwan mnazidi kuupanua uelewa wangu juu ya hilo neno lenye maana pana,
 
Ndugu Jitihada,
Ni vyema tukaelewa kuwa jibu la swali lako linategemea muktadha (context) wa utumizi wa neno hilo. Hii ni kwa sababu neno "pana" au "upana" linaweza kuwa na maana zaidi ya moja kulingana na muktadha wa matumizi.

Kwa mfano, sentensi zifuatazo zitaeleza vema:
(1) "Upana wa barabara ya Mandela umesababisha kuvunjwa kwa nyumba nyingi za wakazi wa eneo la karibu". Hapa muktadha wa neno "upana" ni ule wa vipimo (malathaan vya metriki mf. mita n.k). Katika muktadha huu kinyume cha neno Upana ni WEMBAMBA. (wiide-narrow).
(2) "Suala la uraia wa nchi mbili litazamwe kwa upana wake, yaani madhara na faida zake". Hapa utaona kuwa neno "upana" halina uhusiano wowote na vipimo kama hapo juu. Limetumika katika muktadha mwingine kabisa. Hapa kinyume chake ni "Ufinyu". (broad-narrow)

Kwa hiyo: Ingekuwa bora ukitaka msaada kama hivyo utoe na muktadha wa matumizi kama ikibidi. Vinginevyo unaweza ukapewa majibu katika muktadha ambao hukutaarajia.
Asante.
Kwa ufupi unaweza kinyume chake ni: Ufinyu, Wembamba.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom