nisaidieni na hili

Kipipi unaishi wapi ndg yangu?
Angalia kwenye red hapo chini.
WANAUME WANAOKUBALIWA KUFUNGWA PINGU ZA MAISHA TZ HAWAONEKANI WOTE WANAJIFICHA na kina dada wanawawinda kweli,sasa dada kampata wewe unamwambia amwambie jamaa asubiri?si atafurahia kula vya bure,vikichakaa anachukua vingine brand new?

SIKU HIZI
Kwani huyo mchumba wako anashindwa nini kukusubiri ukamaliza chuo? Manake mi naona kutumikia vitu viwili kwa wakati mmoja napo ni shughuli eti......tena kama nyie mtakaokuwa kwenye ndoa changa unaweza ukajikuta unabase sana kwa mume kuliko hata masomo! Kuna wazazi ambao hawapendi mabinti zao waolewe wakiwa katikati ya masomo, juzijuzi tu nilipishana na binti akilalamikia suala kama hili cjui nae aliishia wapi!
 
huyo my uncle wako anataka uolewe na mwanawe yeye ndio maana hamkubali huyo bwana wako
 
Don't rush into this, Jipange na umalize elimu yako. Mjomba anaangalia furure yako na ni lazima matunda ya elimu yako yaonekane. Trust Me. Kama kweli anakupenda atasubiri tuu...


shule ntamaliza na ntasoma sana 2 ila kapata mahali now..amwache atoe jamani
 
Achana nae mjomba, mwambie huo ndio msimamo wako, kama unampenda mpenzi wako kwa dhati
mjomba nae, kuishi na wewe anataka hadi akuchagulie mume, usikute keshakula pesa za watu
kuna wasichana waliharibiwa maisha yao ya kimahusiano na ndugu kama hao, na mpaka leo wameshikilia
mchuma siti ya kukaa hakuna

Nikwambie mrembo, wakati nataka kuolewa, nilikatazwa na kila mtu, kwangu mie nahisi ilikuwa kwa nia nzuri tu
sababu nilikuwa mdogo, yaani ndio kwanza nimemaliza form 4 tu, watu walikuja juu sana, itakuwaje uolewe, mara mtoto
wetu anajitahidi ila unamkatiza shule, nusu niwasikize, ila moyoni nilijua kabisa huyu ndie mume, nikashikilia msimamo
niliolewa na mengine yote waliyotaka nifanye nikayafanya ndoani, kwa hiyo kama unahisi toka moyoni ndio huyo jamaa unampenda olewa
ili hata kama mambo yakienda mrama usijute huko mbele,mwambie mjomba huyo ndiye mume uliyechaguliwa na Mungu
Pia sali Mungu akuonyeshe njia sahihi




asante mpenzi,ntasimama na msimamo wangu,manake wasije wakadhani kua mimi kuondoka na kuish na huyo mwanaume nashindwa naweza ila sema nawaheshimu sana,nimepata this kwangu naita bahati kama mambo hayata niendea vizuri basi nijute kwa kujilaumu
 
tauta mtu mzima ambaye ni ndugu yenu amkalishe mjomba kumshawishi. ila akikataa kabisa na mama akakubaliana nae, sidhani kama itakuwa vema kuolewa sasa au hata na huyo jamaa. kitu kimoja naamini, ur parents knows baby gal! so trust them,manake kesho na keshokutwa ukipatwa na lolote u will need them. waliona jua kabla yako, experience is a good teacher.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom