nisaidieni na hili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

nisaidieni na hili

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by oldd vampire, Aug 11, 2011.

 1. oldd vampire

  oldd vampire JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 253
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mh wana jf nisaidieni..mimi naishi na mjomba wangu na yeye ndie kama mzazi wangu kwa hapa jijini,lakini nina mama yangu mzazi yupo mkoani huko na hapa jijini nasoma chuo mwaka wa pili naingia wa tatu hapo october..sasa nina boyfriend wangu ambae tumetoka mbali sana na nina mpenda sana..sasa anataka kunitolea mahali eti mjomba kakataa nkimukiza kisa anadai time will tell mara hamtaki that mwanaume,wakati mama yangu mzazi kakubari ila nae anamsikiliza sana mjomba...na mbaya zaidi kaniambia ni cancell kila kitu.wakati upande wa mwanaumewamekuja tayari na wapo kwenye kujipanga..nifanyaje?
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  mijomba mingine bana.....kero tupu..........
   
 3. G_crisis

  G_crisis JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2011
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 715
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Hivi bado kuna kutoa mahari hadi sasa??kwa sababu mmependana wenyewe we waambie kama hawataki utaolewa bila hata hiyo mahari
   
 4. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Achana nae mjomba, mwambie huo ndio msimamo wako, kama unampenda mpenzi wako kwa dhati
  mjomba nae, kuishi na wewe anataka hadi akuchagulie mume, usikute keshakula pesa za watu
  kuna wasichana waliharibiwa maisha yao ya kimahusiano na ndugu kama hao, na mpaka leo wameshikilia
  mchuma siti ya kukaa hakuna

  Nikwambie mrembo, wakati nataka kuolewa, nilikatazwa na kila mtu, kwangu mie nahisi ilikuwa kwa nia nzuri tu
  sababu nilikuwa mdogo, yaani ndio kwanza nimemaliza form 4 tu, watu walikuja juu sana, itakuwaje uolewe, mara mtoto
  wetu anajitahidi ila unamkatiza shule, nusu niwasikize, ila moyoni nilijua kabisa huyu ndie mume, nikashikilia msimamo
  niliolewa na mengine yote waliyotaka nifanye nikayafanya ndoani, kwa hiyo kama unahisi toka moyoni ndio huyo jamaa unampenda olewa
  ili hata kama mambo yakienda mrama usijute huko mbele,mwambie mjomba huyo ndiye mume uliyechaguliwa na Mungu
  Pia sali Mungu akuonyeshe njia sahihi
   
 5. I

  Iron-rock Member

  #5
  Aug 11, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I had a friend who had a boyfriend,soon she declared 2be maried with,bt her eldest brother rejected her engagement at al,bt she forced and get maried wit such person bt 4now she is in a commah regreating and repenting.
  So plz listen old men coz they may know much about ur husband2be
   
 6. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Huwezi juwa labda ni mtoto wa mjomba kwa nyumba ndogo sasa mjomba hataki kufafanua.
   
 7. BlackBerry

  BlackBerry JF-Expert Member

  #7
  Aug 11, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 1,844
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Haaaaa kaka nimsikilize? na hiyo commah inahusiana vipi na huyo mume? kuna la kusikiliza kama lipo, ila kama hawana reason ya kunikataza kuolewa na mpenzi wangu watanisamehe, sidhani hata kama vitabu vya dini vinaruhusu hili, wazee wengune wanakukataza tu simply wana maugomvi yao ya siku nyingi
   
 8. BlackBerry

  BlackBerry JF-Expert Member

  #8
  Aug 11, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 1,844
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ndio haya makosa ya wazazi tunayalipa sie wakati wao wanaishi raha mstarehe na wake/waume zao
   
 9. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #9
  Aug 11, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Mjombaaaaaa! kwani wewe ndo utaishi na huyo mchumba? achia bana watu wakaishi maisha waliyochagua siyo mjomba una bana tuuuu!!!
   
 10. LexAid

  LexAid JF-Expert Member

  #10
  Aug 11, 2011
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 1,950
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Don't rush into this, Jipange na umalize elimu yako. Mjomba anaangalia furure yako na ni lazima matunda ya elimu yako yaonekane. Trust Me. Kama kweli anakupenda atasubiri tuu...
   
 11. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Nakushauri ujipe muda kidogo kabla ya kuamua...Kwa nini na huyo muoaji amekuja full gear? Mwambie naye apunguze speed kidogo...Ukipata muda kupumua labda unaweza kuelewa kwa nini mjomba wako anakuzuia. Haiwezekani akuzuie tu bila sababu...!

  Kwa uamuzi wowote utakaochukua katika mazingira ya sasa lazima utabaki na jeraha la aina fulani..Labda usichoweza kujua kwa sasa ni ukubwa wa hilo jeraha...Jipe muda mdogo wangu kabla ya kujiingiza jela!!
   
 12. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #12
  Aug 11, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  BB...hata huyo mjomba kalipa gharama ambayo si ndogo...Nimelea watoto wa watu (ndugu wa karibu na wengine) na hakuna kazi ngumu kama hiyo. Nahisi huyo mjomba hana nia mbaya...!
   
 13. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #13
  Aug 11, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,278
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Mwambie mjomba akupe sababu akikataa ongea na shangazi atakuwa anajua tu. Usikubali akupe jibu la time will tell. Yawezekana kuna kubwa ambalo wanshindwa kukwambia. Je mama yako amekuwa vipi convinced na kaka yake (mjomba) mpaka nae akaunga trela. There must be something they are hiding. Je unadhani mjomba anaweza kuwa anamfahamu huyo kijana au ndugu zake? Nadhani ukipeleleza vizuri lazima utapata sababu.

  Angekuwa baba yako ningesema itakuwa ni kawaida kwani najua wababa wengi ni wagumu kukubali watoto wao waolewe; lakini wajomba ni watu wenye busara na hawana hizo. There must be somehting they fear telling you. Be carefull.

  Unajua sisi tunakutana kimjini mjini na kukimbilia ndoa. Yawezekana mjomba ka dig deeper kakuta mambo si mambo. watu wengine kwao kwao wanga! Hata mimi kabla sijaolewa wazazi walifanya research ili mtoto wao nsijeenda kwenye koo za wachawi.
   
 14. Mpatanishi

  Mpatanishi JF-Expert Member

  #14
  Aug 12, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Soma binti tengeneza GPA elimu yako ndio maisha yako na sio mume.

  Msikilize anko wako naamini ana busara.

  Imagine umeolewa then chuo ukafeli kwa ku base kwako kwenye ndoa,jamaa akakuzalisha then akaanza mambo ya ajabu ulevi umalaya n.k hayo msaibu utampelekea nani?

  Ndoa si lelemama isikie hvyo hvyo, najua umeshajenga taswira ya matamu ya kwenye ndoa bt always r'mber
  ''Kikupacho utamu na Uchungu kitakupa''
  Piga kitabu sawa eenh mtoto mzuri.
   
 15. Shantel

  Shantel JF-Expert Member

  #15
  Aug 12, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 2,021
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  mhhh gpa bila mume si unaweza pata stress mpaka gpa ukaiona nzito kama nyumba
   
 16. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #16
  Aug 12, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,278
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Afu maneno ya kuwa ndoa ni wewe na mumeo ni theory zaidi. Hiyo ina work tu kama mtaishi happily ever after. Asikwambie mtu pale ndani ya ndoa mambo yakienda ndivyo sivyo it is your mother, sisters, brothers that will offer their shoulder for you to lean on. Mimi naheshimu sana ndugu zangu. Utajajitia kitanzi kwa kukosa wa kushare nae matatizo yakikufika shingoni kwa kuwa home umerikoroga.
   
 17. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #17
  Aug 12, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Kwani huyo mchumba wako anashindwa nini kukusubiri ukamaliza chuo? Manake mi naona kutumikia vitu viwili kwa wakati mmoja napo ni shughuli eti......tena kama nyie mtakaokuwa kwenye ndoa changa unaweza ukajikuta unabase sana kwa mume kuliko hata masomo! Kuna wazazi ambao hawapendi mabinti zao waolewe wakiwa katikati ya masomo, juzijuzi tu nilipishana na binti akilalamikia suala kama hili cjui nae aliishia wapi!
   
 18. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #18
  Aug 12, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Yaani hapo umeongea kweli kabisaaaaa!
   
 19. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #19
  Aug 12, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Anza maombi kuvunja kauli za mjomba wako, ana laana ya utotoni huyo!! kwa yesu kila kitu inawezekana. we omba kwa bidii.
   
 20. r

  rakeyescarl JF-Expert Member

  #20
  Aug 12, 2011
  Joined: Dec 9, 2007
  Messages: 408
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Pole dada,
  Ndio maana siku hizi wasichana wanaolewa bila kutoa taarifa haswa akiishaona kuna kigingi cha design hiyo,mnakuja kuona dada anakuja na mtoto,anaomba samahani eti haturudia tena!
  Wazee wanamalizia mlete haraka atoe mahali kabla hatujamuua huyo mchafuzi! ngoma inaisha hapo x 2,uzuri wa TZ procedure za mahali ukija mna mtoto na ukichukuliwa kabla kwa makabila mengi ni sawa.Unawahi chap chap church unatubu basi unaendelea

  Jinasishe halafu waambie tayari umenasa ingawa doooh midume ikijua kuwa sasa yy ndie mjomba,mama etc inabidi uwe na option 2 incase anaanza tabia zetu za kiume!
  :boxing:
  RE
   
Loading...