Habari za humu ndani wakuu, mimi ni kijana wa kiume umri wangu ni miaka 25, nimepanga hapa Dar na nina jitegemea. Hebu ni saidieni sehemu nzuri ya kupata girlfriend maana naona kama tokea nipange now ni mwezi wa nane sijapata demu mzuri ninayemtaka.
Wengi hupata magirlfriend sehemu za kazi but kwangu sehemu yangu ya kazi hamna mabinti, wengine pia wanawapata kitaa too bad for me maana natoka saa 11 asubuhi narudi saa mbili usiku na nimechoka nakosa hadi muda wa kuzurura kuangalia hata kama ninaweza kupata girlfriend.
Hebu wakuu nisaidieni kwa hapa Dar sehemu ipi ninaweza kupata girlfriend awe mzuri kwa haraka nimechoka kuwa mpweke. Note nataka girlfriend mwenye heshima zake nasio wale wanaojiuza