Nisaidieni kumuokoa mke wangu mtarajiwa

Mzee huhitaji ushauri kila kitu kiko wazi hapa. Ukiona kumuacha ni ghali kwa thamani 1.2m basi oa but maisha yako yana thamani zaidi ya hiyo pesa
 
kama wewe ulivyoganda kwa desh desh.

bora mie nilieganda kwa mapenzi mema......sina timbwilitimbwili.....
huyu mwenzetu naona anajigandisha na kifo.....khaaa
kweli Bushoke aliimba......

 
Nahisi bado wampenda kwa dhati mkeo mtarajiwa ila nikinukuu maneno yako ni kuwa "Kunguru hafugiki"!!!!
Hata ukijakumuoa ataendelea tu kuwa "jamvi la wageni". Kumbuka ya kuwa maisha yako yana thamani kubwa sana kuliko 1.2M. Huyo dada atakuja kukuletea gonjwa la UKIMWI na utakuja juta maisha yako yote, kisa umependa usipopendwa. Huyo hata ukioa ni pasua kichwa ataendelea tu kugawa dozi kama pipi.

Achana nae, kaa kwa muda umsahau na kumpotezea jumla. Mungu atakupatia mke mwema ambaye atakusikiliza na kukuheshimu milele yote!!!!
 
Pole mkuu, Misambano( mwanamuziki) alishasema usimng'ang'anie asiyekupenda. Bora umegundua mapema angali mchumba.

Sahau kuhusu mahari anza upya, furaha yako ina thamani zaidi ya hiyo mahari.
 
story kama hizi ndio zinazofanya watu waamini kwamba kumbe kuna possibility ya mtu kupewa limbwata... yaani pamoja na solid evidence aliyonayo, jamaa bado anaomba ushauri wa nini cha kufanya badala ya kuchukua hatua?
 
pole sana ,umebakiza kwenye kupima ukakutwa umeathirika kwa staili hii..pole sana
 
........mwenzako ana cheat we bado unasubiri ushauri? Sijui kwako, ila mimi mtu akicheat sisubiri ushauri na wala siangalii kama ndoa ya kanisa au ya wapi!! Hiyo mahari samehe, ni pesa ndogo sana ukilinganisha na uhai wako. Ila fuata moyo wako.
 
swala la kumpenda lisahau kwa sasa-maana inaonyesha yeye hakupendi kiasi hicho unachompenda
achana naye mapema asije kuletea ukimwi akakumaliza kabsa
 
Grader pole saana kaka... Kweli umependa... Na wewe hapo ullipo hapo sidhani kama hata waweza kubali ushauri... Kwa muktadha wa kufahamu yooote hayo nilo weka blue bado unataka ushauri na bado umejiandaa kutoa mahari ya 1.2... We kaka wewe Mwanaume wa wapi? Dah! Kweli Umejaliwa roho nzuri.... Naomba elezea... Unataka ushauri wa kumbadilisha tabia ama wa jinsi ya kuvumilia? Maani ni dhahiri mpango wa kumuoa uko pale pale.... Na take note: Lazima atakuendesha hivo just brace yourself.
Kweli this is a lost case! hadi AshaDii aseme hivi ujue hakuna chance kabisaaaaa!:lol:
Kwa mtoa mada, mshahuri awe anatumia condom huko nje. Inaonekana umesha mkubali alivo, basi angalau jikinge
 
Ushukuru umegundua kutokua muaminifu kwake kabla hujaoa. Mchunguze zaidi ukiona bado anazngua mpotezee
 
si huwa mnasema walimu ndio wake wazuri? pole mlengwa msaidie ana matatizo huyo usimuache
 
Kama kusoma huwezi hata picha,na akili za kuambiwa changanya na zako kijana,tafuta mwingne kaka au mpaka upewe kadi ya harusi,n actions speak louder than words
 
ndugu yangu,
umeshajua kuwa huyo mchumba wako ni mzinzi tena wa kupindukia....

hebu ipende nafsi yako hata kiduchuuuuu
muache huyo mwanamke, maradhi mengi

uzima wa nafsi yako una thamani kubwa kuliko 1,200,000!!!!
kumbuka uhai ni mara moja tu!!!

waarifu wazazi wake kuwa umeshindwa kutokana na tabia za binti yao, bwaga manyanga
maana usipopata ukimwi, utapata maradhi ya moyo, au utakufa kwa kihoro...
 
Kweli this is a lost case! hadi AshaDii aseme hivi ujue hakuna chance kabisaaaaa!:lol:
Kwa mtoa mada, mshahuri awe anatumia condom huko nje. Inaonekana umesha mkubali alivo, basi angalau jikinge

hahahaha ni kweli loh...
anapopeleka misaada ukweni asisahau kumtumia wife maboksi ya kondom. ndo njia pekee ya kujikinga ingawa kama wife to be wake atazitumia au la hiyo ni ishu nyingine
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom