Nisaidieni kumuokoa mke wangu mtarajiwa

Hamna ushauri hapo zaidi ya kupiga chini, au mpaka akupatie ukimwi ndo uanze zile za ningejua? PIGA CHINI FASTA, ALAAAAH!
 
Ndugu zangu,nawaomba mnisaidie kwani mke wangu mtarajiwa siyo muaminifu kwani anazini hovyo na watu kila anavyoona yeye sijui nifanyeje?
1. yeye anafundisha kwenye shule moja huko Tabora na mimi nafanya kazi kwenye kampuni ya ujenzi Dar.
2. Namsaidia kila kitu ikiwa pamoja na wazazi wake pia LAKINI kweli kunguru hafugiki na kila kukicha anaendeleza dozi ya wanaume.
3. Wakati wa likizo ndiyo kubwa zaidi amenidanganya anakuja huku Dar,kumbe amekwenda kwa mwanaume mwingine.
4. Bibi yake anamjua huyo jamaa mwingine anamfichia.
5. Ndugu zangu nitaongea mengi LAKINI moyo unaniuma hali ambapo nimempenda mtu lakini ananifanyia hivyo hali ambapo nimegharamia hela nyingi kwenye mahali pekee ni Tsh 1,200,000/-

Unasubri nini sasa? Kimbia kunguru hilo litakuua!
 
kumwacha mpenzi wako ni maamuzi magumu ambayo kiukweli baadaye yanakuwa na faida, kwa sasa una kila sababu ya kumwacha though inaonyesha wampenda sana but jipende mwenyewe pia, raha ya mapenzi ni kupendana na siyo kuumizana kama anakupa hard time ni dhahiri akupendi na kama anakupenda angekulinda, kukutunza na kukuheshimu, yan mpaka unamjua mpenzio kuwa ni kunguru afugiki ni dhahiri akuheshimu hata kidogo.
 
masikini wee pole ndugu yangu pole sana.
achana nae huyo atakuumiza zaidi ya hapo yan, inaonekana io tabia iko damuni kbs so kama utamuoa tegemea hayo mambo siku zoote.
na ukimuoa utakuwa umefanya mistake moja balaa , hakufaiii.
 
Napata wazo kuwa unadhani ukimwoa atatulia,kwa sababu pamoja na kuyajua yote hayo bado umetoa mahari!(mi nasema hilo la kutulia SAHAU!!)
Naamini hata kwa mtu aliye kwenye ndoa yangemtokea hayo ya kwako angefikiria upya uamuzi wa kuendelea.
Tuchukulie kuwa umemwoa na kweli ametulia, unadhani utakuwa na imani naye kabisa?! Nijuavyo mimi ile hisia tu kuwa anaweza kutoka nje ya ndoa unapokuwa safarini itakukosesha amani! Sasa, je uko tayari kuishi hivyo kwa miaka yako yote iliyobaki ukiwa naye?! coz hiyo ndo maana halisi ya ndoa!!
Kwangu mimi kutoa mahari na kumsaidia yeye kwa kila kitu pamoja na nyumbani kwao ni kama ushamuoa, so alipaswa kukuheshimu zaidi! au hata kukuogopa kidogo basi (Najua hata hakuogopi,tafakari hilo pia..)
Hebu jaribu kufikiria yuko hivo sasa hivi, je pale utakaposema hutamwacha hadi kifo atakuwaje?!
Bibi anajua wewe ndo unayepeleka matumizi nyumbani, unadhani kwa maisha yalivyo kwa sasa hata kama ni wewe ungesema!?
Chukua hatua haraka,au labda hata ushapigwa dude!
 
Ndugu zangu,nawaomba mnisaidie kwani mke wangu mtarajiwa siyo muaminifu kwani anazini hovyo na watu kila anavyoona yeye sijui nifanyeje?
1. yeye anafundisha kwenye shule moja huko Tabora na mimi nafanya kazi kwenye kampuni ya ujenzi Dar.
2. Namsaidia kila kitu ikiwa pamoja na wazazi wake pia LAKINI kweli kunguru hafugiki na kila kukicha anaendeleza dozi ya wanaume.
3. Wakati wa likizo ndiyo kubwa zaidi amenidanganya anakuja huku Dar,kumbe amekwenda kwa mwanaume mwingine.
4. Bibi yake anamjua huyo jamaa mwingine anamfichia.
5. Ndugu zangu nitaongea mengi LAKINI moyo unaniuma hali ambapo nimempenda mtu lakini ananifanyia hivyo hali ambapo nimegharamia hela nyingi kwenye mahali pekee ni Tsh 1,200,000/-

nduigu yangu ushauri wangu kwako ni kuwa ni vizuri umuache huyo mwanamke kwani hakupendi kabisa. Endapo angekupenda hata kama angekuwa na wanaume wa nje kabla yako angekuwa amewaacha wtoe

tumia akili ndogo, mwanamke amabye umeshamlipia na mahali halafu bado anatembea na wanaume wengine na kulala huko kwa kisingizio kuwa anakuja kwako

tafadhali huyo mwache, anza kutafuta mwanamke aliye tulia upate kumuoa,

nakushauri hiyo sh. miloni 1.2 ni hela nyingi lakini ni hela ndogo sana ukilinganisha na dhamani yako, hivyo isamehe, Mungu atakupatia nyingine

usiposikia haya utalia baadae,

kumbuka ww si wa kwanza kuacha mwanamke aliyelipiwa mahali wako wengi wamefanya hivyo akiwemo mjomba wangu mwenyewe alimpiga chini mwanamke wake amabye hakuwa mwaminifu na ameoa mwanamke mwingine

kufanya maamuzi magumu ndiko kunadhihrisha uwezo wako kama mwanaume ambaye utaisimamia familia yako
 
Hamna ushauri hapo zaidi ya kupiga chini, au mpaka akupatie ukimwi ndo uanze zile za ningejua? PIGA CHINI FASTA, ALAAAAH!

mwanamke akikupenda atafuata sheria zako mojawapo ikiwa kutotoa mwili wake kwa mwanaume mwingine

dunia imechafuka, tafuta mwanamke mwingine, fuata taratibu oa na uishi naye

kumbuka huyo mwnamke sio riziki yako
 
Hiyo 1.2 ni ndogo sana ukilinganisha na uhai wako
Ila nachokushauri mgosi jaribu kuchunguza je izo shutuma unazompa ni za kweli ? i mean umefanyia uchunguzi
manake umesema mara nyingi we ni mtu wa ruti sana,kama una uhakika go ahed ila usiusemee moyo kama bado unampenda endelea kuugulia manake usije ku regeret mbeleni.
 
ndugu zangu,nawaomba mnisaidie kwani mke wangu mtarajiwa siyo muaminifu kwani anazini hovyo na watu kila anavyoona yeye sijui nifanyeje?
1. Yeye anafundisha kwenye shule moja huko tabora na mimi nafanya kazi kwenye kampuni ya ujenzi dar.
2. Namsaidia kila kitu ikiwa pamoja na wazazi wake pia lakini kweli kunguru hafugiki na kila kukicha anaendeleza dozi ya wanaume.
3. Wakati wa likizo ndiyo kubwa zaidi amenidanganya anakuja huku dar,kumbe amekwenda kwa mwanaume mwingine.
4. Bibi yake anamjua huyo jamaa mwingine anamfichia.
5. Ndugu zangu nitaongea mengi lakini moyo unaniuma hali ambapo nimempenda mtu lakini ananifanyia hivyo hali ambapo nimegharamia hela nyingi kwenye mahali pekee ni tsh 1,200,000/-

maisha yako ni muhimu kuliko hizo pesa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom