Nisaidieni jamani logistics za rufiji

sikiolakufa

JF-Expert Member
Feb 1, 2010
411
54
Wadau naomba msaada ninakusudia kusafiri kwa gari ndogo kwenda rufiji lengo ni kwenda kuongea na wanavijiji wanaoishi pembezoni mwa delta ya rufiji, je ninapitia njia gani? Ni lami tupu? Je gari ndogo itafika mafuta niweke kiasi gani? Je ni mambo gani ya kuzingatia kabla sijaanza safari yangu? Naombeni maoni yenu
 
Kama ni utete, ni kilometer 200, lami kilometer 160 na zinazobaki vumbi.
 
Ukienda maeneo ya delta yenyewe mh baiskel ,mguu ,mtumbwi bila kusahau ulinzi kutoka askari nyama pori -simba mamba wa kumwaga!
 
Wadau naomba msaada ninakusudia kusafiri kwa gari ndogo kwenda rufiji lengo ni kwenda kuongea na wanavijiji wanaoishi pembezoni mwa delta ya rufiji, je ninapitia njia gani? Ni lami tupu? Je gari ndogo itafika mafuta niweke kiasi gani? Je ni mambo gani ya kuzingatia kabla sijaanza safari yangu? Naombeni maoni yenu

Kayagila.

Sehemu za Delta niliwahi kufika mwaka 2009, nilileta watu waliotaka kuwekeza katika eneo hilo katika utalii wa kimazingira(BIO tourrism).

Unaposema Delta unamanisha ni vijiji vya Salali,kiasi,kiechulu, twasalie,jaja,kiongoloni, mpombwe, mtunda, nyamisati.
Unaweza kuingilia nyamisati. ambapo unaenda mpaka kijiji cha Bungu kisha unaacha njia kuu na kutembea barabara za vumbi kama kilomota 45.Hapo utatumia boti kutembelea vijiji vyote

Au unaweza kwenda mpaka Mohoro ambapo ni kima 240 kisha unaingia.

Cha msingi ni lazima uchukue boti. Gari utaacha. Ni sehemu zenye changamoto kubwa sana na zina mengi a kujifunza.
Mbunge wao anaitwa Malombwa na mwingine Dr Seif.

Back
Top Bottom