Nisaidieni hospital inayodili na ugonjwa wa uvimbe

jmratino

Member
Jul 20, 2017
15
5
Kama kichwa cha habari kinavyoonyesha baba yangu anasumbuliwa na huo uvimbe, umekua ukimdhoofisha afya yake, tumejaribu mara kadhaa kumpeleka hospital lakini matibabu anayopewa yameshindwa kumponyesha, kwa maelezo yake anasema linavuta kwa ndani kama mtu aliyekulenga na mshale wa sindano.

Nimejaribu kuongea na dokta kuona uwezekano wa kufanya operation wanasema limekaa sehemu mbaya kwa sababu wanadai shina la huo uvimbe limekaa karibu sana na mishipa ya moyo, kuhusu kansa tumepima mara kadhaa na majibu yanasema sio kansa.

Historia yake palianza kama kipele kidogo mwanzoni mwa mwaka 2000 na matibabu alianza 2006 pale Muhimbili lakini hata hivyo matibabu waliyompa yalimpa nafuu ya muda tu.

Nawasilisha.

20240104_170132.jpg
 
hospitali zenye vitengo vya saratani (ONCOLOGY DEPARTMENT) kama KCMC, OCEAN ROAD, huko utakutana na ma bingwa bobezi.
 
Kama kichwa cha habari kinavyoonyesha baba yangu anasumbuliwa na huo uvimbe, umekua ukimdhoofisha afya yake, tumejaribu mara kadhaa kumpeleka hospital lakini matibabu anayopewa yameshindwa kumponyesha, kwa maelezo yake anasema linavuta kwa ndani kama mtu aliyekulenga na mshale wa sindano.

Nimejaribu kuongea na dokta kuona uwezekano wa kufanya operation wanasema limekaa sehemu mbaya kwa sababu wanadai shina la huo uvimbe limekaa karibu sana na mishipa ya moyo, kuhusu kansa tumepima mara kadhaa na majibu yanasema sio kansa.

Historia yake palianza kama kipele kidogo mwanzoni mwa mwaka 2000 na matibabu alianza 2006 pale Muhimbili lakini hata hivyo matibabu waliyompa yalimpa nafuu ya muda tu.

Nawasilisha.

View attachment 2861811

Habari!
Hili ni tatizo linalotakiwa kutibiwa na Cosmetics surgeon akiwashirikisha madaktari wengine ambao ataona inafaa kama timu moja.

Sina hakika kama wakati akitibiwa Muhimbili, hiki kitengo kilikuwezo. Kwani kwa maelezo yako hii inaonyesha ni kitu kinaitwa Keloid.

Kama kwa wakati huo hukupata kuonana na daktari bingwa wa aina hiyo au kitengo hicho, ni vyema kufika na kupata ushauri wao kwa sasa.

Kama hakuna mabadiliko yoyote ndani yake, athari yake kubwa ni maumivu makali sababu ya kamba za misuli zilizojivuta^kuwamba nfani na juu zikihusisha ngozi na kuzuia mnyumbuliko sawa wa utanukaji wa kifua.

Mgonjwa anaweza kuathirika zaidi kisaikolojia kwa maumivu na kutokujua tatizo lake la msingi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom