magode
JF-Expert Member
- Oct 2, 2014
- 2,204
- 3,338
Wanajamvi salaam,
Ilikuwa ijumaa tar.16/10/2015. Nilikuwa naelekea kumuona mzee mmoja kiongozi wa jumuiya ndogondogo huko kwangu nnakoishi maeneo ya Mbagala.
Nikiwa njiani kabla sijafika kwa mwenyekiti, niliona pochi ya kike, njia niliyokuwa napita,haikuwa na watu wengi. Nilitaka niiache ile pochi,lakini nikaamua kuichukua, bahati mimi pia nilikuwa na begi nikaitupia kwenye begi nikaendelea na safari yangu.Nimefika kwa mwenyekiti nikaongea mambo yangu kisha nikarejea kwangu. Nilipomaliza kuoga nikaikumbuka ile pochi! Nikaifuata nikaje nayo sebuleni nikaifungua,ndani nikakuta kuna simu android ya Kichina Tecno h6 na pesa taslimu ya kiasi cha tsh.laki 4 na 700. Pia kulikuwa na karatasi ina majina ya watu na kiasi walichotoa na yote yalikuwa majina ya kike.
Ile simu ilikuwa imezimwa,nikajaribu kuiwasha haikuwaka, nikajaribu kuiweka kwenye charge ikakubali nikaiwasha ikawaka kulikuwa na simcard 2 tigo na airtel. Lkn zote zilikuwa hazisomi,yaani zilikuwa zimekufa! Zote ziliandika"sim registration failed".Kwenye call history kulikuwa kumepigwa pin,kwenye sms pin,phonebook pin..! Ktk ile karatasi yenye orodha ya majina juu ya hiyo karatasi kulikuwa na namba ya simu. Nikajaribu kuipiga haikupatikana!
Nikaizima ile simu nikaiondoa kwenye moto kisha nikavirudisha vitu vyote pamoja na ile fedha. Kiukweli sikuwa hata na wazo la kutumia chochote ktk hivyo vitu nilivyookota. Nilitaka kufanya jitihada ya kumpata muhusika kwa wakati ili aendelee na mipango yake.Nilimsimulia mke wangu mkasa mzima na dhamira yangu. Kichwani nikawa nawaza,hivi ikiwa hii pochi mwenye nayo alivamiwa na kuawa kisha wauaji wakatoweka itakuaje!? Nikipeleka police napo bila shaka maafande watagawana tu hizo fedha!
Niliendelea kuipigia ile namba niliyoikuta kwenye ile karatasi,haikuwa ikipatikana mpaka siku ya 3 ndo nikaipata.! Nikampigia akapokea mdada mwenye sauti nzuri sana,nikamsabahi kisha akaniambia samahani nilipoteza simu siku 2 zilizopita nimerudisha namba leo,nani mwenzangu!? Nikamjibu,me pia nilikuwa nakupigia simu nijue wewe nani hii namba ipo kwenye simu yangu na nimeandika mrembo.!
Huo ukawa mwanzo wa urafiki na huyo binti,tukawa tunachat kila wakati tunapopata wasaa! Sikuwahi kumueleza chochote kuhusu ile pochi. Tuliendelea kuchat na kujikuta tunazoeana sana kwenye simu hadi tukaingia kwenye kutongozana.Me ni mtu mzma kiasi nna mke na watoto lkn alivyoniuliza kuhusu mke nikamwambia sijaoa lkn nilimwambia niliwahi kuoa tukaachana lkn watoto ambao nilizaa na huyo mke nnao naishi nao..!
Yeye akaniambia ni mwalimu wa shule moja ya sekondari mkoa mpwani. Nyumbani ni mbagala na kwamba hana mume. Hapo tulikuwa hatujawahi kuonana na alinisimulia jinsi alivyopoteza pesa na simu za kitchen party ya rafiki yake ikiwa ni michango ya waalimu wenzie. Na kwamba alilazimika kukopa ili akapeleke zile pesa kwa sababu kitchen party ilikuwa siku inayofuata.
Pamoja na kunieleza hayo,sikumwambia kama mimi ndo niliikota,nilitaka nimuone kwanza. Baada ya kuzoeana sana,hatimae siku moja akaja ofisini kwangu nnapofanyia shughuli zangu za tigopesa. Dah..! Dem alikuwa mrembo hatari! Tuliongea machache pale ofisini lkn pale wateja ni wengi ikabidi nimuite kijana wangu aje akae sisi tukatoka kwa ajili ya lunch na story.
Hii ilikuwa mwezi november tar.21. Tulienda kwenye mgahawa mmoja wa wapemba pale Tandika tukapata lunch,tukapiga story za kutosha na nilipomuomba tutafute sehemu tupumzike hakuwa na shida. Nikaenda kusaka lodge kisha nikamfuata,tukafanya yetu mpaka saa 1 jioni. Kwa vile mbagala kunakuwa na foleni sana,nikaamua nimchukulie bodaboda tukaachana me nikarudi ofisini.! Tukawa tumeanza ukurasa mpya wa uhusiano wa kimapenzi.Mpaka hapo sikuwahi kumwambia kuhusu ile pochi yake ingawa niliitunza vilevile ikiwa na hela zake pamoja na simu.
Tumeendelea kuwa wapenzi kila anapokuja dar,lazima aje anione kwanza mzee wake. Mpaka hapo hajui km nimeoa. Tar.10/12/2015. Siku ya alhamis alirudi likizo rasmi. Alifika mapema tu,hii ndo siku nilipanga kumpa pochi yake.! Yeye alitangulia lodge,baadae nami nikamfuata. Baada ya kufanya yetu na story za hapa na pale,katikati ya furaha yetu nikanyanyuka na kuitoa ile pochi kisha nikamkabidhi..! Alistuka sana na furaha yote aliyokuwa nayo ikatoweka akabaki ananikodolea macho kumbe alikuwa amezimia! Nikamlaza kitandani,baada ya km dakika 8 akainuka. Alikuwa ameshaingiwa na hofu hakuamini km me ni binadamu alijua ni jini.
Niliigundua ile hali nikamwambia atulie nimweleze nilikoitoa. Nikamsimulia mwanzo mpaka mwisho..! Akawa amenielewa lakini akawa anahoji sana juu ya uaminifu wangu. Kwanini niwe mwaminifu hivyo kwake! Nikamwambia si kwake tu haya ndo maisha tunayopaswa kuishi binadamu wote.Baada ya tukio lile,binti hasikii lolote kuhusu mimi,ameshatangaza ndoa anataka nimuoe.!
Kwa sasa mpaka imekuwa kero,sina furaha nikirudi nyumbani kwangu,binti anapiga simu za mahaba kila wakati. Mke wangu akigundua sijui itakuaje!Najiuliza nikimwambia ukweli huyu teacher ataukubali!!? Ameonyesha imani ya juu sana kwangu,itakuaje nikimwambia ukweli huu utakaomuumiza? Lakini lingine nilipenda niwe nae kama mchepuko kwasababu ameonekana binti anayejitambua. Nikimwambia ukweli atakubali kuwa mchepuko.!?
Naomba mchango wa mawazo, kwa wale wanaopenda kuhukumu, karibuni pia mtoe hukumu zenu.
~magode~